2 Kings 16 (BOKCV)
1 Katika mwaka wa kumi na saba wa utawala wa Peka mwana wa Remalia, Ahazi mwana wa Yothamu mfalme wa Yuda alianza kutawala. 2 Ahazi alikuwa na miaka ishirini alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na sita. Tofauti na Daudi baba yake, hakufanya yaliyo mema machoni pa Bwana, Mungu wake. 3 Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, na hata akamtoa mwanawe kafara katika moto, akifuata njia za machukizo za mataifa ambayo BWANA alikuwa ameyafukuza mbele ya Waisraeli. 4 Akatoa kafara na kufukiza uvumba katika mahali pa juu pa kuabudia miungu, juu ya vilima, na chini ya kila mti uliotanda. 5 Kisha Resini mfalme wa Aramu na Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli wakaondoka kwenda kupigana dhidi ya Yerusalemu na kumzunguka Ahazi kwa jeshi, lakini hawakuweza kumshinda. 6 Wakati ule, Resini mfalme wa Aramu akaurudisha Elathi kwa Aramu kwa kuwafukuza watu wa Yuda. Kisha Waedomu wakahamia Elathi, nao wanaishi huko mpaka leo. 7 Ahazi akatuma wajumbe kumwambia Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru kwamba, “Mimi ni mtumishi na mtumwa wako. Njoo na uniokoe kutoka mkononi mwa mfalme wa Aramu na wa mfalme wa Israeli, ambao wananishambulia.” 8 Naye Ahazi akachukua fedha na dhahabu zilizopatikana ndani ya Hekalu la BWANA na katika hazina ya jumba la mfalme, na kuzituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru. 9 Mfalme wa Ashuru akamwitikia kwa kushambulia Dameski na kuiteka. Akawahamishia wenyeji wake huko Kiri, na kumuua Resini. 10 Kisha Mfalme Ahazi akaenda Dameski kukutana na Tiglath-Pileseri wa Ashuru. Akaona madhabahu huko Dameski, naye akamtumia Uria kuhani mchoro wa hayo madhabahu, pamoja na maelezo ya mpango kamili wa ujenzi wake. 11 Kwa hiyo Uria kuhani akajenga madhabahu kulingana na mipango yote ambayo Mfalme Ahazi alikuwa ameituma kutoka Dameski, na akamaliza ujenzi kabla ya Mfalme Ahazi kurudi. 12 Mfalme aliporudi kutoka Dameski na kuona hayo madhabahu, akayasogelea na kutoa sadaka juu yake. 13 Akatoa sadaka yake ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka, akamimina sadaka ya kinywaji na kunyunyizia damu ya sadaka zake za amani juu ya hayo madhabahu. 14 Mfalme Ahazi akayaondoa madhabahu ya zamani ya shaba kutoka hapo mbele ya Hekalu la BWANA, yaliyokuwa yamesimama kati ya ingilio la Hekalu na hayo madhabahu mapya, naye akayaweka upande wa kaskazini mwa hayo madhabahu mapya. 15 Ndipo Mfalme Ahazi akatoa amri zifuatazo kwa Uria kuhani: “Juu ya hayo madhabahu kubwa mapya, toa sadaka ya asubuhi ya kuteketezwa na sadaka ya jioni ya nafaka, sadaka ya mfalme ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, sadaka ya kuteketezwa ya watu wote wa nchi, pamoja na sadaka yao ya nafaka na sadaka yao ya kinywaji. Unyunyize juu ya hayo madhabahu damu yote ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu. Lakini mimi nitatumia hayo madhabahu ya zamani ya shaba kwa ajili ya kutafuta uongozi.” 16 Naye Uria kuhani akafanya kama Mfalme Ahazi alivyoagiza. 17 Mfalme Ahazi akaondoa mbao za pembeni na kuondoa masinia kwenye vile vishikilio vilivyohamishika. Akaondoa ile Bahari kutoka kwenye mafahali wa shaba walioishikilia, na kuiweka kwenye kitako cha jiwe. 18 Kwa heshima ya mfalme wa Ashuru, akaliondoa pia pazia la Sabato lililokuwa limewekwa ndani ya Hekalu, na akaondoa ile njia ya kifalme ya kuingia kwenye Hekalu la BWANA. 19 Matukio mengine ya utawala wa Ahazi na yale aliyoyafanya, je hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 20 Ahazi akalala na baba zake, naye akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Naye Hezekia mwanawe akawa mfalme baada yake.
In Other Versions
2 Kings 16 in the ANGEFD
2 Kings 16 in the ANTPNG2D
2 Kings 16 in the AS21
2 Kings 16 in the BAGH
2 Kings 16 in the BBPNG
2 Kings 16 in the BBT1E
2 Kings 16 in the BDS
2 Kings 16 in the BEV
2 Kings 16 in the BHAD
2 Kings 16 in the BIB
2 Kings 16 in the BLPT
2 Kings 16 in the BNT
2 Kings 16 in the BNTABOOT
2 Kings 16 in the BNTLV
2 Kings 16 in the BOATCB
2 Kings 16 in the BOATCB2
2 Kings 16 in the BOBCV
2 Kings 16 in the BOCNT
2 Kings 16 in the BOECS
2 Kings 16 in the BOGWICC
2 Kings 16 in the BOHCB
2 Kings 16 in the BOHCV
2 Kings 16 in the BOHLNT
2 Kings 16 in the BOHNTLTAL
2 Kings 16 in the BOICB
2 Kings 16 in the BOILNTAP
2 Kings 16 in the BOITCV
2 Kings 16 in the BOKCV2
2 Kings 16 in the BOKHWOG
2 Kings 16 in the BOKSSV
2 Kings 16 in the BOLCB
2 Kings 16 in the BOLCB2
2 Kings 16 in the BOMCV
2 Kings 16 in the BONAV
2 Kings 16 in the BONCB
2 Kings 16 in the BONLT
2 Kings 16 in the BONUT2
2 Kings 16 in the BOPLNT
2 Kings 16 in the BOSCB
2 Kings 16 in the BOSNC
2 Kings 16 in the BOTLNT
2 Kings 16 in the BOVCB
2 Kings 16 in the BOYCB
2 Kings 16 in the BPBB
2 Kings 16 in the BPH
2 Kings 16 in the BSB
2 Kings 16 in the CCB
2 Kings 16 in the CUV
2 Kings 16 in the CUVS
2 Kings 16 in the DBT
2 Kings 16 in the DGDNT
2 Kings 16 in the DHNT
2 Kings 16 in the DNT
2 Kings 16 in the ELBE
2 Kings 16 in the EMTV
2 Kings 16 in the ESV
2 Kings 16 in the FBV
2 Kings 16 in the FEB
2 Kings 16 in the GGMNT
2 Kings 16 in the GNT
2 Kings 16 in the HARY
2 Kings 16 in the HNT
2 Kings 16 in the IRVA
2 Kings 16 in the IRVB
2 Kings 16 in the IRVG
2 Kings 16 in the IRVH
2 Kings 16 in the IRVK
2 Kings 16 in the IRVM
2 Kings 16 in the IRVM2
2 Kings 16 in the IRVO
2 Kings 16 in the IRVP
2 Kings 16 in the IRVT
2 Kings 16 in the IRVT2
2 Kings 16 in the IRVU
2 Kings 16 in the ISVN
2 Kings 16 in the JSNT
2 Kings 16 in the KAPI
2 Kings 16 in the KBT1ETNIK
2 Kings 16 in the KBV
2 Kings 16 in the KJV
2 Kings 16 in the KNFD
2 Kings 16 in the LBA
2 Kings 16 in the LBLA
2 Kings 16 in the LNT
2 Kings 16 in the LSV
2 Kings 16 in the MAAL
2 Kings 16 in the MBV
2 Kings 16 in the MBV2
2 Kings 16 in the MHNT
2 Kings 16 in the MKNFD
2 Kings 16 in the MNG
2 Kings 16 in the MNT
2 Kings 16 in the MNT2
2 Kings 16 in the MRS1T
2 Kings 16 in the NAA
2 Kings 16 in the NASB
2 Kings 16 in the NBLA
2 Kings 16 in the NBS
2 Kings 16 in the NBVTP
2 Kings 16 in the NET2
2 Kings 16 in the NIV11
2 Kings 16 in the NNT
2 Kings 16 in the NNT2
2 Kings 16 in the NNT3
2 Kings 16 in the PDDPT
2 Kings 16 in the PFNT
2 Kings 16 in the RMNT
2 Kings 16 in the SBIAS
2 Kings 16 in the SBIBS
2 Kings 16 in the SBIBS2
2 Kings 16 in the SBICS
2 Kings 16 in the SBIDS
2 Kings 16 in the SBIGS
2 Kings 16 in the SBIHS
2 Kings 16 in the SBIIS
2 Kings 16 in the SBIIS2
2 Kings 16 in the SBIIS3
2 Kings 16 in the SBIKS
2 Kings 16 in the SBIKS2
2 Kings 16 in the SBIMS
2 Kings 16 in the SBIOS
2 Kings 16 in the SBIPS
2 Kings 16 in the SBISS
2 Kings 16 in the SBITS
2 Kings 16 in the SBITS2
2 Kings 16 in the SBITS3
2 Kings 16 in the SBITS4
2 Kings 16 in the SBIUS
2 Kings 16 in the SBIVS
2 Kings 16 in the SBT
2 Kings 16 in the SBT1E
2 Kings 16 in the SCHL
2 Kings 16 in the SNT
2 Kings 16 in the SUSU
2 Kings 16 in the SUSU2
2 Kings 16 in the SYNO
2 Kings 16 in the TBIAOTANT
2 Kings 16 in the TBT1E
2 Kings 16 in the TBT1E2
2 Kings 16 in the TFTIP
2 Kings 16 in the TFTU
2 Kings 16 in the TGNTATF3T
2 Kings 16 in the THAI
2 Kings 16 in the TNFD
2 Kings 16 in the TNT
2 Kings 16 in the TNTIK
2 Kings 16 in the TNTIL
2 Kings 16 in the TNTIN
2 Kings 16 in the TNTIP
2 Kings 16 in the TNTIZ
2 Kings 16 in the TOMA
2 Kings 16 in the TTENT
2 Kings 16 in the UBG
2 Kings 16 in the UGV
2 Kings 16 in the UGV2
2 Kings 16 in the UGV3
2 Kings 16 in the VBL
2 Kings 16 in the VDCC
2 Kings 16 in the YALU
2 Kings 16 in the YAPE
2 Kings 16 in the YBVTP
2 Kings 16 in the ZBP