Psalms 93 (BOKCV)
1 BWANA anatawala, amejivika utukufu; BWANA amejivika utukufutena amejivika nguvu.Dunia imewekwa imara,haitaondoshwa. 2 Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;wewe umekuwako tangu milele. 3 Bahari zimeinua, Ee BWANA,bahari zimeinua sauti zake;bahari zimeinua sauti za mawimbi yake. 4 Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: BWANA aishiye juu sana ni mkuu. 5 Ee BWANA, sheria zako ni imara;utakatifu umepamba nyumba yakopasipo mwisho.