Jeremiah 2 (BOKCV)

1 Neno la BWANA lilinijia kusema, 2 “Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu:“ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako,jinsi ulivyonipenda kama bibi arusina kunifuata katika jangwa lile lote,katika nchi isiyopandwa mbegu. 3 Israeli alikuwa mtakatifu kwa BWANA,kama malimbuko ya kwanza ya mavuno yake;wote waliowaangamiza walihesabiwa kuwa na hatia,nayo maafa yaliwakumba,’ ”asema BWANA. 4 Sikia neno la BWANA, ee nyumba ya Yakobo,nanyi nyote jamaa za nyumba ya Israeli. 5 Hivi ndivyo asemavyo BWANA:“Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu,hata wakatangatanga mbali nami hivyo?Walifuata sanamu zisizofaa,nao wenyewe wakawa hawafai. 6 Hawakuuliza, ‘Yuko wapi BWANA,aliyetupandisha kutoka Misrina kutuongoza kupitia nyika kame,kupitia nchi ya majangwa na mabonde,nchi ya ukame na giza,nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yakewala hakuna mtu aishiye humo?’ 7 Niliwaleta katika nchi yenye wingi wa vituili mpate kula matunda yakena utajiri wa mazao yake.Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu,na kuufanya urithi wangu chukizo. 8 Makuhani hawakuuliza,‘Yuko wapi BWANA?’Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi;viongozi waliasi dhidi yangu.Manabii walitabiri kwa jina la Baali,wakifuata sanamu zisizofaa. 9 “Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,”asema BWANA.“Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako. 10 Vuka, nenda ngʼambo mpaka pwani ya Kitimu nawe uangalie,tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini,uone kama kumekuwepo kitu kama hiki. 11 Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote?(Hata ingawa hao si miungu kamwe.)Lakini watu wangu wamebadili Utukufu waokwa sanamu zisizofaa kitu. 12 Shangaeni katika hili, ee mbingu,nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,”asema BWANA. 13 “Watu wangu wametenda dhambi mbili:Wameniacha mimi,niliye chemchemi ya maji yaliyo hai,nao wamejichimbia visima vyao wenyewe,visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji. 14 Je, Israeli ni mtumishi, yaani mtumwa kwa kuzaliwa?Kwa nini basi amekuwa mateka? 15 Simba wamenguruma;wamemngurumia.Wameifanya nchi yake kuwa ukiwa;miji yake imeteketezwa, nayo imeachwa haina watu. 16 Pia watu wa Memfisi na Tahpanhesiwamevunja taji ya kichwa chako. 17 Je, hukujiletea hili wewe mwenyewekwa kumwacha BWANA, Mungu wakoalipowaongoza njiani? 18 Sasa kwa nini uende Misrikunywa maji ya Shihori?Nawe kwa nini kwenda Ashurukunywa maji ya Mto Frati? 19 Uovu wako utakuadhibu;kurudi nyuma kwako kutakukemea.Basi kumbuka, utambuejinsi lilivyo ovu na chungu kwakounapomwacha BWANA Mungu wakona kutokuwa na hofu yangu,”asema Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote. 20 “Zamani nilivunja nira yakona kukatilia mbali vifungo vyako;ukasema, ‘Sitakutumikia!’Naam kweli, kwenye kila kilima kirefuna chini ya kila mti uliotanda matawi yakeulijilaza kama kahaba. 21 Nilikupanda ukiwa mzabibu ulio bora sana,mkamilifu na wa mbegu nzuri.Ilikuwaje basi ukawa kinyume nami,ukaharibika na kuwa mzabibu mwitu? 22 Hata ujisafishe kwa magadina kutumia sabuni nyingi,bado doa la hatia yako liko mbele zangu,”asema BWANA Mwenyezi. 23 “Wawezaje kusema, ‘Mimi si najisi,sijawafuata Mabaali’?Kumbuka jinsi ulivyotenda kule bondeni;fikiri uliyoyafanya.Wewe ni ngamia jike mwenye mbioukikimbia hapa na pale, 24 punda-mwitu aliyezoea jangwa,anayenusa upepo katika tamaa yake kubwa:katika wakati wake wa kuhitaji mbeguni nani awezaye kumzuia?Madume yoyote yanayomfuatiliahayana haja ya kujichosha;wakati wa kupandwa kwake watampata tu. 25 Usikimbie hadi miguu yako iwe haina viatu,na koo lako liwe limekauka.Lakini ulisema, ‘Haina maana!Ninaipenda miungu ya kigeni,nami lazima niifuatie.’ 26 “Kama vile mwizi aaibikavyo wakati amekamatwa,hivyo ndivyo nyumba ya Israeli inavyoaibishwa:wao wenyewe, wafalme wao na maafisa wao,makuhani wao na manabii wao. 27 Wanaiambia miti, ‘Wewe ndiwe baba yangu,’nalo jiwe, ‘Wewe ndiwe uliyenizaa.’Wamenipa visogo vyaowala hawakunigeuzia nyuso zao;lakini wakiwa katika taabu, wanasema,‘Njoo utuokoe!’ 28 Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea?Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoawakati mko katika taabu!Kwa maana mna miungu mingikama mlivyo na miji, ee Yuda. 29 “Kwa nini mnaleta mashtaka dhidi yangu?Ninyi nyote mmeniasi,”asema BWANA. 30 “Nimeadhibu watu wako bure tu,hawakujirekebisha.Upanga wako umewala manabii wakokama simba mwenye njaa. 31 “Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la BWANA:“Je, nimekuwa jangwa kwa Israeliau nchi ya giza kuu?Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura,hatutarudi kwako tena’? 32 Je, mwanamwali husahau vito vyake,au bibi arusi mapambo yake ya arusi?Lakini watu wangu wamenisahau mimi,tena kwa siku zisizo na hesabu. 33 Je, wewe una ustadi kiasi gani katika kufuatia mapenzi!Hata wale wanawake wabaya kuliko wotewanaweza kujifunza kutokana na njia zako. 34 Katika nguo zako watu huonadamu ya uhai ya maskini wasio na hatia,ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba.Lakini katika haya yote 35 unasema, ‘Sina hatia;Mungu hajanikasirikia.’Lakini nitakuhukumu kwa sababu unasema,‘Mimi sijatenda dhambi.’ 36 Kwa nini unatangatanga sana,kubadili njia zako?Utakatishwa tamaa na Misrikama ulivyokatishwa na Ashuru. 37 Pia utaondoka mahali hapoukiwa umeweka mikono kichwani,kwa kuwa BWANA amewakataa wale unaowatumainia;hutasaidiwa nao.

In Other Versions

Jeremiah 2 in the ANGEFD

Jeremiah 2 in the ANTPNG2D

Jeremiah 2 in the AS21

Jeremiah 2 in the BAGH

Jeremiah 2 in the BBPNG

Jeremiah 2 in the BBT1E

Jeremiah 2 in the BDS

Jeremiah 2 in the BEV

Jeremiah 2 in the BHAD

Jeremiah 2 in the BIB

Jeremiah 2 in the BLPT

Jeremiah 2 in the BNT

Jeremiah 2 in the BNTABOOT

Jeremiah 2 in the BNTLV

Jeremiah 2 in the BOATCB

Jeremiah 2 in the BOATCB2

Jeremiah 2 in the BOBCV

Jeremiah 2 in the BOCNT

Jeremiah 2 in the BOECS

Jeremiah 2 in the BOGWICC

Jeremiah 2 in the BOHCB

Jeremiah 2 in the BOHCV

Jeremiah 2 in the BOHLNT

Jeremiah 2 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 2 in the BOICB

Jeremiah 2 in the BOILNTAP

Jeremiah 2 in the BOITCV

Jeremiah 2 in the BOKCV2

Jeremiah 2 in the BOKHWOG

Jeremiah 2 in the BOKSSV

Jeremiah 2 in the BOLCB

Jeremiah 2 in the BOLCB2

Jeremiah 2 in the BOMCV

Jeremiah 2 in the BONAV

Jeremiah 2 in the BONCB

Jeremiah 2 in the BONLT

Jeremiah 2 in the BONUT2

Jeremiah 2 in the BOPLNT

Jeremiah 2 in the BOSCB

Jeremiah 2 in the BOSNC

Jeremiah 2 in the BOTLNT

Jeremiah 2 in the BOVCB

Jeremiah 2 in the BOYCB

Jeremiah 2 in the BPBB

Jeremiah 2 in the BPH

Jeremiah 2 in the BSB

Jeremiah 2 in the CCB

Jeremiah 2 in the CUV

Jeremiah 2 in the CUVS

Jeremiah 2 in the DBT

Jeremiah 2 in the DGDNT

Jeremiah 2 in the DHNT

Jeremiah 2 in the DNT

Jeremiah 2 in the ELBE

Jeremiah 2 in the EMTV

Jeremiah 2 in the ESV

Jeremiah 2 in the FBV

Jeremiah 2 in the FEB

Jeremiah 2 in the GGMNT

Jeremiah 2 in the GNT

Jeremiah 2 in the HARY

Jeremiah 2 in the HNT

Jeremiah 2 in the IRVA

Jeremiah 2 in the IRVB

Jeremiah 2 in the IRVG

Jeremiah 2 in the IRVH

Jeremiah 2 in the IRVK

Jeremiah 2 in the IRVM

Jeremiah 2 in the IRVM2

Jeremiah 2 in the IRVO

Jeremiah 2 in the IRVP

Jeremiah 2 in the IRVT

Jeremiah 2 in the IRVT2

Jeremiah 2 in the IRVU

Jeremiah 2 in the ISVN

Jeremiah 2 in the JSNT

Jeremiah 2 in the KAPI

Jeremiah 2 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 2 in the KBV

Jeremiah 2 in the KJV

Jeremiah 2 in the KNFD

Jeremiah 2 in the LBA

Jeremiah 2 in the LBLA

Jeremiah 2 in the LNT

Jeremiah 2 in the LSV

Jeremiah 2 in the MAAL

Jeremiah 2 in the MBV

Jeremiah 2 in the MBV2

Jeremiah 2 in the MHNT

Jeremiah 2 in the MKNFD

Jeremiah 2 in the MNG

Jeremiah 2 in the MNT

Jeremiah 2 in the MNT2

Jeremiah 2 in the MRS1T

Jeremiah 2 in the NAA

Jeremiah 2 in the NASB

Jeremiah 2 in the NBLA

Jeremiah 2 in the NBS

Jeremiah 2 in the NBVTP

Jeremiah 2 in the NET2

Jeremiah 2 in the NIV11

Jeremiah 2 in the NNT

Jeremiah 2 in the NNT2

Jeremiah 2 in the NNT3

Jeremiah 2 in the PDDPT

Jeremiah 2 in the PFNT

Jeremiah 2 in the RMNT

Jeremiah 2 in the SBIAS

Jeremiah 2 in the SBIBS

Jeremiah 2 in the SBIBS2

Jeremiah 2 in the SBICS

Jeremiah 2 in the SBIDS

Jeremiah 2 in the SBIGS

Jeremiah 2 in the SBIHS

Jeremiah 2 in the SBIIS

Jeremiah 2 in the SBIIS2

Jeremiah 2 in the SBIIS3

Jeremiah 2 in the SBIKS

Jeremiah 2 in the SBIKS2

Jeremiah 2 in the SBIMS

Jeremiah 2 in the SBIOS

Jeremiah 2 in the SBIPS

Jeremiah 2 in the SBISS

Jeremiah 2 in the SBITS

Jeremiah 2 in the SBITS2

Jeremiah 2 in the SBITS3

Jeremiah 2 in the SBITS4

Jeremiah 2 in the SBIUS

Jeremiah 2 in the SBIVS

Jeremiah 2 in the SBT

Jeremiah 2 in the SBT1E

Jeremiah 2 in the SCHL

Jeremiah 2 in the SNT

Jeremiah 2 in the SUSU

Jeremiah 2 in the SUSU2

Jeremiah 2 in the SYNO

Jeremiah 2 in the TBIAOTANT

Jeremiah 2 in the TBT1E

Jeremiah 2 in the TBT1E2

Jeremiah 2 in the TFTIP

Jeremiah 2 in the TFTU

Jeremiah 2 in the TGNTATF3T

Jeremiah 2 in the THAI

Jeremiah 2 in the TNFD

Jeremiah 2 in the TNT

Jeremiah 2 in the TNTIK

Jeremiah 2 in the TNTIL

Jeremiah 2 in the TNTIN

Jeremiah 2 in the TNTIP

Jeremiah 2 in the TNTIZ

Jeremiah 2 in the TOMA

Jeremiah 2 in the TTENT

Jeremiah 2 in the UBG

Jeremiah 2 in the UGV

Jeremiah 2 in the UGV2

Jeremiah 2 in the UGV3

Jeremiah 2 in the VBL

Jeremiah 2 in the VDCC

Jeremiah 2 in the YALU

Jeremiah 2 in the YAPE

Jeremiah 2 in the YBVTP

Jeremiah 2 in the ZBP