Jeremiah 15 (BOKCV)
1 Kisha BWANA akaniambia: “Hata kama Mose na Samweli wangesimama mbele zangu, moyo wangu usingewaelekea watu hawa. Waondoe mbele za macho yangu! Waache waende! 2 Nao kama wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndilo BWANA asemalo:“ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, wakafe;waliowekwa kwa ajili ya upanga, kwa upanga;waliowekwa kwa ajili ya njaa, kwa njaa:waliowekwa kwa ajili ya kutekwa, watekwe.’ ” 3 BWANA asema, “Nitatuma aina nne za waharabu dhidi yao: nazo ni upanga ili kuua na mbwa ili wakokote mbali, ndege wa angani na wanyama wa nchi ili kula na kuangamiza. 4 Nitawafanya wawe machukizo kwa falme zote za dunia kwa sababu ya kile alichofanya Manase mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda huko Yerusalemu. 5 “Ni nani atakayekuhurumia, ee Yerusalemu?Ni nani atakayeomboleza kwa ajili yako?Ni nani atakayesimama ili kuulizakuhusu hali yako? 6 Umenikataa mimi,” asema BWANA.“Unazidi kukengeuka.Hivyo nitanyoosha mkono wangu juu yako na kukuangamiza,siwezi kuendelea kukuonea huruma. 7 Nitawapepeta kwa uma wa kupepeteakwenye malango ya miji katika nchi.Nitaleta msiba na maangamizi juu ya watu wangu,kwa maana hawajabadili njia zao. 8 Nitawafanya wajane wao kuwa wengikuliko mchanga wa bahari.Wakati wa adhuhuri nitamleta mharabudhidi ya mama wa vijana wao waume;kwa ghafula nitaleta juu yaomaumivu makuu na hofu kuu. 9 Mama mwenye watoto saba atazimiana kupumua pumzi yake ya mwisho.Jua lake litatua kungali bado mchana,atatahayarika na kufedheheka.Wale wote waliobaki nitawaua kwa upangambele ya adui zao,”asema BWANA. 10 Ole wangu, mama yangu, kwamba ulinizaa,mtu ambaye ulimwengu woteunashindana na kugombana naye!Sikukopa wala sikukopesha,lakini kila mmoja ananilaani. 11 BWANA akasema,“Hakika nitakuokoa kwa kusudi jema,hakika nitawafanya adui zako wakuombe msaadanyakati za maafa na nyakati za dhiki. 12 “Je, mtu aweza kuvunja chuma,chuma kitokacho kaskazini, au shaba? 13 Utajiri wako na hazina zako nitavitoa kuwa nyara,bila gharama,kwa sababu ya dhambi zako zotekatika nchi yako yote. 14 Nitakufanya uwe mtumwa wa adui zakokatika nchi usiyoijua,kwa kuwa katika hasira yangu moto umewashwautakaowaka juu yako daima.” 15 Wewe unafahamu, Ee BWANA,unikumbuke na unitunze mimi.Lipiza kisasi juu ya watesi wangu.Kwa uvumilivu wako usiniondolee mbali;kumbuka jinsi ninavyoshutumiwa. 16 Maneno yako yalipokuja, niliyala;yakawa shangwe yanguna furaha ya moyo wangu,kwa kuwa nimeitwa kwa jina lako,Ee BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote. 17 Kamwe sikuketi katika kundi la wafanyao sherehe,wala kamwe sikujifurahisha pamoja nao;niliketi peke yangu kwa sababu mkono wako ulikuwa juu yangu,na wewe ulikuwa umenijaza hasira. 18 Kwa nini maumivu yangu hayakomi,na jeraha langu ni la kuhuzunisha,wala haliponyeki?Je, utakuwa kwangu kama kijito cha udanganyifu,kama chemchemi iliyokauka? 19 Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA:“Kama ukitubu, nitakurejezaili uweze kunitumikia;kama ukinena maneno yenye maana,wala si ya upuzi,utakuwa mnenaji wangu.Watu hawa ndio watakaokugeukia,wala si wewe utakayewageukia wao. 20 Nitakufanya wewe uwe ukuta kwa watu hawa,ngome ya ukuta wa shaba;watapigana nawelakini hawatakushinda,kwa maana mimi niko pamoja nawekukuponya na kukuokoa,”asema BWANA. 21 “Nitakuokoa kutoka mikono ya waovu,na kukukomboa kutoka makucha ya watu wakatili.”
In Other Versions
Jeremiah 15 in the ANGEFD
Jeremiah 15 in the ANTPNG2D
Jeremiah 15 in the AS21
Jeremiah 15 in the BAGH
Jeremiah 15 in the BBPNG
Jeremiah 15 in the BBT1E
Jeremiah 15 in the BDS
Jeremiah 15 in the BEV
Jeremiah 15 in the BHAD
Jeremiah 15 in the BIB
Jeremiah 15 in the BLPT
Jeremiah 15 in the BNT
Jeremiah 15 in the BNTABOOT
Jeremiah 15 in the BNTLV
Jeremiah 15 in the BOATCB
Jeremiah 15 in the BOATCB2
Jeremiah 15 in the BOBCV
Jeremiah 15 in the BOCNT
Jeremiah 15 in the BOECS
Jeremiah 15 in the BOGWICC
Jeremiah 15 in the BOHCB
Jeremiah 15 in the BOHCV
Jeremiah 15 in the BOHLNT
Jeremiah 15 in the BOHNTLTAL
Jeremiah 15 in the BOICB
Jeremiah 15 in the BOILNTAP
Jeremiah 15 in the BOITCV
Jeremiah 15 in the BOKCV2
Jeremiah 15 in the BOKHWOG
Jeremiah 15 in the BOKSSV
Jeremiah 15 in the BOLCB
Jeremiah 15 in the BOLCB2
Jeremiah 15 in the BOMCV
Jeremiah 15 in the BONAV
Jeremiah 15 in the BONCB
Jeremiah 15 in the BONLT
Jeremiah 15 in the BONUT2
Jeremiah 15 in the BOPLNT
Jeremiah 15 in the BOSCB
Jeremiah 15 in the BOSNC
Jeremiah 15 in the BOTLNT
Jeremiah 15 in the BOVCB
Jeremiah 15 in the BOYCB
Jeremiah 15 in the BPBB
Jeremiah 15 in the BPH
Jeremiah 15 in the BSB
Jeremiah 15 in the CCB
Jeremiah 15 in the CUV
Jeremiah 15 in the CUVS
Jeremiah 15 in the DBT
Jeremiah 15 in the DGDNT
Jeremiah 15 in the DHNT
Jeremiah 15 in the DNT
Jeremiah 15 in the ELBE
Jeremiah 15 in the EMTV
Jeremiah 15 in the ESV
Jeremiah 15 in the FBV
Jeremiah 15 in the FEB
Jeremiah 15 in the GGMNT
Jeremiah 15 in the GNT
Jeremiah 15 in the HARY
Jeremiah 15 in the HNT
Jeremiah 15 in the IRVA
Jeremiah 15 in the IRVB
Jeremiah 15 in the IRVG
Jeremiah 15 in the IRVH
Jeremiah 15 in the IRVK
Jeremiah 15 in the IRVM
Jeremiah 15 in the IRVM2
Jeremiah 15 in the IRVO
Jeremiah 15 in the IRVP
Jeremiah 15 in the IRVT
Jeremiah 15 in the IRVT2
Jeremiah 15 in the IRVU
Jeremiah 15 in the ISVN
Jeremiah 15 in the JSNT
Jeremiah 15 in the KAPI
Jeremiah 15 in the KBT1ETNIK
Jeremiah 15 in the KBV
Jeremiah 15 in the KJV
Jeremiah 15 in the KNFD
Jeremiah 15 in the LBA
Jeremiah 15 in the LBLA
Jeremiah 15 in the LNT
Jeremiah 15 in the LSV
Jeremiah 15 in the MAAL
Jeremiah 15 in the MBV
Jeremiah 15 in the MBV2
Jeremiah 15 in the MHNT
Jeremiah 15 in the MKNFD
Jeremiah 15 in the MNG
Jeremiah 15 in the MNT
Jeremiah 15 in the MNT2
Jeremiah 15 in the MRS1T
Jeremiah 15 in the NAA
Jeremiah 15 in the NASB
Jeremiah 15 in the NBLA
Jeremiah 15 in the NBS
Jeremiah 15 in the NBVTP
Jeremiah 15 in the NET2
Jeremiah 15 in the NIV11
Jeremiah 15 in the NNT
Jeremiah 15 in the NNT2
Jeremiah 15 in the NNT3
Jeremiah 15 in the PDDPT
Jeremiah 15 in the PFNT
Jeremiah 15 in the RMNT
Jeremiah 15 in the SBIAS
Jeremiah 15 in the SBIBS
Jeremiah 15 in the SBIBS2
Jeremiah 15 in the SBICS
Jeremiah 15 in the SBIDS
Jeremiah 15 in the SBIGS
Jeremiah 15 in the SBIHS
Jeremiah 15 in the SBIIS
Jeremiah 15 in the SBIIS2
Jeremiah 15 in the SBIIS3
Jeremiah 15 in the SBIKS
Jeremiah 15 in the SBIKS2
Jeremiah 15 in the SBIMS
Jeremiah 15 in the SBIOS
Jeremiah 15 in the SBIPS
Jeremiah 15 in the SBISS
Jeremiah 15 in the SBITS
Jeremiah 15 in the SBITS2
Jeremiah 15 in the SBITS3
Jeremiah 15 in the SBITS4
Jeremiah 15 in the SBIUS
Jeremiah 15 in the SBIVS
Jeremiah 15 in the SBT
Jeremiah 15 in the SBT1E
Jeremiah 15 in the SCHL
Jeremiah 15 in the SNT
Jeremiah 15 in the SUSU
Jeremiah 15 in the SUSU2
Jeremiah 15 in the SYNO
Jeremiah 15 in the TBIAOTANT
Jeremiah 15 in the TBT1E
Jeremiah 15 in the TBT1E2
Jeremiah 15 in the TFTIP
Jeremiah 15 in the TFTU
Jeremiah 15 in the TGNTATF3T
Jeremiah 15 in the THAI
Jeremiah 15 in the TNFD
Jeremiah 15 in the TNT
Jeremiah 15 in the TNTIK
Jeremiah 15 in the TNTIL
Jeremiah 15 in the TNTIN
Jeremiah 15 in the TNTIP
Jeremiah 15 in the TNTIZ
Jeremiah 15 in the TOMA
Jeremiah 15 in the TTENT
Jeremiah 15 in the UBG
Jeremiah 15 in the UGV
Jeremiah 15 in the UGV2
Jeremiah 15 in the UGV3
Jeremiah 15 in the VBL
Jeremiah 15 in the VDCC
Jeremiah 15 in the YALU
Jeremiah 15 in the YAPE
Jeremiah 15 in the YBVTP
Jeremiah 15 in the ZBP