Isaiah 44 (BOKCV)

1 “Lakini sasa sikiliza, ee Yakobo, mtumishi wangu,Israeli, niliyemchagua. 2 Hili ndilo asemalo BWANA,yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni,yeye atakayekusaidia:Usiogope, ee Yakobo, mtumishi wangu,Yeshuruni, niliyekuchagua. 3 Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu,na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka;nitamimina Roho wangu juu ya watoto wako,nayo baraka yangu juu ya wazao wako. 4 Nao watachipua kama manyasi katika shamba la majani,kama mierezi kando ya vijito vya maji yatiririkayo. 5 Mmoja atasema, ‘Mimi ni wa BWANA’;mwingine atajiita kwa jina la Yakobo;vilevile mwingine ataandika juu ya mkono wake, ‘Wa BWANA,’na kujiita kwa jina la Israeli. 6 “Hili ndilo asemalo BWANA,Mfalme wa Israeli na Mkombozi, BWANA Mwenye Nguvu Zote:Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho;zaidi yangu hakuna Mungu. 7 Ni nani basi aliye kama mimi? Yeye na atangaze.Yeye atangaze na kuweka mbele yanguni kitu gani kilichotokea tangu nilipoumba watu wangu wa kale,tena ni nini kitakachotokea:naam, yeye na atoe unabii ni nini kitakachokuja. 8 Msitetemeke, msiogope.Je, sikutangaza hili, na kutoa unabii tangu zamani?Ninyi ni mashahidi wangu.Je, yuko Mungu zaidi yangu mimi?Hasha, hakuna Mwamba mwingine;mimi simjui mwingine.” 9 Wote wachongao sanamu ni ubatili,navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu.Wale ambao wanazitetea ni vipofu,ni wajinga, nao waaibika. 10 Ni nani atengenezaye mungu na kusubu sanamu,ambayo haiwezi kumfaidia kitu chochote? 11 Yeye pamoja na wenziwe wa aina yake wataaibishwa,mafundi wao si kitu ila ni wanadamu tu.Wote wakusanyike pamoja na kuwa na msimamo wao,watashushwa chini kwa hofu na kwa fedheha. 12 Muhunzi huchukua kifaana kukifanyia kazi kwenye makaa ya moto,hutengeneza sanamu kwa nyundo,huifanyiza kwa nguvu za mkono wake.Huona njaa na kupoteza nguvu zake,asipokunywa maji huzimia. 13 Seremala hupima kwa kutumia kambana huuchora mstari kwa kalamu;huchonga kwa patasina kutia alama kwa bikari.Huifanyiza katika umbo la binadamu,la mwanadamu katika utukufu wake wote,ili iweze kukaa katika sehemu yake ya ibada ya miungu. 14 Hukata miti ya mierezi,huchukua mtiriza au mwaloni.Huuacha ukue miongoni mwa miti ya msituni,au hupanda msunobari, nayo mvua huufanya ukue. 15 Ni kuni ya binadamu:yeye huchukua baadhi yake na kuota moto,huwasha moto na kuoka mkate.Lakini pia huutumia kumtengeneza mungu na akamwabudu,huitengeneza sanamu na kuisujudia. 16 Sehemu ya kuni huziweka motoni,akapikia chakula chake,hubanika nyama na kula hadi ashibe.Huota moto na kusema,“Aha! Ninahisi joto, ninaona moto.” 17 Mabaki yake hutengeneza mungu, sanamu yake;yeye huisujudia na kuiabudu.Huiomba na kusema,“Niokoe; wewe ni mungu wangu.” 18 Hawajui chochote, hawaelewi chochote,macho yao yamefungwa hata hawawezi kuona,akili zao zimefungwa hata hawawezi kufahamu. 19 Hakuna anayefikiri,hakuna mwenye maarifa wala ufahamu wa kusema,“Sehemu yake nilitumia kwa kuni;hata pia nilioka mkate juu ya makaa yake,nikabanika nyama na kuila.Je, nifanye machukizo kwa kile kilichobaki?Je, nisujudie gogo la mti?” 20 Hujilisha kwa majivu, moyo uliodanganyika humpotosha;hawezi kujiokoa mwenyewe, au kusema,“Je, kitu hiki kilichoko katika mkono wangu wa kuume si ni uongo?” 21 “Ee Yakobo, kumbuka mambo haya,ee Israeli, kwa kuwa wewe ni mtumishi wangu.Nimekuumba wewe, wewe ni mtumishi wangu.Ee Israeli, sitakusahau. 22 Nimeyafuta makosa yako kama wingu,dhambi zako kama ukungu wa asubuhi.Nirudie mimi,kwa kuwa nimekukomboa wewe.” 23 Enyi mbingu, imbeni kwa furaha,kwa maana BWANA amefanya jambo hili.Ee vilindi vya dunia, piga kelele.Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo,enyi misitu na miti yenu yote,kwa maana BWANA amemkomboa Yakobo,ameuonyesha utukufu wake katika Israeli. 24 “Hili ndilo asemalo BWANA,Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni: “Mimi ni BWANA,niliyeumba vitu vyote,niliyezitanda mbingu peke yangu,niliyeitandaza nchi mwenyewe, 25 “mimi huzipinga ishara za manabii wa uongo,na kuwatia upumbavu waaguzi,niyapinduaye maarifa ya wenye hekima,na kuyafanya kuwa upuzi, 26 niyathibitishaye maneno ya watumishi wake,na kutimiza utabiri wa wajumbe wake, “niambiaye Yerusalemu, ‘Itakaliwa na watu,’niambiaye miji ya Yuda kuwa, ‘Itajengwa,’na kuhusu magofu yake, ‘Mimi nitayatengeneza,’ 27 niambiaye kilindi cha maji, ‘Kauka,nami nitakausha vijito vyako,’ 28 nisemaye kuhusu Koreshi, ‘Yeye ni mchungaji wangu,naye atatimiza yote yanipendezayo;atauambia Yerusalemu, “Ukajengwe tena,”na kuhusu Hekalu, “Misingi yake na iwekwe.” ’

In Other Versions

Isaiah 44 in the ANGEFD

Isaiah 44 in the ANTPNG2D

Isaiah 44 in the AS21

Isaiah 44 in the BAGH

Isaiah 44 in the BBPNG

Isaiah 44 in the BBT1E

Isaiah 44 in the BDS

Isaiah 44 in the BEV

Isaiah 44 in the BHAD

Isaiah 44 in the BIB

Isaiah 44 in the BLPT

Isaiah 44 in the BNT

Isaiah 44 in the BNTABOOT

Isaiah 44 in the BNTLV

Isaiah 44 in the BOATCB

Isaiah 44 in the BOATCB2

Isaiah 44 in the BOBCV

Isaiah 44 in the BOCNT

Isaiah 44 in the BOECS

Isaiah 44 in the BOGWICC

Isaiah 44 in the BOHCB

Isaiah 44 in the BOHCV

Isaiah 44 in the BOHLNT

Isaiah 44 in the BOHNTLTAL

Isaiah 44 in the BOICB

Isaiah 44 in the BOILNTAP

Isaiah 44 in the BOITCV

Isaiah 44 in the BOKCV2

Isaiah 44 in the BOKHWOG

Isaiah 44 in the BOKSSV

Isaiah 44 in the BOLCB

Isaiah 44 in the BOLCB2

Isaiah 44 in the BOMCV

Isaiah 44 in the BONAV

Isaiah 44 in the BONCB

Isaiah 44 in the BONLT

Isaiah 44 in the BONUT2

Isaiah 44 in the BOPLNT

Isaiah 44 in the BOSCB

Isaiah 44 in the BOSNC

Isaiah 44 in the BOTLNT

Isaiah 44 in the BOVCB

Isaiah 44 in the BOYCB

Isaiah 44 in the BPBB

Isaiah 44 in the BPH

Isaiah 44 in the BSB

Isaiah 44 in the CCB

Isaiah 44 in the CUV

Isaiah 44 in the CUVS

Isaiah 44 in the DBT

Isaiah 44 in the DGDNT

Isaiah 44 in the DHNT

Isaiah 44 in the DNT

Isaiah 44 in the ELBE

Isaiah 44 in the EMTV

Isaiah 44 in the ESV

Isaiah 44 in the FBV

Isaiah 44 in the FEB

Isaiah 44 in the GGMNT

Isaiah 44 in the GNT

Isaiah 44 in the HARY

Isaiah 44 in the HNT

Isaiah 44 in the IRVA

Isaiah 44 in the IRVB

Isaiah 44 in the IRVG

Isaiah 44 in the IRVH

Isaiah 44 in the IRVK

Isaiah 44 in the IRVM

Isaiah 44 in the IRVM2

Isaiah 44 in the IRVO

Isaiah 44 in the IRVP

Isaiah 44 in the IRVT

Isaiah 44 in the IRVT2

Isaiah 44 in the IRVU

Isaiah 44 in the ISVN

Isaiah 44 in the JSNT

Isaiah 44 in the KAPI

Isaiah 44 in the KBT1ETNIK

Isaiah 44 in the KBV

Isaiah 44 in the KJV

Isaiah 44 in the KNFD

Isaiah 44 in the LBA

Isaiah 44 in the LBLA

Isaiah 44 in the LNT

Isaiah 44 in the LSV

Isaiah 44 in the MAAL

Isaiah 44 in the MBV

Isaiah 44 in the MBV2

Isaiah 44 in the MHNT

Isaiah 44 in the MKNFD

Isaiah 44 in the MNG

Isaiah 44 in the MNT

Isaiah 44 in the MNT2

Isaiah 44 in the MRS1T

Isaiah 44 in the NAA

Isaiah 44 in the NASB

Isaiah 44 in the NBLA

Isaiah 44 in the NBS

Isaiah 44 in the NBVTP

Isaiah 44 in the NET2

Isaiah 44 in the NIV11

Isaiah 44 in the NNT

Isaiah 44 in the NNT2

Isaiah 44 in the NNT3

Isaiah 44 in the PDDPT

Isaiah 44 in the PFNT

Isaiah 44 in the RMNT

Isaiah 44 in the SBIAS

Isaiah 44 in the SBIBS

Isaiah 44 in the SBIBS2

Isaiah 44 in the SBICS

Isaiah 44 in the SBIDS

Isaiah 44 in the SBIGS

Isaiah 44 in the SBIHS

Isaiah 44 in the SBIIS

Isaiah 44 in the SBIIS2

Isaiah 44 in the SBIIS3

Isaiah 44 in the SBIKS

Isaiah 44 in the SBIKS2

Isaiah 44 in the SBIMS

Isaiah 44 in the SBIOS

Isaiah 44 in the SBIPS

Isaiah 44 in the SBISS

Isaiah 44 in the SBITS

Isaiah 44 in the SBITS2

Isaiah 44 in the SBITS3

Isaiah 44 in the SBITS4

Isaiah 44 in the SBIUS

Isaiah 44 in the SBIVS

Isaiah 44 in the SBT

Isaiah 44 in the SBT1E

Isaiah 44 in the SCHL

Isaiah 44 in the SNT

Isaiah 44 in the SUSU

Isaiah 44 in the SUSU2

Isaiah 44 in the SYNO

Isaiah 44 in the TBIAOTANT

Isaiah 44 in the TBT1E

Isaiah 44 in the TBT1E2

Isaiah 44 in the TFTIP

Isaiah 44 in the TFTU

Isaiah 44 in the TGNTATF3T

Isaiah 44 in the THAI

Isaiah 44 in the TNFD

Isaiah 44 in the TNT

Isaiah 44 in the TNTIK

Isaiah 44 in the TNTIL

Isaiah 44 in the TNTIN

Isaiah 44 in the TNTIP

Isaiah 44 in the TNTIZ

Isaiah 44 in the TOMA

Isaiah 44 in the TTENT

Isaiah 44 in the UBG

Isaiah 44 in the UGV

Isaiah 44 in the UGV2

Isaiah 44 in the UGV3

Isaiah 44 in the VBL

Isaiah 44 in the VDCC

Isaiah 44 in the YALU

Isaiah 44 in the YAPE

Isaiah 44 in the YBVTP

Isaiah 44 in the ZBP