Judges 5 (BOKCV)
1 Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu: 2 “Wakuu katika Israeli wanapoongoza,wakati watu wanapojitoakwa hiari yao wenyewe:mhimidini BWANA! 3 “Sikieni hili, enyi wafalme!Sikilizeni, enyi watawala!Nitamwimbia BWANA, nitaimba;kwa wimbo nitamhimidi BWANA,Mungu wa Israeli. 4 “Ee BWANA, ulipotoka katika Seiri,ulipopita katika mashamba ya Edomu,nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga,naam, mawingu yakamwaga maji. 5 Milima ilitetemeka mbele za BWANA,hata ule wa Sinai,mbele za BWANA,Mungu wa Israeli. 6 “Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi,katika siku za Yaeli,barabara kuu hazikuwa na watu;wasafiri walipita njia za kando. 7 Mashujaa walikoma katika Israeli,walikoma mpaka mimi, Debora, nilipoinuka,nilipoinuka kama mama katika Israeli. 8 Walipochagua miungu migeni,vita vilikuja katika malango ya mji,hapakuonekana ngao wala mkukimiongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli. 9 Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli,pamoja na wale wanaojitoa wenyewekwa hiari yao miongoni mwa watu.Mhimidini BWANA! 10 “Nanyi mpandao punda weupe,mkiketi juu ya matandiko ya thamani,nanyi mtembeao barabarani,fikirini 11 juu ya sauti za waimbajimahali pa kunyweshea maji.Wanasimulia matendo ya haki ya BWANA,matendo ya haki ya mashujaa wakekatika Israeli. “Ndipo watu wa BWANAwalipoteremka malangoni pa mji. 12 ‘Amka, amka! Debora!Amka, amka, uimbe!Ee Baraka! Inuka,chukua mateka wako uliowateka,ee mwana wa Abinoamu.’ 13 “Ndipo mabaki ya watuwakashuka dhidi ya wenye nguvu,watu wa BWANA,wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu. 14 Kutoka Efraimu wakaja watu, ambao chimbuko lao ni Amaleki;Benyamini akiwa miongonimwa watu waliokufuata.Kutoka Makiri wakashuka viongozi,na kutoka Zabuloni wale washikaofimbo ya jemadari. 15 Wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora;naam, Isakari alikuwa pamoja na Baraka,wakija nyuma yake kwa mbiowakielekea bondeni.Katika jamaa za Reubeni,palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni. 16 Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondookusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi?Kwa jamaa za Reubeni,palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni. 17 Gileadi alikaa ngʼambo ya Yordani.Naye Dani, kwa nini alikaakwenye merikebu siku nyingi?Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari,akikaa kwenye ghuba zake ndogo. 18 Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao,vilevile nao watu wa Naftali. 19 “Wafalme walikuja na kufanya vita;wafalme wa Kanaani walipiganahuko Taanaki karibu na maji ya Megido,lakini hawakuchukua fedha wala nyara. 20 Kutoka mbinguni nyota zilipigana,nyota kutoka njia zakezilipigana na Sisera. 21 Mto wa Kishoni uliwasomba,ule mto wa zamani, mto wa Kishoni.Songa mbele, ee nafsi yangu,kwa ujasiri! 22 Ndipo kwato za farasi zikafanya mshindo:farasi wake wenye nguvuhuenda mbio kwa kurukaruka. 23 Malaika wa BWANA akasema, ‘Merozi alaaniwe.Walaaniwe watu wake kwa uchungu,kwa kuwa hawakuja kumsaidia BWANA,kumsaidia BWANA dhidi ya hao wenye nguvu.’ 24 “Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote,mkewe Heberi, Mkeni,abarikiwe kuliko wanawake wotewaishio kwenye mahema. 25 Aliomba maji, naye akampa maziwa;kwenye bakuli la heshimaakamletea maziwa mgando. 26 Akanyoosha mkono wakeakashika kigingi cha hema,mkono wake wa kuumeukashika nyundo ya fundi.Akampiga Sisera kwa nyundo,akamponda kichwa chake,akamvunjavunja na kumtoboapaji lake la uso. 27 Aliinama miguuni pa Yaeli,akaanguka; akalala hapo.Pale alipoinama miguuni pake,alianguka;pale alipoinamia, ndipo alipoanguka,akiwa amekufa. 28 “Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia;nyuma ya dirisha alilia, akasema,‘Mbona gari lake linachelewa kufika?Mbona vishindo vya magari yakevimechelewa?’ 29 Wanawake wenye busarakuliko wengine wote wakamjibu;naam, husema moyoni mwake, 30 ‘Je, hawapati na kugawanya nyara:msichana mmoja au wawili kwa kila mtu,mavazi ya rangi mbalimbali kwa Sisera kuwa nyara,mavazi ya rangi mbalimbali yaliyotariziwa,mavazi yaliyotariziwa vizuri kwa ajili ya shingo yangu:yote haya yakiwa nyara?’ 31 “Adui zako wote na waangamie, Ee BWANA!Bali wote wakupendao na wawe kama jualichomozavyo kwa nguvu zake.”Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.