1 Kings 4 (BOKCV)

1 Basi Mfalme Solomoni akatawala Israeli yote. 2 Hawa ndio waliokuwa maafisa wake wakuu: Kuhani: Azaria mwana wa Sadoki; 3 Elihorefu na Ahiya, wana wa Shisha: waandishi;Yehoshafati mwana wa Ahiludi: karani; 4 Benaya mwana wa Yehoyada: jemadari mkuu wa jeshi;Sadoki na Abiathari: makuhani; 5 Azaria mwana wa Nathani: kiongozi wa maafisa wa wilaya;Zabudi mwana wa Nathani: kuhani na mshauri binafsi wa mfalme; 6 Ahishari: msimamizi wa jumba la kifalme;Adoniramu mwana wa Abda: msimamizi wa kazi za kulazimisha. 7 Pia Solomoni alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioleta mahitaji kwa mfalme na kwa watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka. 8 Majina yao ni haya: Ben-Huri: katika nchi ya vilima ya Efraimu; 9 Ben-Dekeri: katika Makasi, Shaalbimu, Beth-Shemeshi na Elon-Bethhanani; 10 Ben-Hesedi: katika Arubothi (Soko na nchi yote ya Heferi zilikuwa zake); 11 Ben-Abinadabu: katika Nafoth-Dori (alimwoa Tafathi binti Solomoni); 12 Baana mwana wa Ahiludi: katika Taanaki na Megido, na katika Beth-Shani yote karibu na Sarethani chini ya Yezreeli, kuanzia Beth-Shani hadi Abel-Mehola kupita hadi Yokmeamu; 13 Ben-Geberi: katika Ramoth-Gileadi (makao ya Yairi mwana wa Manase katika Gileadi ilikuwa miji yake, pamoja na wilaya ya Argobu katika Bashani na miji yake mikubwa sitini yenye kuzungukwa na kuta zenye makomeo ya shaba); 14 Ahinadabu mwana wa Ido: katika Mahanaimu; 15 Ahimaasi: katika Naftali (alikuwa amemwoa Basemathi binti Solomoni); 16 Baana mwana wa Hushai: katika Asheri na katika Bealothi; 17 Yehoshafati mwana wa Parua: katika Isakari; 18 Shimei mwana wa Ela: katika Benyamini; 19 Geberi mwana wa Uri: katika Gileadi (nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani). Naye alikuwa ndiye mtawala pekee katika eneo hilo. 20 Watu wa Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani; walikula, wakanywa na kufurahi. 21 Mfalme Solomoni akatawala katika falme zote kuanzia Mto Frati hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Solomoni, siku zote za maisha yake. 22 Mahitaji ya Solomoni ya kila siku yalikuwa kori thelathini za unga laini, kori sitini za unga wa kawaida. 23 Ngʼombe kumi wa zizini, ngʼombe ishirini wa malisho, kondoo na mbuzi mia moja, pamoja na ayala, paa, kulungu na kuku wazuri sana. 24 Kwa kuwa Solomoni alitawala falme zote magharibi ya mto, kuanzia Tifsa hadi Gaza, naye akawa na amani pande zote. 25 Wakati wa maisha ya Solomoni Yuda na Israeli, kuanzia Dani mpaka Beer-Sheba, wakaishi salama kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake. 26 Solomoni alikuwa na mabanda 4,000 ya magari ya vita, na farasi 12,000. 27 Maafisa wa eneo hilo, kila mmoja katika mwezi wake, walileta mahitaji kwa ajili ya Mfalme Solomoni na wote waliokula mezani mwa mfalme. Walihakikisha kuwa hakuna chochote kilichopungua. 28 Pia walileta sehemu walizopangiwa za shayiri na majani kwa ajili ya farasi wavutao magari na farasi wengine mahali palipostahili. 29 Mungu akampa Solomoni hekima na akili kubwa, pia ufahamu mpana usiopimika kama mchanga ulioko pwani ya bahari. 30 Hekima ya Solomoni ilikuwa kubwa kuliko hekima ya watu wote wa Mashariki na kubwa kuliko hekima yote ya Misri. 31 Alikuwa na hekima kuliko kila mwandishi, akiwemo Ethani Mwezrahi: kuliko Hemani, Kalkoli na Darda, wana wa Maholi. Umaarufu wake ukaenea kwa mataifa yote yaliyomzunguka. 32 Akanena mithali 3,000 na nyimbo zake zilikuwa 1,005. 33 Akaelezea maisha ya mimea kuanzia mwerezi wa Lebanoni hadi hisopo iotayo ukutani. Pia akafundisha kuhusu wanyama na ndege, wanyama wenye damu baridi, wakiwemo samaki. 34 Watu wa mataifa yote wakaja kusikiliza hekima ya Solomoni, waliotumwa na wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamesikia juu ya hekima yake.

In Other Versions

1 Kings 4 in the ANGEFD

1 Kings 4 in the ANTPNG2D

1 Kings 4 in the AS21

1 Kings 4 in the BAGH

1 Kings 4 in the BBPNG

1 Kings 4 in the BBT1E

1 Kings 4 in the BDS

1 Kings 4 in the BEV

1 Kings 4 in the BHAD

1 Kings 4 in the BIB

1 Kings 4 in the BLPT

1 Kings 4 in the BNT

1 Kings 4 in the BNTABOOT

1 Kings 4 in the BNTLV

1 Kings 4 in the BOATCB

1 Kings 4 in the BOATCB2

1 Kings 4 in the BOBCV

1 Kings 4 in the BOCNT

1 Kings 4 in the BOECS

1 Kings 4 in the BOGWICC

1 Kings 4 in the BOHCB

1 Kings 4 in the BOHCV

1 Kings 4 in the BOHLNT

1 Kings 4 in the BOHNTLTAL

1 Kings 4 in the BOICB

1 Kings 4 in the BOILNTAP

1 Kings 4 in the BOITCV

1 Kings 4 in the BOKCV2

1 Kings 4 in the BOKHWOG

1 Kings 4 in the BOKSSV

1 Kings 4 in the BOLCB

1 Kings 4 in the BOLCB2

1 Kings 4 in the BOMCV

1 Kings 4 in the BONAV

1 Kings 4 in the BONCB

1 Kings 4 in the BONLT

1 Kings 4 in the BONUT2

1 Kings 4 in the BOPLNT

1 Kings 4 in the BOSCB

1 Kings 4 in the BOSNC

1 Kings 4 in the BOTLNT

1 Kings 4 in the BOVCB

1 Kings 4 in the BOYCB

1 Kings 4 in the BPBB

1 Kings 4 in the BPH

1 Kings 4 in the BSB

1 Kings 4 in the CCB

1 Kings 4 in the CUV

1 Kings 4 in the CUVS

1 Kings 4 in the DBT

1 Kings 4 in the DGDNT

1 Kings 4 in the DHNT

1 Kings 4 in the DNT

1 Kings 4 in the ELBE

1 Kings 4 in the EMTV

1 Kings 4 in the ESV

1 Kings 4 in the FBV

1 Kings 4 in the FEB

1 Kings 4 in the GGMNT

1 Kings 4 in the GNT

1 Kings 4 in the HARY

1 Kings 4 in the HNT

1 Kings 4 in the IRVA

1 Kings 4 in the IRVB

1 Kings 4 in the IRVG

1 Kings 4 in the IRVH

1 Kings 4 in the IRVK

1 Kings 4 in the IRVM

1 Kings 4 in the IRVM2

1 Kings 4 in the IRVO

1 Kings 4 in the IRVP

1 Kings 4 in the IRVT

1 Kings 4 in the IRVT2

1 Kings 4 in the IRVU

1 Kings 4 in the ISVN

1 Kings 4 in the JSNT

1 Kings 4 in the KAPI

1 Kings 4 in the KBT1ETNIK

1 Kings 4 in the KBV

1 Kings 4 in the KJV

1 Kings 4 in the KNFD

1 Kings 4 in the LBA

1 Kings 4 in the LBLA

1 Kings 4 in the LNT

1 Kings 4 in the LSV

1 Kings 4 in the MAAL

1 Kings 4 in the MBV

1 Kings 4 in the MBV2

1 Kings 4 in the MHNT

1 Kings 4 in the MKNFD

1 Kings 4 in the MNG

1 Kings 4 in the MNT

1 Kings 4 in the MNT2

1 Kings 4 in the MRS1T

1 Kings 4 in the NAA

1 Kings 4 in the NASB

1 Kings 4 in the NBLA

1 Kings 4 in the NBS

1 Kings 4 in the NBVTP

1 Kings 4 in the NET2

1 Kings 4 in the NIV11

1 Kings 4 in the NNT

1 Kings 4 in the NNT2

1 Kings 4 in the NNT3

1 Kings 4 in the PDDPT

1 Kings 4 in the PFNT

1 Kings 4 in the RMNT

1 Kings 4 in the SBIAS

1 Kings 4 in the SBIBS

1 Kings 4 in the SBIBS2

1 Kings 4 in the SBICS

1 Kings 4 in the SBIDS

1 Kings 4 in the SBIGS

1 Kings 4 in the SBIHS

1 Kings 4 in the SBIIS

1 Kings 4 in the SBIIS2

1 Kings 4 in the SBIIS3

1 Kings 4 in the SBIKS

1 Kings 4 in the SBIKS2

1 Kings 4 in the SBIMS

1 Kings 4 in the SBIOS

1 Kings 4 in the SBIPS

1 Kings 4 in the SBISS

1 Kings 4 in the SBITS

1 Kings 4 in the SBITS2

1 Kings 4 in the SBITS3

1 Kings 4 in the SBITS4

1 Kings 4 in the SBIUS

1 Kings 4 in the SBIVS

1 Kings 4 in the SBT

1 Kings 4 in the SBT1E

1 Kings 4 in the SCHL

1 Kings 4 in the SNT

1 Kings 4 in the SUSU

1 Kings 4 in the SUSU2

1 Kings 4 in the SYNO

1 Kings 4 in the TBIAOTANT

1 Kings 4 in the TBT1E

1 Kings 4 in the TBT1E2

1 Kings 4 in the TFTIP

1 Kings 4 in the TFTU

1 Kings 4 in the TGNTATF3T

1 Kings 4 in the THAI

1 Kings 4 in the TNFD

1 Kings 4 in the TNT

1 Kings 4 in the TNTIK

1 Kings 4 in the TNTIL

1 Kings 4 in the TNTIN

1 Kings 4 in the TNTIP

1 Kings 4 in the TNTIZ

1 Kings 4 in the TOMA

1 Kings 4 in the TTENT

1 Kings 4 in the UBG

1 Kings 4 in the UGV

1 Kings 4 in the UGV2

1 Kings 4 in the UGV3

1 Kings 4 in the VBL

1 Kings 4 in the VDCC

1 Kings 4 in the YALU

1 Kings 4 in the YAPE

1 Kings 4 in the YBVTP

1 Kings 4 in the ZBP