Isaiah 19 (BOKCV)

1 Neno kuhusu Misri:Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu liendalo kwa harakanaye anakuja Misri.Sanamu za Misri zinatetemeka mbele yake,nayo mioyo ya Wamisri inayeyuka ndani yao. 2 “Nitamchochea Mmisri dhidi ya Mmisri,ndugu atapigana dhidi ya ndugu,jirani dhidi ya jirani,mji dhidi ya mji,ufalme dhidi ya ufalme. 3 Wamisri watakufa moyo,na nitaibatilisha mipango yao.Watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa,kwa waaguzi na kwa wale waongeao na mizimu. 4 Nitawatia Wamisrimikononi mwa bwana mkatilina mfalme mkali atatawala juu yao,”asema Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote. 5 Maji ya mito yatakauka,chini ya mto kutakauka kwa jua. 6 Mifereji itanuka;vijito vya Misri vitapunguana kukauka.Mafunjo na nyasi vitanyauka, 7 pia mimea iliyoko kando ya Mto Naili,pale mto unapomwaga maji baharini.Kila shamba lililopandwa kando ya Mto Naili litakauka,litapeperushwa na kutoweka kabisa. 8 Wavuvi watalia na kuomboleza,wale wote watupao ndoano katika Mto Naili,watadhoofika kwa majonzi. 9 Wale watu wafanyao kazi ya kitani kilichochambuliwa watakata tamaa,wafumaji wa kitani safi watavunjika moyo. 10 Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa,nao vibarua wataugua moyoni. 11 Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa,washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga.Unawezaje kumwambia Farao,“Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima,mwanafunzi wa wafalme wa zamani”? 12 Wako wapi sasa watu wako wenye hekima?Wao wakuonyeshe na kukufahamishani nini BWANA Mwenye Nguvu Zoteamepanga dhidi ya Misri. 13 Maafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu,viongozi wa Memfisi wamedanganyika,walio mawe ya pembe ya taifa lakewameipotosha Misri. 14 BWANA amewamwagiaroho ya kizunguzungu;wanaifanya Misri iyumbayumbekatika yale yote inayoyafanya,kama vile mlevi ayumbayumbavyokatika kutapika kwake. 15 Misri haiwezi kufanya kitu chochote,cha kichwa wala cha mkia,cha tawi la mtende wala cha tete. 16 Katika siku ile Wamisri watakuwa kama wanawake. Watatetemeka kwa hofu mbele ya mkono wa BWANA Mwenye Nguvu Zote anaoinua dhidi yao. 17 Nayo nchi ya Yuda itawatia hofu Wamisri, kila mmoja atakayetajiwa Yuda ataingiwa na hofu, kwa sababu ya kile ambacho BWANA Mwenye Nguvu Zote anapanga dhidi yao. 18 Katika siku hiyo miji mitano ya Misri, itazungumza lugha ya Kanaani, na kuapa kumtii BWANA Mwenye Nguvu Zote. Mji mmojawapo utaitwa Mji wa Uharibifu. 19 Katika siku hiyo patakuwepo madhabahu ya BWANA katikati ya Misri na mnara wa kumbukumbu kwa BWANA kwenye mpaka wa Misri. 20 Itakuwa alama na ushahidi kwa ajili ya BWANA Mwenye Nguvu Zote katika nchi ya Misri. Watakapomlilia BWANA kwa sababu ya watesi wao, Mungu atawapelekea mwokozi na mtetezi, naye atawaokoa. 21 Hivyo BWANA atajijulisha mwenyewe kwa Wamisri, nao katika siku hiyo watamkubali BWANA. Wataabudu kwa kumtolea dhabihu na sadaka za nafaka, watamwekea BWANA nadhiri na kuzitimiza. 22 BWANA ataipiga Misri kwa tauni; atawapiga na kuwaponya. Watamgeukia BWANA, naye atayasikia maombi yao na kuwaponya. 23 Katika siku hiyo kutakuwepo na njia kuu kutoka Misri hadi Ashuru. Waashuru watakwenda Misri, na Wamisri watakwenda Ashuru. Wamisri na Waashuru wataabudu pamoja. 24 Katika siku hiyo Israeli itakuwa ya tatu, pamoja na Misri na Ashuru, nao watakuwa baraka kwa dunia. 25 BWANA Mwenye Nguvu Zote atawabariki, akisema, “Baraka iwe kwa Misri watu wangu, kwa Ashuru kazi ya mikono yangu, na kwa Israeli urithi wangu.”

In Other Versions

Isaiah 19 in the ANGEFD

Isaiah 19 in the ANTPNG2D

Isaiah 19 in the AS21

Isaiah 19 in the BAGH

Isaiah 19 in the BBPNG

Isaiah 19 in the BBT1E

Isaiah 19 in the BDS

Isaiah 19 in the BEV

Isaiah 19 in the BHAD

Isaiah 19 in the BIB

Isaiah 19 in the BLPT

Isaiah 19 in the BNT

Isaiah 19 in the BNTABOOT

Isaiah 19 in the BNTLV

Isaiah 19 in the BOATCB

Isaiah 19 in the BOATCB2

Isaiah 19 in the BOBCV

Isaiah 19 in the BOCNT

Isaiah 19 in the BOECS

Isaiah 19 in the BOGWICC

Isaiah 19 in the BOHCB

Isaiah 19 in the BOHCV

Isaiah 19 in the BOHLNT

Isaiah 19 in the BOHNTLTAL

Isaiah 19 in the BOICB

Isaiah 19 in the BOILNTAP

Isaiah 19 in the BOITCV

Isaiah 19 in the BOKCV2

Isaiah 19 in the BOKHWOG

Isaiah 19 in the BOKSSV

Isaiah 19 in the BOLCB

Isaiah 19 in the BOLCB2

Isaiah 19 in the BOMCV

Isaiah 19 in the BONAV

Isaiah 19 in the BONCB

Isaiah 19 in the BONLT

Isaiah 19 in the BONUT2

Isaiah 19 in the BOPLNT

Isaiah 19 in the BOSCB

Isaiah 19 in the BOSNC

Isaiah 19 in the BOTLNT

Isaiah 19 in the BOVCB

Isaiah 19 in the BOYCB

Isaiah 19 in the BPBB

Isaiah 19 in the BPH

Isaiah 19 in the BSB

Isaiah 19 in the CCB

Isaiah 19 in the CUV

Isaiah 19 in the CUVS

Isaiah 19 in the DBT

Isaiah 19 in the DGDNT

Isaiah 19 in the DHNT

Isaiah 19 in the DNT

Isaiah 19 in the ELBE

Isaiah 19 in the EMTV

Isaiah 19 in the ESV

Isaiah 19 in the FBV

Isaiah 19 in the FEB

Isaiah 19 in the GGMNT

Isaiah 19 in the GNT

Isaiah 19 in the HARY

Isaiah 19 in the HNT

Isaiah 19 in the IRVA

Isaiah 19 in the IRVB

Isaiah 19 in the IRVG

Isaiah 19 in the IRVH

Isaiah 19 in the IRVK

Isaiah 19 in the IRVM

Isaiah 19 in the IRVM2

Isaiah 19 in the IRVO

Isaiah 19 in the IRVP

Isaiah 19 in the IRVT

Isaiah 19 in the IRVT2

Isaiah 19 in the IRVU

Isaiah 19 in the ISVN

Isaiah 19 in the JSNT

Isaiah 19 in the KAPI

Isaiah 19 in the KBT1ETNIK

Isaiah 19 in the KBV

Isaiah 19 in the KJV

Isaiah 19 in the KNFD

Isaiah 19 in the LBA

Isaiah 19 in the LBLA

Isaiah 19 in the LNT

Isaiah 19 in the LSV

Isaiah 19 in the MAAL

Isaiah 19 in the MBV

Isaiah 19 in the MBV2

Isaiah 19 in the MHNT

Isaiah 19 in the MKNFD

Isaiah 19 in the MNG

Isaiah 19 in the MNT

Isaiah 19 in the MNT2

Isaiah 19 in the MRS1T

Isaiah 19 in the NAA

Isaiah 19 in the NASB

Isaiah 19 in the NBLA

Isaiah 19 in the NBS

Isaiah 19 in the NBVTP

Isaiah 19 in the NET2

Isaiah 19 in the NIV11

Isaiah 19 in the NNT

Isaiah 19 in the NNT2

Isaiah 19 in the NNT3

Isaiah 19 in the PDDPT

Isaiah 19 in the PFNT

Isaiah 19 in the RMNT

Isaiah 19 in the SBIAS

Isaiah 19 in the SBIBS

Isaiah 19 in the SBIBS2

Isaiah 19 in the SBICS

Isaiah 19 in the SBIDS

Isaiah 19 in the SBIGS

Isaiah 19 in the SBIHS

Isaiah 19 in the SBIIS

Isaiah 19 in the SBIIS2

Isaiah 19 in the SBIIS3

Isaiah 19 in the SBIKS

Isaiah 19 in the SBIKS2

Isaiah 19 in the SBIMS

Isaiah 19 in the SBIOS

Isaiah 19 in the SBIPS

Isaiah 19 in the SBISS

Isaiah 19 in the SBITS

Isaiah 19 in the SBITS2

Isaiah 19 in the SBITS3

Isaiah 19 in the SBITS4

Isaiah 19 in the SBIUS

Isaiah 19 in the SBIVS

Isaiah 19 in the SBT

Isaiah 19 in the SBT1E

Isaiah 19 in the SCHL

Isaiah 19 in the SNT

Isaiah 19 in the SUSU

Isaiah 19 in the SUSU2

Isaiah 19 in the SYNO

Isaiah 19 in the TBIAOTANT

Isaiah 19 in the TBT1E

Isaiah 19 in the TBT1E2

Isaiah 19 in the TFTIP

Isaiah 19 in the TFTU

Isaiah 19 in the TGNTATF3T

Isaiah 19 in the THAI

Isaiah 19 in the TNFD

Isaiah 19 in the TNT

Isaiah 19 in the TNTIK

Isaiah 19 in the TNTIL

Isaiah 19 in the TNTIN

Isaiah 19 in the TNTIP

Isaiah 19 in the TNTIZ

Isaiah 19 in the TOMA

Isaiah 19 in the TTENT

Isaiah 19 in the UBG

Isaiah 19 in the UGV

Isaiah 19 in the UGV2

Isaiah 19 in the UGV3

Isaiah 19 in the VBL

Isaiah 19 in the VDCC

Isaiah 19 in the YALU

Isaiah 19 in the YAPE

Isaiah 19 in the YBVTP

Isaiah 19 in the ZBP