Job 21 (BOKCV)

1 Ndipo Ayubu akajibu: 2 “Yasikilizeni maneno yangu kwa makini;hii na iwe faraja mnayonipa mimi. 3 Nivumilieni ninapozungumza,nami nikishazungumza, endeleeni kunidhihaki. 4 “Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu?Kwa nini nisikose subira? 5 Niangalieni mkastaajabu;mkaweke mkono juu ya vinywa vyenu. 6 Ninapowaza juu ya hili, ninaogopa,nao mwili wangu unatetemeka. 7 Kwa nini waovu wanaendelea kuishi,wakifikia umri wa uzee na kuendelea kuwa na nguvu? 8 Huwaona watoto wao wakithibitikawakiwa wamewazunguka,wazao wao mbele za macho yao. 9 Nyumba zao zi salama wala hakuna hofu;fimbo ya Mungu haiko juu yao. 10 Madume yao ya ngʼombe huvyaza bila kushindwa kamwe;ngʼombe wao huzaa wala hawaharibu mimba. 11 Huwatoa watoto wao nje kama kundi;wadogo wao huchezacheza. 12 Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi,nao huifurahia sauti ya filimbi. 13 Huitumia miaka yao katika mafanikionao hushuka kaburini kwa amani. 14 Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’Hatuna haja ya kufahamu njia zako. 15 Mwenyezi ni nani hata tumtumikie?Tutapata faida gani kumwomba? 16 Lakini kufanikiwa kwao hakupo mikononi mwao wenyewe,hivyo najitenga mbali na shauri la waovu. 17 “Lakini ni mara ngapi taa ya waovu huzimwa?Ni mara ngapi maafa huwajia,yale yawapatayo ambayo Munguhuwapangia katika hasira yake? 18 Ni mara ngapi huwa kama majani makavu mbele ya upepo,kama makapi yachukuliwayo na dhoruba? 19 Imesemekana, ‘Mungu huiweka akiba adhabu ya mtukwa ajili ya wanawe.’Mungu na amlipe mtu mwenyewe,ili apate kulijua! 20 Macho yake mwenyewe na yaone maangamizi yake;yeye na ainywe ghadhabu ya Mwenyezi. 21 Kwani anajali nini kuhusu jamaa anayoiacha nyuma,miezi yake aliyopangiwa ifikapo mwisho? 22 “Je, yuko mtu yeyote awezaye kumfundisha Mungu maarifa,iwapo yeye ndiye ahukumuye hata walio juu ya wote? 23 Mtu mmoja hufa akiwa na nguvu zake kamili,akiwa salama na mwenye raha kamili, 24 mwili wake ukiwa umenawiri,nayo mifupa yake ikiwa imejaa mafuta ndani yake. 25 Mtu mwingine hufa katika uchungu wa nafsi,akiwa hajafurahia kamwe jambo lolote zuri. 26 Hao wote hulala mavumbini,nao mabuu huwafunika wote. 27 “Ninayajua kikamilifu yale mnayoyafikiri,mipango ambayo kwayo mngenitendea mabaya. 28 Mwasema, ‘Iko wapi sasa nyumba ya huyo mtu mkuu,mahema ambayo watu waovu walikaa?’ 29 Je, hamkuwahi kuwauliza hao wanaosafiri?Je, hamkutafakari taarifa zao: 30 kwamba mtu mwovu huepushwa kutoka siku ya maafa,kwamba huokolewa kutoka siku ya ghadhabu? 31 Ni nani hulaumu matendo yake mbele ya uso wake?Ni nani ampatilizaye kwa yale aliyoyatenda? 32 Hupelekwa kaburini,nao ulinzi ukawekwa kwenye kaburi lake. 33 Udongo ulio bondeni ni mtamu kwake;watu wote watamfuata,nao umati wa watu usiohesabika umemtangulia. 34 “Hivyo ninyi mnawezaje kunifariji kwa upuzi wenu?Hakuna kilichosalia cha majibu yenu isipokuwa uongo!”

In Other Versions

Job 21 in the ANGEFD

Job 21 in the ANTPNG2D

Job 21 in the AS21

Job 21 in the BAGH

Job 21 in the BBPNG

Job 21 in the BBT1E

Job 21 in the BDS

Job 21 in the BEV

Job 21 in the BHAD

Job 21 in the BIB

Job 21 in the BLPT

Job 21 in the BNT

Job 21 in the BNTABOOT

Job 21 in the BNTLV

Job 21 in the BOATCB

Job 21 in the BOATCB2

Job 21 in the BOBCV

Job 21 in the BOCNT

Job 21 in the BOECS

Job 21 in the BOGWICC

Job 21 in the BOHCB

Job 21 in the BOHCV

Job 21 in the BOHLNT

Job 21 in the BOHNTLTAL

Job 21 in the BOICB

Job 21 in the BOILNTAP

Job 21 in the BOITCV

Job 21 in the BOKCV2

Job 21 in the BOKHWOG

Job 21 in the BOKSSV

Job 21 in the BOLCB

Job 21 in the BOLCB2

Job 21 in the BOMCV

Job 21 in the BONAV

Job 21 in the BONCB

Job 21 in the BONLT

Job 21 in the BONUT2

Job 21 in the BOPLNT

Job 21 in the BOSCB

Job 21 in the BOSNC

Job 21 in the BOTLNT

Job 21 in the BOVCB

Job 21 in the BOYCB

Job 21 in the BPBB

Job 21 in the BPH

Job 21 in the BSB

Job 21 in the CCB

Job 21 in the CUV

Job 21 in the CUVS

Job 21 in the DBT

Job 21 in the DGDNT

Job 21 in the DHNT

Job 21 in the DNT

Job 21 in the ELBE

Job 21 in the EMTV

Job 21 in the ESV

Job 21 in the FBV

Job 21 in the FEB

Job 21 in the GGMNT

Job 21 in the GNT

Job 21 in the HARY

Job 21 in the HNT

Job 21 in the IRVA

Job 21 in the IRVB

Job 21 in the IRVG

Job 21 in the IRVH

Job 21 in the IRVK

Job 21 in the IRVM

Job 21 in the IRVM2

Job 21 in the IRVO

Job 21 in the IRVP

Job 21 in the IRVT

Job 21 in the IRVT2

Job 21 in the IRVU

Job 21 in the ISVN

Job 21 in the JSNT

Job 21 in the KAPI

Job 21 in the KBT1ETNIK

Job 21 in the KBV

Job 21 in the KJV

Job 21 in the KNFD

Job 21 in the LBA

Job 21 in the LBLA

Job 21 in the LNT

Job 21 in the LSV

Job 21 in the MAAL

Job 21 in the MBV

Job 21 in the MBV2

Job 21 in the MHNT

Job 21 in the MKNFD

Job 21 in the MNG

Job 21 in the MNT

Job 21 in the MNT2

Job 21 in the MRS1T

Job 21 in the NAA

Job 21 in the NASB

Job 21 in the NBLA

Job 21 in the NBS

Job 21 in the NBVTP

Job 21 in the NET2

Job 21 in the NIV11

Job 21 in the NNT

Job 21 in the NNT2

Job 21 in the NNT3

Job 21 in the PDDPT

Job 21 in the PFNT

Job 21 in the RMNT

Job 21 in the SBIAS

Job 21 in the SBIBS

Job 21 in the SBIBS2

Job 21 in the SBICS

Job 21 in the SBIDS

Job 21 in the SBIGS

Job 21 in the SBIHS

Job 21 in the SBIIS

Job 21 in the SBIIS2

Job 21 in the SBIIS3

Job 21 in the SBIKS

Job 21 in the SBIKS2

Job 21 in the SBIMS

Job 21 in the SBIOS

Job 21 in the SBIPS

Job 21 in the SBISS

Job 21 in the SBITS

Job 21 in the SBITS2

Job 21 in the SBITS3

Job 21 in the SBITS4

Job 21 in the SBIUS

Job 21 in the SBIVS

Job 21 in the SBT

Job 21 in the SBT1E

Job 21 in the SCHL

Job 21 in the SNT

Job 21 in the SUSU

Job 21 in the SUSU2

Job 21 in the SYNO

Job 21 in the TBIAOTANT

Job 21 in the TBT1E

Job 21 in the TBT1E2

Job 21 in the TFTIP

Job 21 in the TFTU

Job 21 in the TGNTATF3T

Job 21 in the THAI

Job 21 in the TNFD

Job 21 in the TNT

Job 21 in the TNTIK

Job 21 in the TNTIL

Job 21 in the TNTIN

Job 21 in the TNTIP

Job 21 in the TNTIZ

Job 21 in the TOMA

Job 21 in the TTENT

Job 21 in the UBG

Job 21 in the UGV

Job 21 in the UGV2

Job 21 in the UGV3

Job 21 in the VBL

Job 21 in the VDCC

Job 21 in the YALU

Job 21 in the YAPE

Job 21 in the YBVTP

Job 21 in the ZBP