Jeremiah 26 (BOKCV)
1 Mwanzoni mwa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilikuja kutoka kwa BWANA: 2 “Hili ndilo BWANA asemalo: Simama katika ua wa nyumba ya BWANA na useme na watu wote wa miji ya Yuda wanaokuja kuabudu katika nyumba ya BWANA. Waambie kila kitu nitakachokuamuru, usipunguze neno. 3 Huenda watasikiliza, na kila mmoja akageuka kutoka njia yake mbaya. Kisha nitawahurumia na kuacha kuwaletea maafa niliyokuwa ninapanga kwa sababu ya maovu waliyofanya. 4 Waambie, ‘Hili ndilo asemalo BWANA: Ikiwa hamtanisikiliza na kuifuata sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu, 5 nanyi ikiwa hamtayasikiliza maneno ya watumishi wangu manabii, ambao nimewatuma kwenu tena na tena (ijapokuwa hamkuwasikiliza), 6 ndipo nitaifanya nyumba hii kama Shilo na mji huu kuwa kitu cha kulaaniwa na mataifa yote ya dunia.’ ” 7 Makuhani, manabii na watu wote wakamsikia Yeremia akiyasema maneno haya ndani ya nyumba ya BWANA. 8 Lakini mara tu Yeremia alipomaliza kuwaambia watu kila kitu BWANA alichomwamuru kukisema, basi makuhani, manabii na watu wote walimkamata wakisema, “Ni lazima ufe! 9 Kwa nini unatoa unabii katika jina la BWANA kwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa na kuachwa tupu?” Nao watu wote wakamkusanyikia na kumzunguka Yeremia ndani ya nyumba ya BWANA. 10 Maafisa wa Yuda waliposikia kuhusu mambo haya, wakapanda kutoka jumba la kifalme, wakaenda katika nyumba ya BWANA na kushika nafasi zao kwenye ingilio la Lango Jipya la nyumba ya BWANA. 11 Kisha makuhani na manabii wakawaambia maafisa pamoja na watu wote, “Mtu huyu anastahili ahukumiwe kifo kwa sababu ametoa unabii mbaya dhidi ya mji huu. Mmesikia kwa masikio yenu wenyewe!” 12 Kisha Yeremia akawaambia maafisa wote na watu wote: “BWANA amenituma kutoa unabii dhidi ya nyumba hii na mji huu mambo yote mliyoyasikia. 13 Sasa tengenezeni njia zenu na matendo yenu, na kumtii BWANA Mungu wenu. Ndipo BWANA atawahurumia na kuacha kuleta maafa aliyokuwa ameyatamka dhidi yenu. 14 Lakini kwa habari yangu mimi, niko mikononi mwenu, nifanyieni lolote mnaloona kuwa ni jema na la haki. 15 Hata hivyo, jueni kwa hakika, ikiwa mtaniua, mtakuwa mmejipatia dhambi kwa damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe, na juu ya mji huu na wote wanaoishi ndani yake, kwa maana ni kweli BWANA amenituma kwenu ili niseme maneno haya yote masikioni mwenu.” 16 Kisha maafisa na watu wote wakawaambia makuhani na manabii, “Mtu huyu asihukumiwe kifo! Amesema nasi katika jina la BWANA, Mungu wetu.” 17 Baadhi ya wazee wa nchi wakasogea mbele, wakaliambia kusanyiko lote la watu, 18 “Mika Mmoreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote:“ ‘Sayuni italimwa kama shamba,Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto,na kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguukilichofunikwa na vichaka.’ 19 Je, Hezekia mfalme wa Yuda au mtu mwingine yeyote katika Yuda alimhukumu Mika kufa? Je, Hezekia hakumcha BWANA na kuhitaji msaada wake? Je, BWANA hakuwahurumia na akaacha kuleta maafa aliyokuwa ametamka dhidi yao? Tunakaribia sana kujiletea maangamizo ya kutisha sisi wenyewe!” 20 (Wakati huu, Uria mwana wa Shemaya kutoka mji wa Kiriath-Yearimu alikuwa mtu mwingine aliyetoa unabii kwa jina la BWANA. Alitoa unabii juu ya mambo yaliyofanana na haya dhidi ya mji huu na nchi hii kama alivyofanya Yeremia. 21 Mfalme Yehoyakimu na wakuu wake wote na maafisa waliposikia maneno yake, mfalme alitafuta kumuua. Lakini Uria alipata habari, na kwa kuogopa akakimbilia Misri. 22 Hata hivyo, Mfalme Yehoyakimu alimtuma Elnathani mwana wa Akbori huko Misri, pamoja na watu wengine ili kwenda kumkamata Uria. 23 Wakamrudisha Uria kutoka Misri na kumpeleka kwa Mfalme Yehoyakimu, ambaye alimuua kwa upanga, na mwili wake kutupwa kwenye eneo la makaburi ya watu wasio na cheo.) 24 Zaidi ya hayo, Ahikamu mwana wa Shafani akamuunga mkono Yeremia, kwa hiyo hakutiwa tena mikononi mwa watu ili auawe.
In Other Versions
Jeremiah 26 in the ANGEFD
Jeremiah 26 in the ANTPNG2D
Jeremiah 26 in the AS21
Jeremiah 26 in the BAGH
Jeremiah 26 in the BBPNG
Jeremiah 26 in the BBT1E
Jeremiah 26 in the BDS
Jeremiah 26 in the BEV
Jeremiah 26 in the BHAD
Jeremiah 26 in the BIB
Jeremiah 26 in the BLPT
Jeremiah 26 in the BNT
Jeremiah 26 in the BNTABOOT
Jeremiah 26 in the BNTLV
Jeremiah 26 in the BOATCB
Jeremiah 26 in the BOATCB2
Jeremiah 26 in the BOBCV
Jeremiah 26 in the BOCNT
Jeremiah 26 in the BOECS
Jeremiah 26 in the BOGWICC
Jeremiah 26 in the BOHCB
Jeremiah 26 in the BOHCV
Jeremiah 26 in the BOHLNT
Jeremiah 26 in the BOHNTLTAL
Jeremiah 26 in the BOICB
Jeremiah 26 in the BOILNTAP
Jeremiah 26 in the BOITCV
Jeremiah 26 in the BOKCV2
Jeremiah 26 in the BOKHWOG
Jeremiah 26 in the BOKSSV
Jeremiah 26 in the BOLCB
Jeremiah 26 in the BOLCB2
Jeremiah 26 in the BOMCV
Jeremiah 26 in the BONAV
Jeremiah 26 in the BONCB
Jeremiah 26 in the BONLT
Jeremiah 26 in the BONUT2
Jeremiah 26 in the BOPLNT
Jeremiah 26 in the BOSCB
Jeremiah 26 in the BOSNC
Jeremiah 26 in the BOTLNT
Jeremiah 26 in the BOVCB
Jeremiah 26 in the BOYCB
Jeremiah 26 in the BPBB
Jeremiah 26 in the BPH
Jeremiah 26 in the BSB
Jeremiah 26 in the CCB
Jeremiah 26 in the CUV
Jeremiah 26 in the CUVS
Jeremiah 26 in the DBT
Jeremiah 26 in the DGDNT
Jeremiah 26 in the DHNT
Jeremiah 26 in the DNT
Jeremiah 26 in the ELBE
Jeremiah 26 in the EMTV
Jeremiah 26 in the ESV
Jeremiah 26 in the FBV
Jeremiah 26 in the FEB
Jeremiah 26 in the GGMNT
Jeremiah 26 in the GNT
Jeremiah 26 in the HARY
Jeremiah 26 in the HNT
Jeremiah 26 in the IRVA
Jeremiah 26 in the IRVB
Jeremiah 26 in the IRVG
Jeremiah 26 in the IRVH
Jeremiah 26 in the IRVK
Jeremiah 26 in the IRVM
Jeremiah 26 in the IRVM2
Jeremiah 26 in the IRVO
Jeremiah 26 in the IRVP
Jeremiah 26 in the IRVT
Jeremiah 26 in the IRVT2
Jeremiah 26 in the IRVU
Jeremiah 26 in the ISVN
Jeremiah 26 in the JSNT
Jeremiah 26 in the KAPI
Jeremiah 26 in the KBT1ETNIK
Jeremiah 26 in the KBV
Jeremiah 26 in the KJV
Jeremiah 26 in the KNFD
Jeremiah 26 in the LBA
Jeremiah 26 in the LBLA
Jeremiah 26 in the LNT
Jeremiah 26 in the LSV
Jeremiah 26 in the MAAL
Jeremiah 26 in the MBV
Jeremiah 26 in the MBV2
Jeremiah 26 in the MHNT
Jeremiah 26 in the MKNFD
Jeremiah 26 in the MNG
Jeremiah 26 in the MNT
Jeremiah 26 in the MNT2
Jeremiah 26 in the MRS1T
Jeremiah 26 in the NAA
Jeremiah 26 in the NASB
Jeremiah 26 in the NBLA
Jeremiah 26 in the NBS
Jeremiah 26 in the NBVTP
Jeremiah 26 in the NET2
Jeremiah 26 in the NIV11
Jeremiah 26 in the NNT
Jeremiah 26 in the NNT2
Jeremiah 26 in the NNT3
Jeremiah 26 in the PDDPT
Jeremiah 26 in the PFNT
Jeremiah 26 in the RMNT
Jeremiah 26 in the SBIAS
Jeremiah 26 in the SBIBS
Jeremiah 26 in the SBIBS2
Jeremiah 26 in the SBICS
Jeremiah 26 in the SBIDS
Jeremiah 26 in the SBIGS
Jeremiah 26 in the SBIHS
Jeremiah 26 in the SBIIS
Jeremiah 26 in the SBIIS2
Jeremiah 26 in the SBIIS3
Jeremiah 26 in the SBIKS
Jeremiah 26 in the SBIKS2
Jeremiah 26 in the SBIMS
Jeremiah 26 in the SBIOS
Jeremiah 26 in the SBIPS
Jeremiah 26 in the SBISS
Jeremiah 26 in the SBITS
Jeremiah 26 in the SBITS2
Jeremiah 26 in the SBITS3
Jeremiah 26 in the SBITS4
Jeremiah 26 in the SBIUS
Jeremiah 26 in the SBIVS
Jeremiah 26 in the SBT
Jeremiah 26 in the SBT1E
Jeremiah 26 in the SCHL
Jeremiah 26 in the SNT
Jeremiah 26 in the SUSU
Jeremiah 26 in the SUSU2
Jeremiah 26 in the SYNO
Jeremiah 26 in the TBIAOTANT
Jeremiah 26 in the TBT1E
Jeremiah 26 in the TBT1E2
Jeremiah 26 in the TFTIP
Jeremiah 26 in the TFTU
Jeremiah 26 in the TGNTATF3T
Jeremiah 26 in the THAI
Jeremiah 26 in the TNFD
Jeremiah 26 in the TNT
Jeremiah 26 in the TNTIK
Jeremiah 26 in the TNTIL
Jeremiah 26 in the TNTIN
Jeremiah 26 in the TNTIP
Jeremiah 26 in the TNTIZ
Jeremiah 26 in the TOMA
Jeremiah 26 in the TTENT
Jeremiah 26 in the UBG
Jeremiah 26 in the UGV
Jeremiah 26 in the UGV2
Jeremiah 26 in the UGV3
Jeremiah 26 in the VBL
Jeremiah 26 in the VDCC
Jeremiah 26 in the YALU
Jeremiah 26 in the YAPE
Jeremiah 26 in the YBVTP
Jeremiah 26 in the ZBP