Jeremiah 6 (BOKCV)
1 “Kimbieni kwa usalama wenu, enyi watu wa Benyamini!Kimbieni kutoka Yerusalemu!Pigeni tarumbeta katika Tekoa!Inueni ishara juu ya Beth-Hakeremu!Kwa kuwa maafa yanaonekana yakitoka kaskazini,na uharibifu wa kutisha. 2 Nitamwangamiza Binti Sayuni,aliye mzuri sana na mwororo. 3 Wachungaji pamoja na makundi yaowatakuja dhidi yake;watapiga mahema yao kumzunguka,kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.” 4 “Jiandaeni kwa vita dhidi yake!Inukeni tumshambulie mchana!Lakini, ole wetu, mchana unaisha,na vivuli vya jioni vinazidi kuwa virefu. 5 Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku,na kuharibu ngome zake!” 6 Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu Zote:“Kateni miti mjenge bomakuzunguka Yerusalemu.Mji huu ni lazima uadhibiwe,umejazwa na uonevu. 7 Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake,ndivyo anavyomwaga uovu wake.Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake,ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima. 8 Pokea onyo, ee Yerusalemu,la sivyo nitageukia mbali nawena kuifanya nchi yako kuwa ukiwa,asiweze mtu kuishi ndani yake.” 9 Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu Zote:“Wao na wayakusanye mabaki ya Israelikwa uangalifu kama kwenye mzabibu;pitisha mkono wako kwenye matawi tena,kama yeye avunaye zabibu.” 10 Niseme na nani na kumpa onyo?Ni nani atakayenisikiliza mimi?Masikio yao yameziba,kwa hiyo hawawezi kusikia.Neno la BWANA ni chukizo kwao,hawalifurahii. 11 Lakini nimejaa ghadhabu ya BWANA,nami siwezi kuizuia. “Wamwagie watoto walioko barabarani,na juu ya vijana waume waliokusanyika;mume na mke watakumbwa pamoja ndani yake,hata nao wazee waliolemewa na miaka. 12 Nyumba zao zitapewa watu wengine,pamoja na mashamba yao na wake zao,nitakapounyoosha mkono wangudhidi ya wale waishio katika nchi,”asema BWANA. 13 “Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,wote wana tamaa ya kupata faida zaidi;manabii na makuhani wanafanana,wote wanafanya udanganyifu. 14 Wanafunga majeraha ya watu wangubila uangalifu.Wanasema, ‘Amani, amani,’wakati hakuna amani. 15 Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yaoinayochukiza mno?Hapana, hawana aibu hata kidogo;hawajui hata kuona haya.Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka,watashushwa chini nitakapowaadhibu,”asema BWANA. 16 Hivi ndivyo asemavyo BWANA:“Simama kwenye njia panda utazame,ulizia mapito ya zamani,ulizia wapi ilipo njia nzuri, uifuate hiyo,nanyi mtapata raha nafsini mwenu.Lakini ninyi mlisema, ‘Hatutaipita hiyo.’ 17 Niliweka walinzi juu yenu na kusema,‘Sikieni sauti ya tarumbeta!’Lakini mkasema, ‘Hatutasikiliza.’ 18 Kwa hiyo sikilizeni, enyi mataifa,angalieni, enyi mashahidi,lile litakalowatokea. 19 Sikia, ee nchi:Ninaleta maafa juu ya watu hawa,matunda ya mipango yao,kwa sababu hawakusikiliza maneno yanguna wameikataa sheria yangu. 20 Unanifaa nini uvumba kutoka Sheba,au udi wa harufu nzuri kutoka nchi ya mbali?Sadaka zako za kuteketezwa hazikubaliki,dhabihu zako hazinifurahishi mimi.” 21 Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyo BWANA:“Nitaweka vikwazo mbele ya watu hawa.Baba na wana wao watajikwaa juu yake,majirani na marafiki wataangamia.” 22 Hivi ndivyo asemavyo BWANA:“Tazama, jeshi linakujakutoka nchi ya kaskazini,taifa kubwa linaamshwakutoka miisho ya dunia. 23 Wamejifunga pinde na mkuki,ni wakatili na hawana huruma.Wanatoa sauti kama bahari inayongurumawanapoendesha farasi zao.Wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vitaili kukushambulia, ee Binti Sayuni.” 24 Tumesikia taarifa zao,nayo mikono yetu imelegea.Uchungu umetushika,maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa. 25 Usitoke kwenda mashambaniau kutembea barabarani,kwa kuwa adui ana upanga,na kuna vitisho kila upande. 26 Enyi watu wangu, vaeni maguniamjivingirishe kwenye majivu,ombolezeni kwa kilio cha uchungukama amliliaye mwana pekee,kwa maana ghafulamharabu atatujia. 27 “Nimekufanya wewe kuwa kitu cha kujaribu chuma,nao watu wangu kama mawe yenye madini,ili upate kuzijua na kuzijaribu njia zao. 28 Wote ni waasi sugu,wakienda huku na huko kusengenya.Wao ni shaba na chuma,wote wanatenda upotovu. 29 Mivuo inavuma kwa nguvu,kinachoungua kwa huo moto ni risasi,lakini pamoja na kusafisha kote huku ni bure;waovu hawaondolewi. 30 Wanaitwa fedha iliyokataliwa,kwa sababu BWANA amewakataa.”