Jeremiah 48 (BOKCV)

1 Kuhusu Moabu: Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo:“Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa.Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa;Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa. 2 Moabu haitasifiwa tena;huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake:‘Njooni na tuangamize taifa lile.’Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa;upanga utakufuatia. 3 Sikiliza kilio kutoka Horonaimu,kilio cha maangamizi makuu na uharibifu. 4 Moabu utavunjwa,wadogo wake watapiga kelele. 5 Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi,wakilia kwa uchungu wanapotembea,kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu,kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika. 6 Kimbieni! Okoeni maisha yenu,kuweni kama kichaka jangwani. 7 Kwa kuwa mmetumainia matendo yenu na mali zenu,ninyi pia mtachukuliwa mateka,naye Kemoshi atakwenda uhamishoni,pamoja na makuhani wake na maafisa wake. 8 Mharabu atakuja dhidi ya kila mji,wala hakuna mji utakaookoka.Bonde litaangamizwa na uwanda utaharibiwa,kwa sababu BWANA amesema. 9 Wekeni chumvi kwa ajili ya Moabu,kwa kuwa ataangamizwa;miji yake itakuwa ukiwa,pasipo kuwa na mtu atakayeishi ndani yake. 10 “Alaaniwe yeye afanyaye kazi ya BWANA kwa hila!Alaaniwe yeye auzuiaye upanga wake usimwage damu! 11 “Moabu amestarehe tangu ujana wake,kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake,haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine,hajaenda uhamishoni.Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo,nayo harufu yake haijabadilika. 12 Lakini siku zinakuja,”asema BWANA,“nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia,nao watamimina;wataacha magudulia yake yakiwa matupuna kuvunja mitungi yake. 13 Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi,kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibuwalipotegemea mungu wa Betheli. 14 “Mwawezaje kusema, ‘Sisi ni mashujaa,watu jasiri katika vita’? 15 Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa,vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,”asema Mfalme, ambaye jina lakeni BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote. 16 “Kuanguka kwa Moabu kumekaribia,janga kubwa litamjia kwa haraka. 17 Ombolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaomzunguka,ninyi nyote mnaojua sifa zake,semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika fimbo ya kifalme yenye nguvu,tazama jinsi ilivyovunjika fimbo iliyotukuka!’ 18 “Shuka kutoka fahari yakona uketi katika ardhi iliyokauka,enyi wenyeji wa Binti wa Diboni,kwa maana yeye aangamizaye Moabu atakuja dhidi yako,na kuangamiza miji yako iliyozungushiwa maboma. 19 Simama kando ya barabara na utazame,wewe unayeishi Aroeri.Muulize mwanaume anayekimbiana mwanamke anayetoroka,waulize, ‘Kumetokea nini?’ 20 Moabu amefedheheshwa, kwa kuwa amevunjavunjwa.Lieni kwa huzuni na kupiga kelele!Tangazeni kando ya Arnonikwamba Moabu ameangamizwa. 21 Hukumu imefika kwenye uwanda wa juu:katika Holoni, Yahasa na Mefaathi, 22 katika Diboni, Nebona Beth-Diblathaimu, 23 katika Kiriathaimu, Beth-Gamulina Beth-Meoni, 24 katika Keriothi na Bosra;kwa miji yote ya Moabu,iliyoko mbali na karibu. 25 Pembe ya Moabu imekatwa,mkono wake umevunjwa,”asema BWANA. 26 “Mlevye,kwa kuwa amemdharau BWANA.Moabu na agaegae katika matapishi yake,yeye na awe kitu cha dhihaka. 27 Je, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa?Je, alikamatwa miongoni mwa wezi,kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharaukila mara unapozungumza juu yake? 28 Ondokeni kwenye miji yenu, mkaishi katikati ya miamba,enyi mnaoishi Moabu.Kuweni kama huwa ambaye hutengeneza kiota chakekwenye mdomo wa pango. 29 “Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu:kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno,kiburi chake na ufidhuli wake,na kujivuna kwa moyo wake. 30 Ninaujua ujeuri wake, lakini ni bure,”asema BWANA,“nako kujisifu kwake hakumsaidii chochote. 31 Kwa hiyo namlilia Moabu,kwa ajili ya Moabu yote ninalia,ninaomboleza kwa ajiliya watu wa Kir-Haresethi. 32 Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo,enyi mizabibu ya Sibma.Matawi yako yameenea hadi baharini;yamefika hadi bahari ya Yazeri.Mharabu ameyaangukia matunda yako yaliyoivana mizabibu yako iliyoiva. 33 Shangwe na furaha vimetowekakutoka bustani na mashamba ya Moabu.Nimekomesha kutiririka kwa divai kutoka mashinikizo;hakuna hata mmoja ayakanyagaye kwa kelele za shangwe.Ingawa kuna kelele,sio kelele za shangwe. 34 “Sauti ya kilio chao inapandakutoka Heshboni hadi Eleale na Yahazi,kutoka Soari hadi Horonaimu na Eglath-Shelishiya,kwa kuwa hata maji ya Nimrimu yamekauka. 35 Nitakomesha wale wote katika Moabuwatoao sadaka mahali pa juu,na kufukiza uvumba kwa miungu yao,”asema BWANA. 36 “Kwa hiyo moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama filimbi;unaomboleza kama filimbi kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi.Utajiri waliojipatia umetoweka. 37 Kila kichwa kimenyolewana kila mwenye ndevu zimekatwa;kila mkono umekatwana kila kiuno kimefunikwa kwa nguo ya gunia. 38 Juu ya mapaa yote katika Moabuna katika viwanjahakuna kitu chochote isipokuwa maombolezo,kwa kuwa nimemvunja Moabukama gudulia ambalo hakuna mtu yeyote anayelitaka,”asema BWANA. 39 “Tazama jinsi alivyovunjikavunjika!Jinsi wanavyolia kwa huzuni!Tazama jinsi Moabu anavyogeuka kwa aibu!Moabu amekuwa kitu cha kudhihakiwa,kitu cha kutisha kwa wale wotewanaomzunguka.” 40 Hili ndilo asemalo BWANA:“Tazama! Tai anashuka chini,akitanda mabawa yake juu ya Moabu. 41 Miji itatekwa na ngome zakezitatwaliwa.Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Moabuitakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa. 42 Moabu ataangamizwa kama taifakwa sababu amemdharau BWANA. 43 Hofu kuu, shimo na mtego vinawangojea,enyi watu wa Moabu,”asema BWANA. 44 “Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuuataanguka ndani ya shimo,yeyote atakayepanda kutoka shimoni,atanaswa katika mtego,kwa sababu nitaletea Moabumwaka wa adhabu yake,”asema BWANA. 45 “Katika kivuli cha Heshboni,wakimbizi wamesimama pasipo msaada,kwa kuwa moto umezimika huko Heshboni,mwali wa moto kutoka katikati ya Sihoni;unaunguza vipaji vya nyuso za Moabu,mafuvu yao wenye kujivuna kwa kelele. 46 Ole wako, ee Moabu!Watu wa Kemoshi wameangamizwa;wana wako wamepelekwa uhamishonina binti zako wamechukuliwa mateka. 47 “Lakini nitarudisha mateka wa Moabu,katika siku zijazo,”asema BWANA.Huu ndio mwisho wa hukumu juu ya Moabu.

In Other Versions

Jeremiah 48 in the ANGEFD

Jeremiah 48 in the ANTPNG2D

Jeremiah 48 in the AS21

Jeremiah 48 in the BAGH

Jeremiah 48 in the BBPNG

Jeremiah 48 in the BBT1E

Jeremiah 48 in the BDS

Jeremiah 48 in the BEV

Jeremiah 48 in the BHAD

Jeremiah 48 in the BIB

Jeremiah 48 in the BLPT

Jeremiah 48 in the BNT

Jeremiah 48 in the BNTABOOT

Jeremiah 48 in the BNTLV

Jeremiah 48 in the BOATCB

Jeremiah 48 in the BOATCB2

Jeremiah 48 in the BOBCV

Jeremiah 48 in the BOCNT

Jeremiah 48 in the BOECS

Jeremiah 48 in the BOGWICC

Jeremiah 48 in the BOHCB

Jeremiah 48 in the BOHCV

Jeremiah 48 in the BOHLNT

Jeremiah 48 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 48 in the BOICB

Jeremiah 48 in the BOILNTAP

Jeremiah 48 in the BOITCV

Jeremiah 48 in the BOKCV2

Jeremiah 48 in the BOKHWOG

Jeremiah 48 in the BOKSSV

Jeremiah 48 in the BOLCB

Jeremiah 48 in the BOLCB2

Jeremiah 48 in the BOMCV

Jeremiah 48 in the BONAV

Jeremiah 48 in the BONCB

Jeremiah 48 in the BONLT

Jeremiah 48 in the BONUT2

Jeremiah 48 in the BOPLNT

Jeremiah 48 in the BOSCB

Jeremiah 48 in the BOSNC

Jeremiah 48 in the BOTLNT

Jeremiah 48 in the BOVCB

Jeremiah 48 in the BOYCB

Jeremiah 48 in the BPBB

Jeremiah 48 in the BPH

Jeremiah 48 in the BSB

Jeremiah 48 in the CCB

Jeremiah 48 in the CUV

Jeremiah 48 in the CUVS

Jeremiah 48 in the DBT

Jeremiah 48 in the DGDNT

Jeremiah 48 in the DHNT

Jeremiah 48 in the DNT

Jeremiah 48 in the ELBE

Jeremiah 48 in the EMTV

Jeremiah 48 in the ESV

Jeremiah 48 in the FBV

Jeremiah 48 in the FEB

Jeremiah 48 in the GGMNT

Jeremiah 48 in the GNT

Jeremiah 48 in the HARY

Jeremiah 48 in the HNT

Jeremiah 48 in the IRVA

Jeremiah 48 in the IRVB

Jeremiah 48 in the IRVG

Jeremiah 48 in the IRVH

Jeremiah 48 in the IRVK

Jeremiah 48 in the IRVM

Jeremiah 48 in the IRVM2

Jeremiah 48 in the IRVO

Jeremiah 48 in the IRVP

Jeremiah 48 in the IRVT

Jeremiah 48 in the IRVT2

Jeremiah 48 in the IRVU

Jeremiah 48 in the ISVN

Jeremiah 48 in the JSNT

Jeremiah 48 in the KAPI

Jeremiah 48 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 48 in the KBV

Jeremiah 48 in the KJV

Jeremiah 48 in the KNFD

Jeremiah 48 in the LBA

Jeremiah 48 in the LBLA

Jeremiah 48 in the LNT

Jeremiah 48 in the LSV

Jeremiah 48 in the MAAL

Jeremiah 48 in the MBV

Jeremiah 48 in the MBV2

Jeremiah 48 in the MHNT

Jeremiah 48 in the MKNFD

Jeremiah 48 in the MNG

Jeremiah 48 in the MNT

Jeremiah 48 in the MNT2

Jeremiah 48 in the MRS1T

Jeremiah 48 in the NAA

Jeremiah 48 in the NASB

Jeremiah 48 in the NBLA

Jeremiah 48 in the NBS

Jeremiah 48 in the NBVTP

Jeremiah 48 in the NET2

Jeremiah 48 in the NIV11

Jeremiah 48 in the NNT

Jeremiah 48 in the NNT2

Jeremiah 48 in the NNT3

Jeremiah 48 in the PDDPT

Jeremiah 48 in the PFNT

Jeremiah 48 in the RMNT

Jeremiah 48 in the SBIAS

Jeremiah 48 in the SBIBS

Jeremiah 48 in the SBIBS2

Jeremiah 48 in the SBICS

Jeremiah 48 in the SBIDS

Jeremiah 48 in the SBIGS

Jeremiah 48 in the SBIHS

Jeremiah 48 in the SBIIS

Jeremiah 48 in the SBIIS2

Jeremiah 48 in the SBIIS3

Jeremiah 48 in the SBIKS

Jeremiah 48 in the SBIKS2

Jeremiah 48 in the SBIMS

Jeremiah 48 in the SBIOS

Jeremiah 48 in the SBIPS

Jeremiah 48 in the SBISS

Jeremiah 48 in the SBITS

Jeremiah 48 in the SBITS2

Jeremiah 48 in the SBITS3

Jeremiah 48 in the SBITS4

Jeremiah 48 in the SBIUS

Jeremiah 48 in the SBIVS

Jeremiah 48 in the SBT

Jeremiah 48 in the SBT1E

Jeremiah 48 in the SCHL

Jeremiah 48 in the SNT

Jeremiah 48 in the SUSU

Jeremiah 48 in the SUSU2

Jeremiah 48 in the SYNO

Jeremiah 48 in the TBIAOTANT

Jeremiah 48 in the TBT1E

Jeremiah 48 in the TBT1E2

Jeremiah 48 in the TFTIP

Jeremiah 48 in the TFTU

Jeremiah 48 in the TGNTATF3T

Jeremiah 48 in the THAI

Jeremiah 48 in the TNFD

Jeremiah 48 in the TNT

Jeremiah 48 in the TNTIK

Jeremiah 48 in the TNTIL

Jeremiah 48 in the TNTIN

Jeremiah 48 in the TNTIP

Jeremiah 48 in the TNTIZ

Jeremiah 48 in the TOMA

Jeremiah 48 in the TTENT

Jeremiah 48 in the UBG

Jeremiah 48 in the UGV

Jeremiah 48 in the UGV2

Jeremiah 48 in the UGV3

Jeremiah 48 in the VBL

Jeremiah 48 in the VDCC

Jeremiah 48 in the YALU

Jeremiah 48 in the YAPE

Jeremiah 48 in the YBVTP

Jeremiah 48 in the ZBP