Psalms 123 (BOKCV)
undefined Wimbo wa kwenda juu. 1 Ninayainua macho yangu kwako,kwako wewe ambaye kiti chako cha enzi kiko mbinguni. 2 Kama vile macho ya watumwayatazamavyo mkono wa bwana wao,kama vile macho ya mtumishi wa kikeyatazamavyo mkono wa bibi yake,ndivyo macho yetu yamtazamavyo BWANA Mungu wetu,mpaka atakapotuhurumia. 3 Uturehemu, Ee BWANA, uturehemu,kwa maana tumevumilia dharau nyingi. 4 Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi,dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno.