John 14 (BOKCV)
1 Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini Mungu, niaminini na mimi pia. 2 Nyumbani kwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningeliwaambia. Naenda kuwaandalia makao. 3 Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4 Ninyi mnajua njia ya kufika ninakokwenda.” 5 Tomaso akamwambia, “Bwana, sisi hatujui unakokwenda, tutaijuaje njia?” 6 Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu. 7 Kama mngenijua mimi, mngemjua na Baba pia. Tangu sasa, mnamjua Baba yangu, tena mmemwona.” 8 Filipo akamwambia, “Bwana, tuonyeshe Baba yako yatosha.” 9 Yesu akamjibu, “Filipo, nimekaa nanyi muda huu wote hata usinijue? Mtu yeyote aliyeniona mimi, amemwona Baba. Sasa wawezaje kusema, ‘Tuonyeshe Baba’? 10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu? Maneno ninayowaambia siyasemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba akaaye ndani yangu ndiye atendaye hizi kazi. 11 Nisadiki mimi kwamba niko ndani ya Baba na Baba yuko ndani yangu, la sivyo, niaminini kwa sababu ya zile kazi nizitendazo. 12 Amin, amin nawaambia, yeyote aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo yeye atazifanya, naam na kubwa kuliko hizi atazifanya, kwa sababu mimi ninakwenda kwa Baba. 13 Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. 14 Kama mkiniomba lolote kwa Jina langu nitalifanya. 15 “Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu. 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. 17 Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu. 18 Sitawaacha ninyi yatima, naja kwenu. 19 Bado kitambo kidogo ulimwengu hautaniona tena, ila ninyi mtaniona, kwa kuwa mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. 20 Wakati huo mtajua ya kuwa mimi niko ndani ya Baba na ninyi mko ndani yangu na mimi niko ndani yenu. 21 Yeyote mwenye amri zangu na kuzishika ndiye anipendaye, naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.” 22 Ndipo Yuda, siyo Iskariote, akamwambia, “Bwana, itakuwaje kwamba utajidhihirisha kwetu na si kwa ulimwengu?” 23 Yesu akamjibu, “Mtu yeyote akinipenda atalishika neno langu na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kufanya makao yetu kwake. 24 Mtu yeyote asiyenipenda hayashiki maneno yangu na maneno niliyowapa si yangu bali ni ya Baba aliyenituma. 25 “Nimewaambia mambo haya yote wakati bado niko pamoja nanyi. 26 Lakini huyo Msaidizi, yaani, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 27 Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope. 28 “Mlinisikia nikisema, ‘Ninakwenda zangu, lakini nitarudi tena.’ Kama kweli mngelinipenda mngelifurahi kwa kuwa naenda kwa Baba, kwani Baba ni mkuu kuniliko mimi. 29 Nimewaambia mambo haya kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini. 30 Sitasema nanyi zaidi, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu anakuja, naye hana kitu kwangu, 31 lakini ulimwengu upate kujua kuwa ninampenda Baba, nami hufanya vile Baba alivyoniamuru. “Haya inukeni; twendeni zetu.
In Other Versions
John 14 in the ANGEFD
John 14 in the ANTPNG2D
John 14 in the AS21
John 14 in the BAGH
John 14 in the BBPNG
John 14 in the BBT1E
John 14 in the BDS
John 14 in the BEV
John 14 in the BHAD
John 14 in the BIB
John 14 in the BLPT
John 14 in the BNT
John 14 in the BNTABOOT
John 14 in the BNTLV
John 14 in the BOATCB
John 14 in the BOATCB2
John 14 in the BOBCV
John 14 in the BOCNT
John 14 in the BOECS
John 14 in the BOGWICC
John 14 in the BOHCB
John 14 in the BOHCV
John 14 in the BOHLNT
John 14 in the BOHNTLTAL
John 14 in the BOICB
John 14 in the BOILNTAP
John 14 in the BOITCV
John 14 in the BOKCV2
John 14 in the BOKHWOG
John 14 in the BOKSSV
John 14 in the BOLCB
John 14 in the BOLCB2
John 14 in the BOMCV
John 14 in the BONAV
John 14 in the BONCB
John 14 in the BONLT
John 14 in the BONUT2
John 14 in the BOPLNT
John 14 in the BOSCB
John 14 in the BOSNC
John 14 in the BOTLNT
John 14 in the BOVCB
John 14 in the BOYCB
John 14 in the BPBB
John 14 in the BPH
John 14 in the BSB
John 14 in the CCB
John 14 in the CUV
John 14 in the CUVS
John 14 in the DBT
John 14 in the DGDNT
John 14 in the DHNT
John 14 in the DNT
John 14 in the ELBE
John 14 in the EMTV
John 14 in the ESV
John 14 in the FBV
John 14 in the FEB
John 14 in the GGMNT
John 14 in the GNT
John 14 in the HARY
John 14 in the HNT
John 14 in the IRVA
John 14 in the IRVB
John 14 in the IRVG
John 14 in the IRVH
John 14 in the IRVK
John 14 in the IRVM
John 14 in the IRVM2
John 14 in the IRVO
John 14 in the IRVP
John 14 in the IRVT
John 14 in the IRVT2
John 14 in the IRVU
John 14 in the ISVN
John 14 in the JSNT
John 14 in the KAPI
John 14 in the KBT1ETNIK
John 14 in the KBV
John 14 in the KJV
John 14 in the KNFD
John 14 in the LBA
John 14 in the LBLA
John 14 in the LNT
John 14 in the LSV
John 14 in the MAAL
John 14 in the MBV
John 14 in the MBV2
John 14 in the MHNT
John 14 in the MKNFD
John 14 in the MNG
John 14 in the MNT
John 14 in the MNT2
John 14 in the MRS1T
John 14 in the NAA
John 14 in the NASB
John 14 in the NBLA
John 14 in the NBS
John 14 in the NBVTP
John 14 in the NET2
John 14 in the NIV11
John 14 in the NNT
John 14 in the NNT2
John 14 in the NNT3
John 14 in the PDDPT
John 14 in the PFNT
John 14 in the RMNT
John 14 in the SBIAS
John 14 in the SBIBS
John 14 in the SBIBS2
John 14 in the SBICS
John 14 in the SBIDS
John 14 in the SBIGS
John 14 in the SBIHS
John 14 in the SBIIS
John 14 in the SBIIS2
John 14 in the SBIIS3
John 14 in the SBIKS
John 14 in the SBIKS2
John 14 in the SBIMS
John 14 in the SBIOS
John 14 in the SBIPS
John 14 in the SBISS
John 14 in the SBITS
John 14 in the SBITS2
John 14 in the SBITS3
John 14 in the SBITS4
John 14 in the SBIUS
John 14 in the SBIVS
John 14 in the SBT
John 14 in the SBT1E
John 14 in the SCHL
John 14 in the SNT
John 14 in the SUSU
John 14 in the SUSU2
John 14 in the SYNO
John 14 in the TBIAOTANT
John 14 in the TBT1E
John 14 in the TBT1E2
John 14 in the TFTIP
John 14 in the TFTU
John 14 in the TGNTATF3T
John 14 in the THAI
John 14 in the TNFD
John 14 in the TNT
John 14 in the TNTIK
John 14 in the TNTIL
John 14 in the TNTIN
John 14 in the TNTIP
John 14 in the TNTIZ
John 14 in the TOMA
John 14 in the TTENT
John 14 in the UBG
John 14 in the UGV
John 14 in the UGV2
John 14 in the UGV3
John 14 in the VBL
John 14 in the VDCC
John 14 in the YALU
John 14 in the YAPE
John 14 in the YBVTP
John 14 in the ZBP