Jeremiah 19 (BOKCV)

1 Hili ndilo asemalo BWANA: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kutoka kwa mfinyanzi. Wachukue baadhi ya wazee wa watu na wa makuhani 2 na mtoke mwende mpaka kwenye Bonde la Ben-Hinomu, karibu na ingilio la Lango la Vigae. Huko tangaza maneno ninayokuambia, 3 nawe useme, ‘Sikieni neno la BWANA, enyi wafalme wa Yuda na watu wa Yerusalemu. Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Sikilizeni! Nitaleta maafa mahali hapa, ambayo yatafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yawashe. 4 Kwa kuwa wameniacha na kupafanya mahali hapa kuwa pa miungu ya kigeni. Wameiteketezea sadaka miungu ambayo wao wala baba zao wala wafalme wa Yuda kamwe hawakuijua, nao wamelijaza eneo hili kwa damu isiyo na hatia. 5 Wamejenga mahali pa juu pa kuabudia miungu pa Baali ili kuteketeza wana wao katika moto kama sadaka kwa Baali, kitu ambacho sikukiamuru wala kukitaja, wala hakikuingia akilini mwangu. 6 Hivyo jihadharini, siku zinakuja, asema BWANA, wakati watu hawatapaita tena mahali hapa Tofethi ama Bonde la Ben-Hinomu, bali Bonde la Machinjo. 7 “ ‘Nitaiharibu mipango ya Yuda na Yerusalemu mahali hapa. Nitawafanya waanguke kwa upanga mbele ya adui zao, katika mikono ya wale watafutao uhai wao, nami nitaitoa mizoga yao kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi. 8 Nitauharibu mji huu na kuufanya kitu cha kudharauliwa. Wote wapitao karibu watashangaa na kuudhihaki kwa sababu ya majeraha yake yote. 9 Nitawafanya wao kula nyama ya wana wao na binti zao; kila mmoja atakula nyama ya mwenzake wakati wa dhiki ya kuzungukwa na jeshi lililowekwa juu yao na adui wanaotafuta uhai wao.’ 10 “Kisha livunje lile gudulia wale walio pamoja nawe wakiwa wanaangalia, 11 uwaambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: Nitalivunja taifa hili na mji huu kama gudulia hili la mfinyanzi lilivyovunjwa, nalo haliwezi kutengenezeka tena. Watawazika waliokufa huko Tofethi hata isiwepo nafasi zaidi. 12 Hivi ndivyo nitakavyopafanya mahali hapa na kwa wale waishio ndani yake, asema BWANA. Nitaufanya mji huu kama Tofethi. 13 Nyumba zilizoko Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, Tofethi: yaani nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani, na kumimina dhabihu za vinywaji kwa miungu mingine.’ ” 14 Kisha Yeremia akarudi kutoka Tofethi, mahali ambapo BWANA alikuwa amemtuma kutoa unabii, akasimama katika ua wa Hekalu la BWANA na kuwaambia watu wote, 15 “Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Sikilizeni! Nitaleta juu ya mji huu pamoja na vijiji vinavyouzunguka kila maafa niliyosema dhidi yake, kwa sababu wamekuwa na shingo ngumu, na hawakuyasikiliza maneno yangu.’ ”

In Other Versions

Jeremiah 19 in the ANGEFD

Jeremiah 19 in the ANTPNG2D

Jeremiah 19 in the AS21

Jeremiah 19 in the BAGH

Jeremiah 19 in the BBPNG

Jeremiah 19 in the BBT1E

Jeremiah 19 in the BDS

Jeremiah 19 in the BEV

Jeremiah 19 in the BHAD

Jeremiah 19 in the BIB

Jeremiah 19 in the BLPT

Jeremiah 19 in the BNT

Jeremiah 19 in the BNTABOOT

Jeremiah 19 in the BNTLV

Jeremiah 19 in the BOATCB

Jeremiah 19 in the BOATCB2

Jeremiah 19 in the BOBCV

Jeremiah 19 in the BOCNT

Jeremiah 19 in the BOECS

Jeremiah 19 in the BOGWICC

Jeremiah 19 in the BOHCB

Jeremiah 19 in the BOHCV

Jeremiah 19 in the BOHLNT

Jeremiah 19 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 19 in the BOICB

Jeremiah 19 in the BOILNTAP

Jeremiah 19 in the BOITCV

Jeremiah 19 in the BOKCV2

Jeremiah 19 in the BOKHWOG

Jeremiah 19 in the BOKSSV

Jeremiah 19 in the BOLCB

Jeremiah 19 in the BOLCB2

Jeremiah 19 in the BOMCV

Jeremiah 19 in the BONAV

Jeremiah 19 in the BONCB

Jeremiah 19 in the BONLT

Jeremiah 19 in the BONUT2

Jeremiah 19 in the BOPLNT

Jeremiah 19 in the BOSCB

Jeremiah 19 in the BOSNC

Jeremiah 19 in the BOTLNT

Jeremiah 19 in the BOVCB

Jeremiah 19 in the BOYCB

Jeremiah 19 in the BPBB

Jeremiah 19 in the BPH

Jeremiah 19 in the BSB

Jeremiah 19 in the CCB

Jeremiah 19 in the CUV

Jeremiah 19 in the CUVS

Jeremiah 19 in the DBT

Jeremiah 19 in the DGDNT

Jeremiah 19 in the DHNT

Jeremiah 19 in the DNT

Jeremiah 19 in the ELBE

Jeremiah 19 in the EMTV

Jeremiah 19 in the ESV

Jeremiah 19 in the FBV

Jeremiah 19 in the FEB

Jeremiah 19 in the GGMNT

Jeremiah 19 in the GNT

Jeremiah 19 in the HARY

Jeremiah 19 in the HNT

Jeremiah 19 in the IRVA

Jeremiah 19 in the IRVB

Jeremiah 19 in the IRVG

Jeremiah 19 in the IRVH

Jeremiah 19 in the IRVK

Jeremiah 19 in the IRVM

Jeremiah 19 in the IRVM2

Jeremiah 19 in the IRVO

Jeremiah 19 in the IRVP

Jeremiah 19 in the IRVT

Jeremiah 19 in the IRVT2

Jeremiah 19 in the IRVU

Jeremiah 19 in the ISVN

Jeremiah 19 in the JSNT

Jeremiah 19 in the KAPI

Jeremiah 19 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 19 in the KBV

Jeremiah 19 in the KJV

Jeremiah 19 in the KNFD

Jeremiah 19 in the LBA

Jeremiah 19 in the LBLA

Jeremiah 19 in the LNT

Jeremiah 19 in the LSV

Jeremiah 19 in the MAAL

Jeremiah 19 in the MBV

Jeremiah 19 in the MBV2

Jeremiah 19 in the MHNT

Jeremiah 19 in the MKNFD

Jeremiah 19 in the MNG

Jeremiah 19 in the MNT

Jeremiah 19 in the MNT2

Jeremiah 19 in the MRS1T

Jeremiah 19 in the NAA

Jeremiah 19 in the NASB

Jeremiah 19 in the NBLA

Jeremiah 19 in the NBS

Jeremiah 19 in the NBVTP

Jeremiah 19 in the NET2

Jeremiah 19 in the NIV11

Jeremiah 19 in the NNT

Jeremiah 19 in the NNT2

Jeremiah 19 in the NNT3

Jeremiah 19 in the PDDPT

Jeremiah 19 in the PFNT

Jeremiah 19 in the RMNT

Jeremiah 19 in the SBIAS

Jeremiah 19 in the SBIBS

Jeremiah 19 in the SBIBS2

Jeremiah 19 in the SBICS

Jeremiah 19 in the SBIDS

Jeremiah 19 in the SBIGS

Jeremiah 19 in the SBIHS

Jeremiah 19 in the SBIIS

Jeremiah 19 in the SBIIS2

Jeremiah 19 in the SBIIS3

Jeremiah 19 in the SBIKS

Jeremiah 19 in the SBIKS2

Jeremiah 19 in the SBIMS

Jeremiah 19 in the SBIOS

Jeremiah 19 in the SBIPS

Jeremiah 19 in the SBISS

Jeremiah 19 in the SBITS

Jeremiah 19 in the SBITS2

Jeremiah 19 in the SBITS3

Jeremiah 19 in the SBITS4

Jeremiah 19 in the SBIUS

Jeremiah 19 in the SBIVS

Jeremiah 19 in the SBT

Jeremiah 19 in the SBT1E

Jeremiah 19 in the SCHL

Jeremiah 19 in the SNT

Jeremiah 19 in the SUSU

Jeremiah 19 in the SUSU2

Jeremiah 19 in the SYNO

Jeremiah 19 in the TBIAOTANT

Jeremiah 19 in the TBT1E

Jeremiah 19 in the TBT1E2

Jeremiah 19 in the TFTIP

Jeremiah 19 in the TFTU

Jeremiah 19 in the TGNTATF3T

Jeremiah 19 in the THAI

Jeremiah 19 in the TNFD

Jeremiah 19 in the TNT

Jeremiah 19 in the TNTIK

Jeremiah 19 in the TNTIL

Jeremiah 19 in the TNTIN

Jeremiah 19 in the TNTIP

Jeremiah 19 in the TNTIZ

Jeremiah 19 in the TOMA

Jeremiah 19 in the TTENT

Jeremiah 19 in the UBG

Jeremiah 19 in the UGV

Jeremiah 19 in the UGV2

Jeremiah 19 in the UGV3

Jeremiah 19 in the VBL

Jeremiah 19 in the VDCC

Jeremiah 19 in the YALU

Jeremiah 19 in the YAPE

Jeremiah 19 in the YBVTP

Jeremiah 19 in the ZBP