1 Chronicles 17 (BOKCV)
1 Baada ya Daudi kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, akamwambia nabii Nathani, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mierezi, wakati Sanduku la Agano la BWANA liko ndani ya hema.” 2 Nathani akamjibu Daudi, “Lolote ulilo nalo moyoni mwako litende, kwa maana Mungu yu pamoja nawe.” 3 Usiku ule neno la Mungu likamjia Nathani, kusema: 4 “Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo BWANA: Wewe hutanijengea mimi nyumba ili nikae humo. 5 Mimi sijakaa ndani ya nyumba tangu siku ile niliyowatoa Israeli kutoka Misri mpaka leo. Nimehama kutoka hema moja hadi jingine na kutoka mahali pamoja hadi pengine. 6 Je, popote nilipokwenda pamoja na Waisraeli wote, wakati wowote nilimwambia kiongozi yeyote niliyemwagiza kuwachunga watu wangu, kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?’ 7 “Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: Nilikuchukua machungani na kutoka kuandama kondoo ili uwatawale watu wangu Israeli. 8 Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani. 9 Nami nitawapatia watu wangu Israeli mahali na nitawapa ili wawe na mahali pao wenyewe pa kuishi na wasisumbuliwe tena. Watu waovu hawatawaonea tena, kama walivyofanya mwanzoni, 10 na ambavyo wamefanya siku zote tangu nilipowachagua viongozi kwa ajili ya watu wangu Israeli. Pia nitawatiisha adui zenu wote.“ ‘Pamoja na hayo ninakuambia kwamba BWANA atakujengea nyumba: 11 Wakati wako utakapokuwa umekwisha, nawe ukawa umekwenda kukaa na baba zako, nitamwinua mzao wako aingie mahali pako kuwa mfalme, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitaufanya imara ufalme wake. 12 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili yangu, nami nitakifanya imara kiti cha ufalme wake milele. 13 Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Kamwe sitaondoa upendo wangu kwake, kama nilivyouondoa kwa yeye aliyekutangulia. 14 Nitamweka juu ya nyumba yangu na ufalme wangu milele; kiti chake cha enzi nitakifanya imara milele.’ ” 15 Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya. 16 Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za BWANA, akasema:“Mimi ni nani, Ee BWANA Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo? 17 Kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Mungu, umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Umeniangalia kama mtu aliyetukuka kuliko watu wote, Ee BWANA Mungu. 18 “Daudi aweza kukuambia nini zaidi kuhusu kumheshimu mtumishi wako? Kwa maana wewe unamjua mtumishi wako, 19 Ee BWANA Mungu. Kwa ajili ya mtumishi wako, tena sawasawa na mapenzi yako, umefanya jambo hili kubwa sana na kujulisha ahadi hizi zote zilizo kubwa sana. 20 “Hakuna aliye kama wewe, Ee BWANA Mungu, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe. 21 Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli: taifa pekee duniani ambalo Mungu wake alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe na kujifanyia jina kwa ajili yake mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri? 22 Uliwafanya watu wako Israeli kuwa watu wako wewe mwenyewe milele, nawe, Ee BWANA Mungu, umekuwa Mungu wao. 23 “Sasa basi, BWANA ahadi uliyoweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake na uithibitishe milele. Fanya kama ulivyoahidi, 24 ili ithibitike na jina lako litakuwa kuu milele. Kisha watu watasema, ‘BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu aliye juu ya Israeli, ndiye Mungu wa Israeli.’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itafanywa imara mbele zako. 25 “Wewe, Mungu wangu, umemfunulia mtumishi wako Daudi kwamba utamjengea yeye nyumba. Hivyo mtumishi wako amekuwa na ujasiri wa kukuomba maombi haya. 26 Ee BWANA, wewe ndiwe Mungu! Umemwahidi mtumishi wako mambo haya mazuri. 27 Basi imekupendeza kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili idumu milele machoni pako; kwa ajili yako, Ee BWANA, umeibariki, nayo itabarikiwa milele.”
In Other Versions
1 Chronicles 17 in the ANGEFD
1 Chronicles 17 in the ANTPNG2D
1 Chronicles 17 in the AS21
1 Chronicles 17 in the BAGH
1 Chronicles 17 in the BBPNG
1 Chronicles 17 in the BBT1E
1 Chronicles 17 in the BDS
1 Chronicles 17 in the BEV
1 Chronicles 17 in the BHAD
1 Chronicles 17 in the BIB
1 Chronicles 17 in the BLPT
1 Chronicles 17 in the BNT
1 Chronicles 17 in the BNTABOOT
1 Chronicles 17 in the BNTLV
1 Chronicles 17 in the BOATCB
1 Chronicles 17 in the BOATCB2
1 Chronicles 17 in the BOBCV
1 Chronicles 17 in the BOCNT
1 Chronicles 17 in the BOECS
1 Chronicles 17 in the BOGWICC
1 Chronicles 17 in the BOHCB
1 Chronicles 17 in the BOHCV
1 Chronicles 17 in the BOHLNT
1 Chronicles 17 in the BOHNTLTAL
1 Chronicles 17 in the BOICB
1 Chronicles 17 in the BOILNTAP
1 Chronicles 17 in the BOITCV
1 Chronicles 17 in the BOKCV2
1 Chronicles 17 in the BOKHWOG
1 Chronicles 17 in the BOKSSV
1 Chronicles 17 in the BOLCB
1 Chronicles 17 in the BOLCB2
1 Chronicles 17 in the BOMCV
1 Chronicles 17 in the BONAV
1 Chronicles 17 in the BONCB
1 Chronicles 17 in the BONLT
1 Chronicles 17 in the BONUT2
1 Chronicles 17 in the BOPLNT
1 Chronicles 17 in the BOSCB
1 Chronicles 17 in the BOSNC
1 Chronicles 17 in the BOTLNT
1 Chronicles 17 in the BOVCB
1 Chronicles 17 in the BOYCB
1 Chronicles 17 in the BPBB
1 Chronicles 17 in the BPH
1 Chronicles 17 in the BSB
1 Chronicles 17 in the CCB
1 Chronicles 17 in the CUV
1 Chronicles 17 in the CUVS
1 Chronicles 17 in the DBT
1 Chronicles 17 in the DGDNT
1 Chronicles 17 in the DHNT
1 Chronicles 17 in the DNT
1 Chronicles 17 in the ELBE
1 Chronicles 17 in the EMTV
1 Chronicles 17 in the ESV
1 Chronicles 17 in the FBV
1 Chronicles 17 in the FEB
1 Chronicles 17 in the GGMNT
1 Chronicles 17 in the GNT
1 Chronicles 17 in the HARY
1 Chronicles 17 in the HNT
1 Chronicles 17 in the IRVA
1 Chronicles 17 in the IRVB
1 Chronicles 17 in the IRVG
1 Chronicles 17 in the IRVH
1 Chronicles 17 in the IRVK
1 Chronicles 17 in the IRVM
1 Chronicles 17 in the IRVM2
1 Chronicles 17 in the IRVO
1 Chronicles 17 in the IRVP
1 Chronicles 17 in the IRVT
1 Chronicles 17 in the IRVT2
1 Chronicles 17 in the IRVU
1 Chronicles 17 in the ISVN
1 Chronicles 17 in the JSNT
1 Chronicles 17 in the KAPI
1 Chronicles 17 in the KBT1ETNIK
1 Chronicles 17 in the KBV
1 Chronicles 17 in the KJV
1 Chronicles 17 in the KNFD
1 Chronicles 17 in the LBA
1 Chronicles 17 in the LBLA
1 Chronicles 17 in the LNT
1 Chronicles 17 in the LSV
1 Chronicles 17 in the MAAL
1 Chronicles 17 in the MBV
1 Chronicles 17 in the MBV2
1 Chronicles 17 in the MHNT
1 Chronicles 17 in the MKNFD
1 Chronicles 17 in the MNG
1 Chronicles 17 in the MNT
1 Chronicles 17 in the MNT2
1 Chronicles 17 in the MRS1T
1 Chronicles 17 in the NAA
1 Chronicles 17 in the NASB
1 Chronicles 17 in the NBLA
1 Chronicles 17 in the NBS
1 Chronicles 17 in the NBVTP
1 Chronicles 17 in the NET2
1 Chronicles 17 in the NIV11
1 Chronicles 17 in the NNT
1 Chronicles 17 in the NNT2
1 Chronicles 17 in the NNT3
1 Chronicles 17 in the PDDPT
1 Chronicles 17 in the PFNT
1 Chronicles 17 in the RMNT
1 Chronicles 17 in the SBIAS
1 Chronicles 17 in the SBIBS
1 Chronicles 17 in the SBIBS2
1 Chronicles 17 in the SBICS
1 Chronicles 17 in the SBIDS
1 Chronicles 17 in the SBIGS
1 Chronicles 17 in the SBIHS
1 Chronicles 17 in the SBIIS
1 Chronicles 17 in the SBIIS2
1 Chronicles 17 in the SBIIS3
1 Chronicles 17 in the SBIKS
1 Chronicles 17 in the SBIKS2
1 Chronicles 17 in the SBIMS
1 Chronicles 17 in the SBIOS
1 Chronicles 17 in the SBIPS
1 Chronicles 17 in the SBISS
1 Chronicles 17 in the SBITS
1 Chronicles 17 in the SBITS2
1 Chronicles 17 in the SBITS3
1 Chronicles 17 in the SBITS4
1 Chronicles 17 in the SBIUS
1 Chronicles 17 in the SBIVS
1 Chronicles 17 in the SBT
1 Chronicles 17 in the SBT1E
1 Chronicles 17 in the SCHL
1 Chronicles 17 in the SNT
1 Chronicles 17 in the SUSU
1 Chronicles 17 in the SUSU2
1 Chronicles 17 in the SYNO
1 Chronicles 17 in the TBIAOTANT
1 Chronicles 17 in the TBT1E
1 Chronicles 17 in the TBT1E2
1 Chronicles 17 in the TFTIP
1 Chronicles 17 in the TFTU
1 Chronicles 17 in the TGNTATF3T
1 Chronicles 17 in the THAI
1 Chronicles 17 in the TNFD
1 Chronicles 17 in the TNT
1 Chronicles 17 in the TNTIK
1 Chronicles 17 in the TNTIL
1 Chronicles 17 in the TNTIN
1 Chronicles 17 in the TNTIP
1 Chronicles 17 in the TNTIZ
1 Chronicles 17 in the TOMA
1 Chronicles 17 in the TTENT
1 Chronicles 17 in the UBG
1 Chronicles 17 in the UGV
1 Chronicles 17 in the UGV2
1 Chronicles 17 in the UGV3
1 Chronicles 17 in the VBL
1 Chronicles 17 in the VDCC
1 Chronicles 17 in the YALU
1 Chronicles 17 in the YAPE
1 Chronicles 17 in the YBVTP
1 Chronicles 17 in the ZBP