Isaiah 7 (BOKCV)
1 Wakati Ahazi mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, alipokuwa mfalme wa Yuda, Mfalme Resini wa Aramu, na Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli walipanda kupigana dhidi ya Yerusalemu, lakini hawakuweza kuushinda. 2 Wakati huu nyumba ya Daudi iliambiwa, “Aramu wameungana na Efraimu.” Kwa hiyo mioyo ya Ahazi na watu wake ilitikiswa, kama miti ya msituni inavyotikiswa na upepo. 3 Ndipo BWANA akamwambia Isaya, “Toka uende, wewe na mwanao Shear-Yashubu, mkutane na Ahazi huko mwisho wa mfereji wa Bwawa la Juu, kwenye barabara iendayo Shamba la Dobi. 4 Mwambie, ‘Uwe mwangalifu, utulie na usiogope. Usife moyo kwa ajili ya watu hawa wawili walio kama visiki vya kuni vifukavyo moshi, kwa ajili ya hasira kali ya Resini na Aramu na ya mwana wa Remalia. 5 Aramu, Efraimu na mwana wa Remalia wamepanga shauri baya ili wakuangamize, wakisema, 6 “Tuishambulie Yuda, naam, tuirarue vipande vipande na kuigawa miongoni mwetu, na kumtawaza mwana wa Tabeeli awe mfalme juu yake.” 7 Lakini BWANA Mwenyezi asema hivi:“ ‘Jambo hili halitatendeka,halitatokea, 8 kwa kuwa kichwa cha Aramu ni Dameski,na kichwa cha Dameski ni Resini peke yake.Katika muda wa miaka sitini na mitano,Efraimu atakuwa ameharibiwakiasi kwamba hataweza tena kuwa taifa. 9 Kichwa cha Efraimu ni Samaria,na kichwa cha Samariani mwana wa Remalia peke yake.Kama hamtasimama thabiti katika imani yenu,hamtaimarika kamwe.’ ” 10 BWANA akasema na Ahazi tena, 11 “Mwombe BWANA Mungu wako ishara, iwe kwenye vina virefu sana, au kwenye vimo virefu sana.” 12 Lakini Ahazi akasema, “Sitaomba; sitamjaribu BWANA.” 13 Ndipo Isaya akasema, “Sikia sasa, ewe nyumba ya Daudi! Je, haitoshi kujaribu uvumilivu wa wanadamu? Je, mtaujaribu uvumilivu wa Mungu wangu pia? 14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara: Bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, na ataitwa Imanueli. 15 Atakula jibini na asali atakapokuwa ameweza kukataa mabaya na kuchagua mema. 16 Lakini kabla mtoto hajajua kukataa mabaya na kuchagua mema, nchi ya wafalme hao wawili unaowaogopa itafanywa ukiwa. 17 BWANA ataleta juu yako, juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako wakati ambao haujawahi kuwako tangu Efraimu alipojitenga na Yuda: yeye atawaleteeni mfalme wa Ashuru.” 18 Katika siku ile BWANA atawapigia filimbi mainzi kutoka vijito vya mbali vya Misri, na nyuki kutoka nchi ya Ashuru. 19 Wote watakuja na kukaa kwenye mabonde yenye miteremko, na kwenye nyufa za miamba, kwenye vichaka vyote vyenye miiba, na kwenye mashimo yote ya maji. 20 Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ngʼambo ya Mto, yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia. 21 Katika siku ile, mtu atahifadhi hai ndama mmoja na kondoo wawili. 22 Kwa ajili ya wingi wa maziwa watakayotoa, atapata jibini ya kula. Wote watakaobakia katika nchi watakula jibini na asali. 23 Katika siku ile, kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu moja yenye thamani ya shekeli 1,000 za fedha, patakuwa na michongoma na miiba tu. 24 Watu watakwenda huko wakiwa na upinde na mshale, kwa maana nchi itafunikwa na michongoma na miiba. 25 Kuhusu vilima vyote vilivyokuwa vikilimwa kwa jembe, hamtakwenda huko tena kwa ajili ya hofu ya michongoma na miiba. Patakuwa mahali ambapo ngʼombe wataachiwa huru, na kondoo kukimbia kimbia.
In Other Versions
Isaiah 7 in the ANGEFD
Isaiah 7 in the ANTPNG2D
Isaiah 7 in the AS21
Isaiah 7 in the BAGH
Isaiah 7 in the BBPNG
Isaiah 7 in the BBT1E
Isaiah 7 in the BDS
Isaiah 7 in the BEV
Isaiah 7 in the BHAD
Isaiah 7 in the BIB
Isaiah 7 in the BLPT
Isaiah 7 in the BNT
Isaiah 7 in the BNTABOOT
Isaiah 7 in the BNTLV
Isaiah 7 in the BOATCB
Isaiah 7 in the BOATCB2
Isaiah 7 in the BOBCV
Isaiah 7 in the BOCNT
Isaiah 7 in the BOECS
Isaiah 7 in the BOGWICC
Isaiah 7 in the BOHCB
Isaiah 7 in the BOHCV
Isaiah 7 in the BOHLNT
Isaiah 7 in the BOHNTLTAL
Isaiah 7 in the BOICB
Isaiah 7 in the BOILNTAP
Isaiah 7 in the BOITCV
Isaiah 7 in the BOKCV2
Isaiah 7 in the BOKHWOG
Isaiah 7 in the BOKSSV
Isaiah 7 in the BOLCB
Isaiah 7 in the BOLCB2
Isaiah 7 in the BOMCV
Isaiah 7 in the BONAV
Isaiah 7 in the BONCB
Isaiah 7 in the BONLT
Isaiah 7 in the BONUT2
Isaiah 7 in the BOPLNT
Isaiah 7 in the BOSCB
Isaiah 7 in the BOSNC
Isaiah 7 in the BOTLNT
Isaiah 7 in the BOVCB
Isaiah 7 in the BOYCB
Isaiah 7 in the BPBB
Isaiah 7 in the BPH
Isaiah 7 in the BSB
Isaiah 7 in the CCB
Isaiah 7 in the CUV
Isaiah 7 in the CUVS
Isaiah 7 in the DBT
Isaiah 7 in the DGDNT
Isaiah 7 in the DHNT
Isaiah 7 in the DNT
Isaiah 7 in the ELBE
Isaiah 7 in the EMTV
Isaiah 7 in the ESV
Isaiah 7 in the FBV
Isaiah 7 in the FEB
Isaiah 7 in the GGMNT
Isaiah 7 in the GNT
Isaiah 7 in the HARY
Isaiah 7 in the HNT
Isaiah 7 in the IRVA
Isaiah 7 in the IRVB
Isaiah 7 in the IRVG
Isaiah 7 in the IRVH
Isaiah 7 in the IRVK
Isaiah 7 in the IRVM
Isaiah 7 in the IRVM2
Isaiah 7 in the IRVO
Isaiah 7 in the IRVP
Isaiah 7 in the IRVT
Isaiah 7 in the IRVT2
Isaiah 7 in the IRVU
Isaiah 7 in the ISVN
Isaiah 7 in the JSNT
Isaiah 7 in the KAPI
Isaiah 7 in the KBT1ETNIK
Isaiah 7 in the KBV
Isaiah 7 in the KJV
Isaiah 7 in the KNFD
Isaiah 7 in the LBA
Isaiah 7 in the LBLA
Isaiah 7 in the LNT
Isaiah 7 in the LSV
Isaiah 7 in the MAAL
Isaiah 7 in the MBV
Isaiah 7 in the MBV2
Isaiah 7 in the MHNT
Isaiah 7 in the MKNFD
Isaiah 7 in the MNG
Isaiah 7 in the MNT
Isaiah 7 in the MNT2
Isaiah 7 in the MRS1T
Isaiah 7 in the NAA
Isaiah 7 in the NASB
Isaiah 7 in the NBLA
Isaiah 7 in the NBS
Isaiah 7 in the NBVTP
Isaiah 7 in the NET2
Isaiah 7 in the NIV11
Isaiah 7 in the NNT
Isaiah 7 in the NNT2
Isaiah 7 in the NNT3
Isaiah 7 in the PDDPT
Isaiah 7 in the PFNT
Isaiah 7 in the RMNT
Isaiah 7 in the SBIAS
Isaiah 7 in the SBIBS
Isaiah 7 in the SBIBS2
Isaiah 7 in the SBICS
Isaiah 7 in the SBIDS
Isaiah 7 in the SBIGS
Isaiah 7 in the SBIHS
Isaiah 7 in the SBIIS
Isaiah 7 in the SBIIS2
Isaiah 7 in the SBIIS3
Isaiah 7 in the SBIKS
Isaiah 7 in the SBIKS2
Isaiah 7 in the SBIMS
Isaiah 7 in the SBIOS
Isaiah 7 in the SBIPS
Isaiah 7 in the SBISS
Isaiah 7 in the SBITS
Isaiah 7 in the SBITS2
Isaiah 7 in the SBITS3
Isaiah 7 in the SBITS4
Isaiah 7 in the SBIUS
Isaiah 7 in the SBIVS
Isaiah 7 in the SBT
Isaiah 7 in the SBT1E
Isaiah 7 in the SCHL
Isaiah 7 in the SNT
Isaiah 7 in the SUSU
Isaiah 7 in the SUSU2
Isaiah 7 in the SYNO
Isaiah 7 in the TBIAOTANT
Isaiah 7 in the TBT1E
Isaiah 7 in the TBT1E2
Isaiah 7 in the TFTIP
Isaiah 7 in the TFTU
Isaiah 7 in the TGNTATF3T
Isaiah 7 in the THAI
Isaiah 7 in the TNFD
Isaiah 7 in the TNT
Isaiah 7 in the TNTIK
Isaiah 7 in the TNTIL
Isaiah 7 in the TNTIN
Isaiah 7 in the TNTIP
Isaiah 7 in the TNTIZ
Isaiah 7 in the TOMA
Isaiah 7 in the TTENT
Isaiah 7 in the UBG
Isaiah 7 in the UGV
Isaiah 7 in the UGV2
Isaiah 7 in the UGV3
Isaiah 7 in the VBL
Isaiah 7 in the VDCC
Isaiah 7 in the YALU
Isaiah 7 in the YAPE
Isaiah 7 in the YBVTP
Isaiah 7 in the ZBP