Exodus 7 (BOKCV)

1 Kisha BWANA akamwambia Mose, “Tazama, nimekufanya kuwa kama Mungu kwa Farao, naye Aroni, huyo ndugu yako, atakuwa nabii wako. 2 Utasema kila kitu nitakachokuagiza, naye Aroni ndugu yako atamwambia Farao awaachie Waisraeli watoke katika nchi yake. 3 Lakini nitaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu. Ingawa nitazidisha ishara na maajabu katika Misri, 4 hatawasikiliza. Kisha nitaupeleka mkono wangu juu ya Misri, na kwa matendo makuu ya hukumu nitavitoa vikundi vyangu, watu wangu Waisraeli. 5 Nao Wamisri watajua kuwa Mimi ndimi BWANA nitakapounyoosha mkono wangu dhidi ya Misri na kuwatoa Waisraeli watoke humo.” 6 Mose na Aroni wakafanya sawasawa kama vile BWANA alivyowaagiza. 7 Mose alikuwa na umri wa miaka themanini na Aroni alikuwa na umri wa miaka themanini na mitatu walipozungumza na Farao. 8 BWANA akamwambia Mose na Aroni, 9 “Farao atakapowaambia, ‘Fanyeni muujiza,’ basi mwambie Aroni, ‘Chukua fimbo yako na uitupe chini mbele ya Farao,’ nayo fimbo itakuwa nyoka.” 10 Ndipo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao wakafanya sawasawa kama vile BWANA alivyoagiza. Aroni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka. 11 Farao naye akawaita watu wenye maarifa na wachawi na waganga wa Kimisri, nao wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao. 12 Kila mmoja alitupa fimbo yake chini, nayo ikawa nyoka. Lakini fimbo ya Aroni ikazimeza zile fimbo zao. 13 Hata hivyo moyo wa Farao ukawa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vile BWANA alivyokuwa amesema. 14 Kisha BWANA akamwambia Mose, “Moyo wa Farao ni mgumu, anakataa kuwaachia watu kuondoka. 15 Nenda kwa Farao asubuhi wakati anapokwenda mtoni. Ngoja ukingoni mwa Naili ili uonane naye, na uchukue mkononi mwako fimbo ile iliyobadilishwa kuwa nyoka. 16 Kisha umwambie, ‘BWANA, Mungu wa Waebrania, amenituma nikuambie: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu jangwani. Lakini hadi sasa hujasikiliza. 17 Hili ndilo BWANA asemalo: Kwa hili utajua kuwa Mimi ndimi BWANA: Fimbo iliyo mkononi mwangu nitapiga nayo maji ya Naili nayo yatabadilika kuwa damu. 18 Samaki waliomo katika Mto Naili watakufa, nao mto utanuka vibaya, Wamisri hawataweza kunywa hayo maji yake.’ ” 19 BWANA akamwambia Mose, “Mwambie Aroni, ‘Chukua ile fimbo yako unyooshe mkono wako juu ya maji ya Misri, juu ya chemchemi na mifereji, juu ya madimbwi na mabwawa yote,’ navyo vitabadilika kuwa damu. Damu itakuwa kila mahali katika Misri, hata kwenye vyombo vya miti na vya mawe.” 20 Mose na Aroni wakafanya kama vile BWANA alivyokuwa amewaagiza. Akainua fimbo yake machoni pa Farao na maafisa wake na kuyapiga maji ya Mto Naili, na maji yote yakabadilika kuwa damu. 21 Samaki katika Mto Naili wakafa, nao mto ukanuka vibaya sana kiasi kwamba Wamisri hawakuweza kunywa maji yake. Damu ilikuwa kila mahali katika nchi ya Misri. 22 Lakini waganga wa Misri kwa kutumia siri ya uganga wao wakafanya vivyo hivyo, nao moyo wa Farao ukawa mgumu, hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama vile BWANA alivyokuwa amesema. 23 Badala yake, Farao akageuka, akaenda kwenye jumba lake la kifalme, wala hakulitia hili moyoni. 24 Nao Wamisri wote wakachimba kandokando ya Mto Naili kupata maji ya kunywa, kwa sababu hawakuweza kunywa maji ya mto. 25 Zilipita siku saba baada ya BWANA kuyapiga maji ya Mto Naili.

In Other Versions

Exodus 7 in the ANGEFD

Exodus 7 in the ANTPNG2D

Exodus 7 in the AS21

Exodus 7 in the BAGH

Exodus 7 in the BBPNG

Exodus 7 in the BBT1E

Exodus 7 in the BDS

Exodus 7 in the BEV

Exodus 7 in the BHAD

Exodus 7 in the BIB

Exodus 7 in the BLPT

Exodus 7 in the BNT

Exodus 7 in the BNTABOOT

Exodus 7 in the BNTLV

Exodus 7 in the BOATCB

Exodus 7 in the BOATCB2

Exodus 7 in the BOBCV

Exodus 7 in the BOCNT

Exodus 7 in the BOECS

Exodus 7 in the BOGWICC

Exodus 7 in the BOHCB

Exodus 7 in the BOHCV

Exodus 7 in the BOHLNT

Exodus 7 in the BOHNTLTAL

Exodus 7 in the BOICB

Exodus 7 in the BOILNTAP

Exodus 7 in the BOITCV

Exodus 7 in the BOKCV2

Exodus 7 in the BOKHWOG

Exodus 7 in the BOKSSV

Exodus 7 in the BOLCB

Exodus 7 in the BOLCB2

Exodus 7 in the BOMCV

Exodus 7 in the BONAV

Exodus 7 in the BONCB

Exodus 7 in the BONLT

Exodus 7 in the BONUT2

Exodus 7 in the BOPLNT

Exodus 7 in the BOSCB

Exodus 7 in the BOSNC

Exodus 7 in the BOTLNT

Exodus 7 in the BOVCB

Exodus 7 in the BOYCB

Exodus 7 in the BPBB

Exodus 7 in the BPH

Exodus 7 in the BSB

Exodus 7 in the CCB

Exodus 7 in the CUV

Exodus 7 in the CUVS

Exodus 7 in the DBT

Exodus 7 in the DGDNT

Exodus 7 in the DHNT

Exodus 7 in the DNT

Exodus 7 in the ELBE

Exodus 7 in the EMTV

Exodus 7 in the ESV

Exodus 7 in the FBV

Exodus 7 in the FEB

Exodus 7 in the GGMNT

Exodus 7 in the GNT

Exodus 7 in the HARY

Exodus 7 in the HNT

Exodus 7 in the IRVA

Exodus 7 in the IRVB

Exodus 7 in the IRVG

Exodus 7 in the IRVH

Exodus 7 in the IRVK

Exodus 7 in the IRVM

Exodus 7 in the IRVM2

Exodus 7 in the IRVO

Exodus 7 in the IRVP

Exodus 7 in the IRVT

Exodus 7 in the IRVT2

Exodus 7 in the IRVU

Exodus 7 in the ISVN

Exodus 7 in the JSNT

Exodus 7 in the KAPI

Exodus 7 in the KBT1ETNIK

Exodus 7 in the KBV

Exodus 7 in the KJV

Exodus 7 in the KNFD

Exodus 7 in the LBA

Exodus 7 in the LBLA

Exodus 7 in the LNT

Exodus 7 in the LSV

Exodus 7 in the MAAL

Exodus 7 in the MBV

Exodus 7 in the MBV2

Exodus 7 in the MHNT

Exodus 7 in the MKNFD

Exodus 7 in the MNG

Exodus 7 in the MNT

Exodus 7 in the MNT2

Exodus 7 in the MRS1T

Exodus 7 in the NAA

Exodus 7 in the NASB

Exodus 7 in the NBLA

Exodus 7 in the NBS

Exodus 7 in the NBVTP

Exodus 7 in the NET2

Exodus 7 in the NIV11

Exodus 7 in the NNT

Exodus 7 in the NNT2

Exodus 7 in the NNT3

Exodus 7 in the PDDPT

Exodus 7 in the PFNT

Exodus 7 in the RMNT

Exodus 7 in the SBIAS

Exodus 7 in the SBIBS

Exodus 7 in the SBIBS2

Exodus 7 in the SBICS

Exodus 7 in the SBIDS

Exodus 7 in the SBIGS

Exodus 7 in the SBIHS

Exodus 7 in the SBIIS

Exodus 7 in the SBIIS2

Exodus 7 in the SBIIS3

Exodus 7 in the SBIKS

Exodus 7 in the SBIKS2

Exodus 7 in the SBIMS

Exodus 7 in the SBIOS

Exodus 7 in the SBIPS

Exodus 7 in the SBISS

Exodus 7 in the SBITS

Exodus 7 in the SBITS2

Exodus 7 in the SBITS3

Exodus 7 in the SBITS4

Exodus 7 in the SBIUS

Exodus 7 in the SBIVS

Exodus 7 in the SBT

Exodus 7 in the SBT1E

Exodus 7 in the SCHL

Exodus 7 in the SNT

Exodus 7 in the SUSU

Exodus 7 in the SUSU2

Exodus 7 in the SYNO

Exodus 7 in the TBIAOTANT

Exodus 7 in the TBT1E

Exodus 7 in the TBT1E2

Exodus 7 in the TFTIP

Exodus 7 in the TFTU

Exodus 7 in the TGNTATF3T

Exodus 7 in the THAI

Exodus 7 in the TNFD

Exodus 7 in the TNT

Exodus 7 in the TNTIK

Exodus 7 in the TNTIL

Exodus 7 in the TNTIN

Exodus 7 in the TNTIP

Exodus 7 in the TNTIZ

Exodus 7 in the TOMA

Exodus 7 in the TTENT

Exodus 7 in the UBG

Exodus 7 in the UGV

Exodus 7 in the UGV2

Exodus 7 in the UGV3

Exodus 7 in the VBL

Exodus 7 in the VDCC

Exodus 7 in the YALU

Exodus 7 in the YAPE

Exodus 7 in the YBVTP

Exodus 7 in the ZBP