Psalms 124 (BOKCV)
undefined Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. 1 Kama BWANA asingalikuwa upande wetu;Israeli na aseme sasa: 2 kama BWANA asingalikuwa upande wetu,wakati watu walipotushambulia, 3 wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu,wangalitumeza tungali hai, 4 mafuriko yangalitugharikisha,maji mengi yangalitufunika, 5 maji yaendayo kasiyangalituchukua. 6 BWANA asifiwe,yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao. 7 Tumeponyoka kama ndegekutoka mtego wa mwindaji;mtego umevunjika,nasi tukaokoka. 8 Msaada wetu ni katika jina la BWANA,Muumba wa mbingu na dunia.