Psalms 89 (BOKCV)

undefined Utenzi wa Ethani Mwezrahi. 1 Nitaimba juu ya upendo mkuu wa BWANA milele;kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wakoujulikane kwa vizazi vyote. 2 Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milelena uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni. 3 Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu,nimemwapia mtumishi wangu Daudi, 4 ‘Nitaimarisha uzao wako milelena kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ” 5 Ee BWANA, mbingu zinayasifu maajabu yako,uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu. 6 Kwa kuwa ni nani katika mbinguanayeweza kulinganishwa na BWANA?Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbingunialiye kama BWANA? 7 Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana,anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka. 8 Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote,ni nani aliye kama wewe?Ee BWANA, wewe ni mwenye nguvu,na uaminifu wako unakuzunguka. 9 Wewe unatawala bahari yenye msukosuko;wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza. 10 Wewe ulimponda Rahabukama mmojawapo wa waliochinjwa;kwa mkono wako wenye nguvu,uliwatawanya adui zako. 11 Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako,uliuwekea ulimwengu msingipamoja na vyote vilivyomo. 12 Uliumba kaskazini na kusini;Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha. 13 Mkono wako umejaa uwezo;mkono wako una nguvu,mkono wako wa kuume umetukuzwa. 14 Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi;upendo na uaminifu vinakutangulia. 15 Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe,wanaotembea katika mwangawa uwepo wako, Ee BWANA. 16 Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa,wanafurahi katika haki yako. 17 Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao,kwa wema wako unatukuza pembe yetu. 18 Naam, ngao yetu ni mali ya BWANA,na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli. 19 Ulizungumza wakati fulani katika maono,kwa watu wako waaminifu, ukasema:“Nimeweka nguvu kwa shujaa,nimemwinua kijana miongoni mwa watu. 20 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu,na nimemtia mafuta yangu matakatifu. 21 Kitanga changu kitamtegemeza,hakika mkono wangu utamtia nguvu. 22 Hakuna adui atakayemtoza ushuru,hakuna mtu mwovu atakayemwonea. 23 Nitawaponda adui zake mbele zakena kuwaangamiza watesi wake. 24 Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye,kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa. 25 Nitauweka mkono wake juu ya bahari,mkono wake wa kuume juu ya mito. 26 Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu,Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’ 27 Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza,aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia. 28 Nitadumisha upendo wangu kwake milele,na agano langu naye litakuwa imara. 29 Nitaudumisha uzao wake milele,kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu. 30 “Kama wanae wataacha amri yanguna wasifuate sheria zangu, 31 kama wakihalifu maagizo yanguna kutoshika amri zangu, 32 nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo,uovu wao kwa kuwapiga, 33 lakini sitauondoa upendo wangu kwake,wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe. 34 Mimi sitavunja agano languwala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka. 35 Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu,nami sitamdanganya Daudi: 36 kwamba uzao wake utaendelea milele,na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua; 37 kitaimarishwa milele kama mwezi,shahidi mwaminifu angani.” 38 Lakini wewe umemkataa, umemdharau,umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako. 39 Umelikana agano lako na mtumishi wako,na umeinajisi taji yake mavumbini. 40 Umebomoa kuta zake zote,na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu. 41 Wote wapitao karibu wamemnyangʼanya mali zake;amekuwa dharau kwa jirani zake. 42 Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake,umewafanya watesi wake wote washangilie. 43 Umegeuza makali ya upanga wake,na hukumpa msaada katika vita. 44 Umeikomesha fahari yake,na kukiangusha kiti chake cha enzi. 45 Umezifupisha siku za ujana wake,umemfunika kwa vazi la aibu. 46 Hata lini, Ee BWANA? Utajificha milele?Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini? 47 Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka.Ni kwa ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu! 48 Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo,au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi? 49 Ee BWANA, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni,ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi? 50 Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa,jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote, 51 dhihaka ambazo kwazo adui zakowamenisimanga, Ee BWANA,ambazo kwazo wamesimangakila hatua ya mpakwa mafuta wako. 52 Msifuni BWANA milele!Amen na Amen.

In Other Versions

Psalms 89 in the ANGEFD

Psalms 89 in the ANTPNG2D

Psalms 89 in the AS21

Psalms 89 in the BAGH

Psalms 89 in the BBPNG

Psalms 89 in the BBT1E

Psalms 89 in the BDS

Psalms 89 in the BEV

Psalms 89 in the BHAD

Psalms 89 in the BIB

Psalms 89 in the BLPT

Psalms 89 in the BNT

Psalms 89 in the BNTABOOT

Psalms 89 in the BNTLV

Psalms 89 in the BOATCB

Psalms 89 in the BOATCB2

Psalms 89 in the BOBCV

Psalms 89 in the BOCNT

Psalms 89 in the BOECS

Psalms 89 in the BOGWICC

Psalms 89 in the BOHCB

Psalms 89 in the BOHCV

Psalms 89 in the BOHLNT

Psalms 89 in the BOHNTLTAL

Psalms 89 in the BOICB

Psalms 89 in the BOILNTAP

Psalms 89 in the BOITCV

Psalms 89 in the BOKCV2

Psalms 89 in the BOKHWOG

Psalms 89 in the BOKSSV

Psalms 89 in the BOLCB

Psalms 89 in the BOLCB2

Psalms 89 in the BOMCV

Psalms 89 in the BONAV

Psalms 89 in the BONCB

Psalms 89 in the BONLT

Psalms 89 in the BONUT2

Psalms 89 in the BOPLNT

Psalms 89 in the BOSCB

Psalms 89 in the BOSNC

Psalms 89 in the BOTLNT

Psalms 89 in the BOVCB

Psalms 89 in the BOYCB

Psalms 89 in the BPBB

Psalms 89 in the BPH

Psalms 89 in the BSB

Psalms 89 in the CCB

Psalms 89 in the CUV

Psalms 89 in the CUVS

Psalms 89 in the DBT

Psalms 89 in the DGDNT

Psalms 89 in the DHNT

Psalms 89 in the DNT

Psalms 89 in the ELBE

Psalms 89 in the EMTV

Psalms 89 in the ESV

Psalms 89 in the FBV

Psalms 89 in the FEB

Psalms 89 in the GGMNT

Psalms 89 in the GNT

Psalms 89 in the HARY

Psalms 89 in the HNT

Psalms 89 in the IRVA

Psalms 89 in the IRVB

Psalms 89 in the IRVG

Psalms 89 in the IRVH

Psalms 89 in the IRVK

Psalms 89 in the IRVM

Psalms 89 in the IRVM2

Psalms 89 in the IRVO

Psalms 89 in the IRVP

Psalms 89 in the IRVT

Psalms 89 in the IRVT2

Psalms 89 in the IRVU

Psalms 89 in the ISVN

Psalms 89 in the JSNT

Psalms 89 in the KAPI

Psalms 89 in the KBT1ETNIK

Psalms 89 in the KBV

Psalms 89 in the KJV

Psalms 89 in the KNFD

Psalms 89 in the LBA

Psalms 89 in the LBLA

Psalms 89 in the LNT

Psalms 89 in the LSV

Psalms 89 in the MAAL

Psalms 89 in the MBV

Psalms 89 in the MBV2

Psalms 89 in the MHNT

Psalms 89 in the MKNFD

Psalms 89 in the MNG

Psalms 89 in the MNT

Psalms 89 in the MNT2

Psalms 89 in the MRS1T

Psalms 89 in the NAA

Psalms 89 in the NASB

Psalms 89 in the NBLA

Psalms 89 in the NBS

Psalms 89 in the NBVTP

Psalms 89 in the NET2

Psalms 89 in the NIV11

Psalms 89 in the NNT

Psalms 89 in the NNT2

Psalms 89 in the NNT3

Psalms 89 in the PDDPT

Psalms 89 in the PFNT

Psalms 89 in the RMNT

Psalms 89 in the SBIAS

Psalms 89 in the SBIBS

Psalms 89 in the SBIBS2

Psalms 89 in the SBICS

Psalms 89 in the SBIDS

Psalms 89 in the SBIGS

Psalms 89 in the SBIHS

Psalms 89 in the SBIIS

Psalms 89 in the SBIIS2

Psalms 89 in the SBIIS3

Psalms 89 in the SBIKS

Psalms 89 in the SBIKS2

Psalms 89 in the SBIMS

Psalms 89 in the SBIOS

Psalms 89 in the SBIPS

Psalms 89 in the SBISS

Psalms 89 in the SBITS

Psalms 89 in the SBITS2

Psalms 89 in the SBITS3

Psalms 89 in the SBITS4

Psalms 89 in the SBIUS

Psalms 89 in the SBIVS

Psalms 89 in the SBT

Psalms 89 in the SBT1E

Psalms 89 in the SCHL

Psalms 89 in the SNT

Psalms 89 in the SUSU

Psalms 89 in the SUSU2

Psalms 89 in the SYNO

Psalms 89 in the TBIAOTANT

Psalms 89 in the TBT1E

Psalms 89 in the TBT1E2

Psalms 89 in the TFTIP

Psalms 89 in the TFTU

Psalms 89 in the TGNTATF3T

Psalms 89 in the THAI

Psalms 89 in the TNFD

Psalms 89 in the TNT

Psalms 89 in the TNTIK

Psalms 89 in the TNTIL

Psalms 89 in the TNTIN

Psalms 89 in the TNTIP

Psalms 89 in the TNTIZ

Psalms 89 in the TOMA

Psalms 89 in the TTENT

Psalms 89 in the UBG

Psalms 89 in the UGV

Psalms 89 in the UGV2

Psalms 89 in the UGV3

Psalms 89 in the VBL

Psalms 89 in the VDCC

Psalms 89 in the YALU

Psalms 89 in the YAPE

Psalms 89 in the YBVTP

Psalms 89 in the ZBP