James 1 (BOKCV)
1 Yakobo, mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo:Kwa makabila kumi na mawili yaliyotawanyika ulimwenguni:Salamu. 2 Ndugu zangu, hesabuni kuwa ni furaha tupu mnapopatwa na majaribu mbalimbali, 3 kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 4 Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu chochote. 5 Kama mtu yeyote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa. 6 Lakini anapoomba, lazima aamini wala asiwe na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kutupwa huku na huku. 7 Mtu kama huyo asidhani ya kuwa atapata kitu chochote kutoka kwa Bwana. 8 Yeye ni mtu mwenye nia mbili, mwenye kusitasita katika njia zake zote. 9 Ndugu asiye na cheo kikubwa yampasa ajivunie hali hiyo maana ametukuzwa. 10 Lakini yeye aliye tajiri afurahi kwa kuwa ameshushwa, kwa sababu atatoweka kama ua la shambani. 11 Kwa maana jua kali lenye kuchoma huchomoza na kuliunguza, likayakausha majani, na ua lake likapukutika, nao uzuri wake huharibika. Vivyo hivyo tajiri naye atanyauka akiwa anaendelea na shughuli zake. 12 Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji la uzima Mungu alilowaahidia wale wampendao. 13 Mtu anapojaribiwa asiseme, “Ninajaribiwa na Mungu.” Kwa maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu wala yeye hamjaribu mtu yeyote. 14 Lakini kila mtu hujaribiwa wakati anapovutwa na kudanganywa na tamaa zake mwenyewe zilizo mbaya. 15 Basi ile tamaa mbaya ikishachukua mimba, huzaa dhambi, nayo ile dhambi ikikomaa, huzaa mauti. 16 Ndugu zangu wapendwa, msidanganyike. 17 Kila kitolewacho kilicho chema na kilicho kamili, hutoka juu, na hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka. 18 Kwa mapenzi yake mwenyewe alituzaa kwa neno la kweli, kusudi tuwe kama mazao ya kwanza katika viumbe vyake vyote. 19 Ndugu zangu wapendwa, fahamuni jambo hili: Kila mtu awe mwepesi wa kusikiliza, lakini asiwe mwepesi wa kusema wala wa kukasirika. 20 Kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu. 21 Kwa hiyo, ondoleeni mbali uchafu wote na uovu ambao umezidi kuwa mwingi, mkalipokee kwa unyenyekevu lile Neno lililopandwa ndani yenu ambalo laweza kuokoa nafsi zenu. 22 Basi kuweni watendaji wa Neno wala msiwe wasikiaji tu, huku mkijidanganya nafsi zenu. 23 Kwa maana kama mtu ni msikiaji tu wa Neno wala hatendi kile linachosema, yeye ni kama mtu ajitazamaye uso wake kwenye kioo 24 na baada ya kujiona alivyo, huenda zake na mara husahau jinsi alivyo. 25 Lakini yeye anayeangalia kwa bidii katika sheria kamilifu, ile iletayo uhuru, naye akaendelea kufanya hivyo bila kusahau alichosikia, bali akalitenda, atabarikiwa katika kile anachofanya. 26 Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hujidanganya moyoni mwake, wala dini yake mtu huyo haifai kitu. 27 Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.
In Other Versions
James 1 in the ANGEFD
James 1 in the ANTPNG2D
James 1 in the AS21
James 1 in the BAGH
James 1 in the BBPNG
James 1 in the BBT1E
James 1 in the BDS
James 1 in the BEV
James 1 in the BHAD
James 1 in the BIB
James 1 in the BLPT
James 1 in the BNT
James 1 in the BNTABOOT
James 1 in the BNTLV
James 1 in the BOATCB
James 1 in the BOATCB2
James 1 in the BOBCV
James 1 in the BOCNT
James 1 in the BOECS
James 1 in the BOGWICC
James 1 in the BOHCB
James 1 in the BOHCV
James 1 in the BOHLNT
James 1 in the BOHNTLTAL
James 1 in the BOICB
James 1 in the BOILNTAP
James 1 in the BOITCV
James 1 in the BOKCV2
James 1 in the BOKHWOG
James 1 in the BOKSSV
James 1 in the BOLCB
James 1 in the BOLCB2
James 1 in the BOMCV
James 1 in the BONAV
James 1 in the BONCB
James 1 in the BONLT
James 1 in the BONUT2
James 1 in the BOPLNT
James 1 in the BOSCB
James 1 in the BOSNC
James 1 in the BOTLNT
James 1 in the BOVCB
James 1 in the BOYCB
James 1 in the BPBB
James 1 in the BPH
James 1 in the BSB
James 1 in the CCB
James 1 in the CUV
James 1 in the CUVS
James 1 in the DBT
James 1 in the DGDNT
James 1 in the DHNT
James 1 in the DNT
James 1 in the ELBE
James 1 in the EMTV
James 1 in the ESV
James 1 in the FBV
James 1 in the FEB
James 1 in the GGMNT
James 1 in the GNT
James 1 in the HARY
James 1 in the HNT
James 1 in the IRVA
James 1 in the IRVB
James 1 in the IRVG
James 1 in the IRVH
James 1 in the IRVK
James 1 in the IRVM
James 1 in the IRVM2
James 1 in the IRVO
James 1 in the IRVP
James 1 in the IRVT
James 1 in the IRVT2
James 1 in the IRVU
James 1 in the ISVN
James 1 in the JSNT
James 1 in the KAPI
James 1 in the KBT1ETNIK
James 1 in the KBV
James 1 in the KJV
James 1 in the KNFD
James 1 in the LBA
James 1 in the LBLA
James 1 in the LNT
James 1 in the LSV
James 1 in the MAAL
James 1 in the MBV
James 1 in the MBV2
James 1 in the MHNT
James 1 in the MKNFD
James 1 in the MNG
James 1 in the MNT
James 1 in the MNT2
James 1 in the MRS1T
James 1 in the NAA
James 1 in the NASB
James 1 in the NBLA
James 1 in the NBS
James 1 in the NBVTP
James 1 in the NET2
James 1 in the NIV11
James 1 in the NNT
James 1 in the NNT2
James 1 in the NNT3
James 1 in the PDDPT
James 1 in the PFNT
James 1 in the RMNT
James 1 in the SBIAS
James 1 in the SBIBS
James 1 in the SBIBS2
James 1 in the SBICS
James 1 in the SBIDS
James 1 in the SBIGS
James 1 in the SBIHS
James 1 in the SBIIS
James 1 in the SBIIS2
James 1 in the SBIIS3
James 1 in the SBIKS
James 1 in the SBIKS2
James 1 in the SBIMS
James 1 in the SBIOS
James 1 in the SBIPS
James 1 in the SBISS
James 1 in the SBITS
James 1 in the SBITS2
James 1 in the SBITS3
James 1 in the SBITS4
James 1 in the SBIUS
James 1 in the SBIVS
James 1 in the SBT
James 1 in the SBT1E
James 1 in the SCHL
James 1 in the SNT
James 1 in the SUSU
James 1 in the SUSU2
James 1 in the SYNO
James 1 in the TBIAOTANT
James 1 in the TBT1E
James 1 in the TBT1E2
James 1 in the TFTIP
James 1 in the TFTU
James 1 in the TGNTATF3T
James 1 in the THAI
James 1 in the TNFD
James 1 in the TNT
James 1 in the TNTIK
James 1 in the TNTIL
James 1 in the TNTIN
James 1 in the TNTIP
James 1 in the TNTIZ
James 1 in the TOMA
James 1 in the TTENT
James 1 in the UBG
James 1 in the UGV
James 1 in the UGV2
James 1 in the UGV3
James 1 in the VBL
James 1 in the VDCC
James 1 in the YALU
James 1 in the YAPE
James 1 in the YBVTP
James 1 in the ZBP