Genesis 11 (BOKCV)

1 Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja. 2 Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari nao wakaishi huko. 3 Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali. 4 Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.” 5 Lakini BWANA akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu waliokuwa wanaujenga. 6 BWANA akasema, “Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao. 7 Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.” 8 Hivyo BWANA akawatawanya kutoka mahali pale kwenda katika dunia yote, nao wakaacha kuujenga huo mji. 9 Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo BWANA alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo BWANA akawatawanya katika uso wa dunia yote. 10 Hivi ndivyo vizazi vya Shemu. Miaka miwili baada ya gharika, Shemu alipokuwa na miaka 100, akamzaa Arfaksadi. 11 Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. 12 Wakati Arfaksadi alipokuwa na miaka thelathini na mitano, akamzaa Shela. 13 Baada ya Arfaksadi kumzaa Shela, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. 14 Shela alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Eberi. 15 Shela baada ya kumzaa Eberi, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. 16 Eberi alipokuwa na miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. 17 Baada ya Eberi kumzaa Pelegi, aliishi miaka 430, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. 18 Pelegi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Reu. 19 Baada ya Pelegi kumzaa Reu, aliishi miaka 209, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. 20 Reu alipokuwa na miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. 21 Baada ya Reu kumzaa Serugi, aliishi miaka 207, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. 22 Serugi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Nahori. 23 Baada ya Serugi kumzaa Nahori, aliishi miaka 200, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. 24 Nahori alipokuwa na miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. 25 Baada ya Nahori kumzaa Tera, aliishi miaka 119, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. 26 Tera alipokuwa na miaka sabini, akamzaa Abramu, Nahori na Harani. 27 Hawa ndio wazao wa Tera. Tera aliwazaa Abramu, Nahori na Harani. Harani akamzaa Loti. 28 Tera alipokuwa bado hai, Harani akafa huko Uru ya Wakaldayo, nchi alimozaliwa. 29 Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai, na mke wa Nahori aliitwa Milka; Milka na Iska walikuwa watoto wa Harani. 30 Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto. 31 Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mwana wa Harani mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka kwa pamoja katika Uru ya Wakaldayo kwenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko. 32 Tera alikufa huko Harani akiwa na miaka 205.

In Other Versions

Genesis 11 in the ANGEFD

Genesis 11 in the ANTPNG2D

Genesis 11 in the AS21

Genesis 11 in the BAGH

Genesis 11 in the BBPNG

Genesis 11 in the BBT1E

Genesis 11 in the BDS

Genesis 11 in the BEV

Genesis 11 in the BHAD

Genesis 11 in the BIB

Genesis 11 in the BLPT

Genesis 11 in the BNT

Genesis 11 in the BNTABOOT

Genesis 11 in the BNTLV

Genesis 11 in the BOATCB

Genesis 11 in the BOATCB2

Genesis 11 in the BOBCV

Genesis 11 in the BOCNT

Genesis 11 in the BOECS

Genesis 11 in the BOGWICC

Genesis 11 in the BOHCB

Genesis 11 in the BOHCV

Genesis 11 in the BOHLNT

Genesis 11 in the BOHNTLTAL

Genesis 11 in the BOICB

Genesis 11 in the BOILNTAP

Genesis 11 in the BOITCV

Genesis 11 in the BOKCV2

Genesis 11 in the BOKHWOG

Genesis 11 in the BOKSSV

Genesis 11 in the BOLCB

Genesis 11 in the BOLCB2

Genesis 11 in the BOMCV

Genesis 11 in the BONAV

Genesis 11 in the BONCB

Genesis 11 in the BONLT

Genesis 11 in the BONUT2

Genesis 11 in the BOPLNT

Genesis 11 in the BOSCB

Genesis 11 in the BOSNC

Genesis 11 in the BOTLNT

Genesis 11 in the BOVCB

Genesis 11 in the BOYCB

Genesis 11 in the BPBB

Genesis 11 in the BPH

Genesis 11 in the BSB

Genesis 11 in the CCB

Genesis 11 in the CUV

Genesis 11 in the CUVS

Genesis 11 in the DBT

Genesis 11 in the DGDNT

Genesis 11 in the DHNT

Genesis 11 in the DNT

Genesis 11 in the ELBE

Genesis 11 in the EMTV

Genesis 11 in the ESV

Genesis 11 in the FBV

Genesis 11 in the FEB

Genesis 11 in the GGMNT

Genesis 11 in the GNT

Genesis 11 in the HARY

Genesis 11 in the HNT

Genesis 11 in the IRVA

Genesis 11 in the IRVB

Genesis 11 in the IRVG

Genesis 11 in the IRVH

Genesis 11 in the IRVK

Genesis 11 in the IRVM

Genesis 11 in the IRVM2

Genesis 11 in the IRVO

Genesis 11 in the IRVP

Genesis 11 in the IRVT

Genesis 11 in the IRVT2

Genesis 11 in the IRVU

Genesis 11 in the ISVN

Genesis 11 in the JSNT

Genesis 11 in the KAPI

Genesis 11 in the KBT1ETNIK

Genesis 11 in the KBV

Genesis 11 in the KJV

Genesis 11 in the KNFD

Genesis 11 in the LBA

Genesis 11 in the LBLA

Genesis 11 in the LNT

Genesis 11 in the LSV

Genesis 11 in the MAAL

Genesis 11 in the MBV

Genesis 11 in the MBV2

Genesis 11 in the MHNT

Genesis 11 in the MKNFD

Genesis 11 in the MNG

Genesis 11 in the MNT

Genesis 11 in the MNT2

Genesis 11 in the MRS1T

Genesis 11 in the NAA

Genesis 11 in the NASB

Genesis 11 in the NBLA

Genesis 11 in the NBS

Genesis 11 in the NBVTP

Genesis 11 in the NET2

Genesis 11 in the NIV11

Genesis 11 in the NNT

Genesis 11 in the NNT2

Genesis 11 in the NNT3

Genesis 11 in the PDDPT

Genesis 11 in the PFNT

Genesis 11 in the RMNT

Genesis 11 in the SBIAS

Genesis 11 in the SBIBS

Genesis 11 in the SBIBS2

Genesis 11 in the SBICS

Genesis 11 in the SBIDS

Genesis 11 in the SBIGS

Genesis 11 in the SBIHS

Genesis 11 in the SBIIS

Genesis 11 in the SBIIS2

Genesis 11 in the SBIIS3

Genesis 11 in the SBIKS

Genesis 11 in the SBIKS2

Genesis 11 in the SBIMS

Genesis 11 in the SBIOS

Genesis 11 in the SBIPS

Genesis 11 in the SBISS

Genesis 11 in the SBITS

Genesis 11 in the SBITS2

Genesis 11 in the SBITS3

Genesis 11 in the SBITS4

Genesis 11 in the SBIUS

Genesis 11 in the SBIVS

Genesis 11 in the SBT

Genesis 11 in the SBT1E

Genesis 11 in the SCHL

Genesis 11 in the SNT

Genesis 11 in the SUSU

Genesis 11 in the SUSU2

Genesis 11 in the SYNO

Genesis 11 in the TBIAOTANT

Genesis 11 in the TBT1E

Genesis 11 in the TBT1E2

Genesis 11 in the TFTIP

Genesis 11 in the TFTU

Genesis 11 in the TGNTATF3T

Genesis 11 in the THAI

Genesis 11 in the TNFD

Genesis 11 in the TNT

Genesis 11 in the TNTIK

Genesis 11 in the TNTIL

Genesis 11 in the TNTIN

Genesis 11 in the TNTIP

Genesis 11 in the TNTIZ

Genesis 11 in the TOMA

Genesis 11 in the TTENT

Genesis 11 in the UBG

Genesis 11 in the UGV

Genesis 11 in the UGV2

Genesis 11 in the UGV3

Genesis 11 in the VBL

Genesis 11 in the VDCC

Genesis 11 in the YALU

Genesis 11 in the YAPE

Genesis 11 in the YBVTP

Genesis 11 in the ZBP