Genesis 14 (BOKCV)

1 Wakati huu Amrafeli mfalme wa Shinari, Arioko mfalme wa Elasari, Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu 2 kwa pamoja walikwenda kupigana vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha mfalme wa Gomora, Shinabu mfalme wa Adma, Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari). 3 Hawa wote waliotajwa mwishoni waliunganisha majeshi yao kutoka Bonde la Sidimu (yaani Bahari ya Chumvi). 4 Walikuwa wametawaliwa na Mfalme Kedorlaoma kwa miaka kumi na miwili, lakini mwaka wa kumi na tatu waliasi. 5 Mnamo mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walikwenda kupigana na kuwashinda Warefai katika Ashtaroth-Kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu, 6 na Wahori katika nchi ya kilima cha Seiri, hadi El-Parani karibu na jangwa. 7 Kisha wakarudi wakaenda En-Misfati (yaani Kadeshi), wakashinda nchi yote ya Waamaleki, pamoja na Waamori waliokuwa wakiishi Hasason-Tamari. 8 Ndipo mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari) wakatoka kupanga majeshi yao kwenye Bonde la Sidimu 9 dhidi ya Kedorlaoma, mfalme wa Elamu, Tidali mfalme wa Goimu, Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, yaani wafalme wanne dhidi ya wafalme watano. 10 Basi Bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, nao wafalme wa Sodoma na wa Gomora walipokimbia, baadhi ya watu walitumbukia huko na wengine wakakimbilia vilimani. 11 Wale wafalme wanne wakateka mali yote ya Sodoma na Gomora pamoja na vyakula vyao vyote, kisha wakaenda zao. 12 Pia walimteka Loti mwana wa ndugu yake Abramu pamoja na mali zake, kwa kuwa alikuwa akiishi Sodoma. 13 Mtu mmoja aliyekuwa ametoroka akaja kumpa Abramu Mwebrania taarifa. Wakati huu Abramu alikuwa anaishi karibu na mialoni ya Mamre Mwamori, aliyekuwa ndugu yake Eshkoli na Aneri, ambao wote walikuwa wameungana na Abramu. 14 Abramu alipopata habari kwamba jamaa yake amechukuliwa mateka, akawaita watu 318 wa nyumbani mwake waliokuwa wamefunzwa kupigana vita, wakawafuatilia hadi Dani. 15 Wakati wa usiku Abramu aliwagawa watu wake katika vikosi ili awashambulie, na akawafuatilia, akawafukuza hadi Hoba, kaskazini ya Dameski. 16 Akarudisha mali zote, na akamrudisha Loti jamaa yake na mali zake, pamoja na wanawake na watu wengine. 17 Abramu aliporudi baada ya kumshinda Mfalme Kedorlaoma na wale wafalme waliojiunga naye, mfalme wa Sodoma akatoka kwenda kumlaki katika Bonde la Shawe (yaani Bonde la Mfalme). 18 Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu alipoleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. 19 Naye akambariki Abramu, akisema,“Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana,Muumba wa mbingu na nchi. 20 Abarikiwe Mungu Aliye Juu Sana,ambaye amewaweka adui zako mkononi mwako.”Ndipo Abramu akampa Melkizedeki sehemu ya kumi ya kila kitu. 21 Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, “Nipe hao watu na hizo mali uchukue wewe mwenyewe.” 22 Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na dunia, na nimeapa 23 kwamba sitapokea kitu chochote kilicho chako, hata kama ni uzi au gidamu ya kiatu, ili kamwe usije ukasema, ‘Nimemtajirisha Abramu.’ 24 Sitapokea chochote, ila kile tu watu wangu walichokula na sehemu ambayo ni fungu la watu waliokwenda pamoja nami, ambao ni Aneri, Eshkoli na Mamre. Wao na wapewe fungu lao.”

In Other Versions

Genesis 14 in the ANGEFD

Genesis 14 in the ANTPNG2D

Genesis 14 in the AS21

Genesis 14 in the BAGH

Genesis 14 in the BBPNG

Genesis 14 in the BBT1E

Genesis 14 in the BDS

Genesis 14 in the BEV

Genesis 14 in the BHAD

Genesis 14 in the BIB

Genesis 14 in the BLPT

Genesis 14 in the BNT

Genesis 14 in the BNTABOOT

Genesis 14 in the BNTLV

Genesis 14 in the BOATCB

Genesis 14 in the BOATCB2

Genesis 14 in the BOBCV

Genesis 14 in the BOCNT

Genesis 14 in the BOECS

Genesis 14 in the BOGWICC

Genesis 14 in the BOHCB

Genesis 14 in the BOHCV

Genesis 14 in the BOHLNT

Genesis 14 in the BOHNTLTAL

Genesis 14 in the BOICB

Genesis 14 in the BOILNTAP

Genesis 14 in the BOITCV

Genesis 14 in the BOKCV2

Genesis 14 in the BOKHWOG

Genesis 14 in the BOKSSV

Genesis 14 in the BOLCB

Genesis 14 in the BOLCB2

Genesis 14 in the BOMCV

Genesis 14 in the BONAV

Genesis 14 in the BONCB

Genesis 14 in the BONLT

Genesis 14 in the BONUT2

Genesis 14 in the BOPLNT

Genesis 14 in the BOSCB

Genesis 14 in the BOSNC

Genesis 14 in the BOTLNT

Genesis 14 in the BOVCB

Genesis 14 in the BOYCB

Genesis 14 in the BPBB

Genesis 14 in the BPH

Genesis 14 in the BSB

Genesis 14 in the CCB

Genesis 14 in the CUV

Genesis 14 in the CUVS

Genesis 14 in the DBT

Genesis 14 in the DGDNT

Genesis 14 in the DHNT

Genesis 14 in the DNT

Genesis 14 in the ELBE

Genesis 14 in the EMTV

Genesis 14 in the ESV

Genesis 14 in the FBV

Genesis 14 in the FEB

Genesis 14 in the GGMNT

Genesis 14 in the GNT

Genesis 14 in the HARY

Genesis 14 in the HNT

Genesis 14 in the IRVA

Genesis 14 in the IRVB

Genesis 14 in the IRVG

Genesis 14 in the IRVH

Genesis 14 in the IRVK

Genesis 14 in the IRVM

Genesis 14 in the IRVM2

Genesis 14 in the IRVO

Genesis 14 in the IRVP

Genesis 14 in the IRVT

Genesis 14 in the IRVT2

Genesis 14 in the IRVU

Genesis 14 in the ISVN

Genesis 14 in the JSNT

Genesis 14 in the KAPI

Genesis 14 in the KBT1ETNIK

Genesis 14 in the KBV

Genesis 14 in the KJV

Genesis 14 in the KNFD

Genesis 14 in the LBA

Genesis 14 in the LBLA

Genesis 14 in the LNT

Genesis 14 in the LSV

Genesis 14 in the MAAL

Genesis 14 in the MBV

Genesis 14 in the MBV2

Genesis 14 in the MHNT

Genesis 14 in the MKNFD

Genesis 14 in the MNG

Genesis 14 in the MNT

Genesis 14 in the MNT2

Genesis 14 in the MRS1T

Genesis 14 in the NAA

Genesis 14 in the NASB

Genesis 14 in the NBLA

Genesis 14 in the NBS

Genesis 14 in the NBVTP

Genesis 14 in the NET2

Genesis 14 in the NIV11

Genesis 14 in the NNT

Genesis 14 in the NNT2

Genesis 14 in the NNT3

Genesis 14 in the PDDPT

Genesis 14 in the PFNT

Genesis 14 in the RMNT

Genesis 14 in the SBIAS

Genesis 14 in the SBIBS

Genesis 14 in the SBIBS2

Genesis 14 in the SBICS

Genesis 14 in the SBIDS

Genesis 14 in the SBIGS

Genesis 14 in the SBIHS

Genesis 14 in the SBIIS

Genesis 14 in the SBIIS2

Genesis 14 in the SBIIS3

Genesis 14 in the SBIKS

Genesis 14 in the SBIKS2

Genesis 14 in the SBIMS

Genesis 14 in the SBIOS

Genesis 14 in the SBIPS

Genesis 14 in the SBISS

Genesis 14 in the SBITS

Genesis 14 in the SBITS2

Genesis 14 in the SBITS3

Genesis 14 in the SBITS4

Genesis 14 in the SBIUS

Genesis 14 in the SBIVS

Genesis 14 in the SBT

Genesis 14 in the SBT1E

Genesis 14 in the SCHL

Genesis 14 in the SNT

Genesis 14 in the SUSU

Genesis 14 in the SUSU2

Genesis 14 in the SYNO

Genesis 14 in the TBIAOTANT

Genesis 14 in the TBT1E

Genesis 14 in the TBT1E2

Genesis 14 in the TFTIP

Genesis 14 in the TFTU

Genesis 14 in the TGNTATF3T

Genesis 14 in the THAI

Genesis 14 in the TNFD

Genesis 14 in the TNT

Genesis 14 in the TNTIK

Genesis 14 in the TNTIL

Genesis 14 in the TNTIN

Genesis 14 in the TNTIP

Genesis 14 in the TNTIZ

Genesis 14 in the TOMA

Genesis 14 in the TTENT

Genesis 14 in the UBG

Genesis 14 in the UGV

Genesis 14 in the UGV2

Genesis 14 in the UGV3

Genesis 14 in the VBL

Genesis 14 in the VDCC

Genesis 14 in the YALU

Genesis 14 in the YAPE

Genesis 14 in the YBVTP

Genesis 14 in the ZBP