Job 34 (BOKCV)

1 Kisha Elihu akasema: 2 “Sikieni maneno yangu, enyi watu wenye hekima;nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye maarifa. 3 Kwa kuwa sikio huyajaribu manenokama vile ulimi uonjavyo chakula. 4 Tujichagulie wenyewe yaliyo sawa,nasi tujifunze pamoja yaliyo mema. 5 “Ayubu anasema, ‘Mimi sina hatia,lakini Mungu ameninyima haki yangu. 6 Ingawa niko sawa,ninaonekana mwongo;nami ingawa sina kosa,kidonda changu hakiponi.’ 7 Ni mtu gani aliye kama Ayubu,anywaye dharau kama maji? 8 Ashirikianaye na watenda mabayana kuchangamana na watu waovu. 9 Kwa kuwa anasema, ‘Haimfaidi mwanadamu kitu chochoteanapojitahidi kumpendeza Mungu.’ 10 “Hivyo nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye ufahamu.Kamwe Mungu hatendi uovu,Mwenyezi hafanyi kosa. 11 Humlipa mwanadamu kwa ajili ya lile alilotenda;huleta juu yake kile ambacho matendo yake yanastahili. 12 Ni jambo lisiloweza kufikiriwa kwamba Mungu angefanya makosa,kwamba Mwenyezi angepotosha hukumu. 13 Je, ni nani aliyemtawaza juu ya dunia?Ni nani aliyemweka kuwa mwangalizi wa ulimwengu wote? 14 Kama lilikuwa kusudi la Mungu,naye akaiondoa Roho yake na pumzi yake, 15 wanadamu wote wangeliangamia kwa pamoja,na mtu angerudi mavumbini. 16 “Kama ninyi mnaufahamu, sikieni hili;sikilizeni hili nisemalo. 17 Je, yeye aichukiaye haki aweza kutawala?Je, utamhukumu mwenye haki, Aliye na Nguvu Zote? 18 Je, si ni yeye awaambiaye wafalme, ‘Ninyi hamfai kitu,’nao watu mashuhuri, ‘Ninyi ni waovu,’ 19 yeye asiyependelea wakuu,wala haonyeshi upendeleo kwa matajiri kuliko maskini,kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake? 20 Wanakufa ghafula, usiku wa manane;watu wanatikiswa nao hupita;wenye nguvu huondolewabila mkono wa mwanadamu. 21 “Macho yake yanazitazama njia za wanadamu;anaona kila hatua yao. 22 Hakuna mahali penye giza nene, wala uvuli mkubwa,ambapo watenda mabaya wanaweza kujificha. 23 Mungu hana haja ya kumchunguza mtu sana,ili apate kuja mbele zake kwa hukumu. 24 Bila kuuliza huwapondaponda wenye nguvu nyingina kuwaweka wengine mahali pao. 25 Kwa sababu huyaangalia matendo yao yote,huwaondoa usiku, nao wakaangamia. 26 Anawaadhibu kwa ajili ya uovu waomahali ambapo kila mmoja ataweza kuwaona, 27 kwa sababu wameacha kumfuata Mungu,nao hawakuiheshimu njia yake hata moja. 28 Wamesababisha kilio cha maskini kifike mbele zake,hivyo akasikia kilio cha wahitaji. 29 Lakini kama akinyamaza kimya,ni nani awezaye kumhukumu?Kama akiuficha uso wake,ni nani awezaye kumwona?Ikiwa ni taifa au mtu mmoja, kwake ni sawa, 30 ili kumzuia mtu mwovu kutawala,au wale ambao huwategea watu mitego. 31 “Kama mwanadamu akimwambia Mungu,‘Nimekosa lakini sitatenda dhambi tena. 32 Nifundishe nisichoweza kuona;kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’ 33 Je basi, Mungu atakulipa kwa masharti yako,wakati wewe umekataa kutubu?Yakupasa wewe uamue, wala si mimi;sasa niambie lile ulijualo. 34 “Wanadamu wenye ufahamu husema,wenye hekima wanaonisikia huniambia, 35 ‘Ayubu huongea bila maarifa;maneno yake hayana busara.’ 36 Laiti Ayubu angejaribiwa hadi kikomo cha mwisho,kwa sababu anajibu kama mtu mwovu! 37 Kwenye dhambi yake huongeza uasi;kwa dharau hupiga makofi miongoni mwetu,na kuzidisha maneno yake dhidi ya Mungu.”

In Other Versions

Job 34 in the ANGEFD

Job 34 in the ANTPNG2D

Job 34 in the AS21

Job 34 in the BAGH

Job 34 in the BBPNG

Job 34 in the BBT1E

Job 34 in the BDS

Job 34 in the BEV

Job 34 in the BHAD

Job 34 in the BIB

Job 34 in the BLPT

Job 34 in the BNT

Job 34 in the BNTABOOT

Job 34 in the BNTLV

Job 34 in the BOATCB

Job 34 in the BOATCB2

Job 34 in the BOBCV

Job 34 in the BOCNT

Job 34 in the BOECS

Job 34 in the BOGWICC

Job 34 in the BOHCB

Job 34 in the BOHCV

Job 34 in the BOHLNT

Job 34 in the BOHNTLTAL

Job 34 in the BOICB

Job 34 in the BOILNTAP

Job 34 in the BOITCV

Job 34 in the BOKCV2

Job 34 in the BOKHWOG

Job 34 in the BOKSSV

Job 34 in the BOLCB

Job 34 in the BOLCB2

Job 34 in the BOMCV

Job 34 in the BONAV

Job 34 in the BONCB

Job 34 in the BONLT

Job 34 in the BONUT2

Job 34 in the BOPLNT

Job 34 in the BOSCB

Job 34 in the BOSNC

Job 34 in the BOTLNT

Job 34 in the BOVCB

Job 34 in the BOYCB

Job 34 in the BPBB

Job 34 in the BPH

Job 34 in the BSB

Job 34 in the CCB

Job 34 in the CUV

Job 34 in the CUVS

Job 34 in the DBT

Job 34 in the DGDNT

Job 34 in the DHNT

Job 34 in the DNT

Job 34 in the ELBE

Job 34 in the EMTV

Job 34 in the ESV

Job 34 in the FBV

Job 34 in the FEB

Job 34 in the GGMNT

Job 34 in the GNT

Job 34 in the HARY

Job 34 in the HNT

Job 34 in the IRVA

Job 34 in the IRVB

Job 34 in the IRVG

Job 34 in the IRVH

Job 34 in the IRVK

Job 34 in the IRVM

Job 34 in the IRVM2

Job 34 in the IRVO

Job 34 in the IRVP

Job 34 in the IRVT

Job 34 in the IRVT2

Job 34 in the IRVU

Job 34 in the ISVN

Job 34 in the JSNT

Job 34 in the KAPI

Job 34 in the KBT1ETNIK

Job 34 in the KBV

Job 34 in the KJV

Job 34 in the KNFD

Job 34 in the LBA

Job 34 in the LBLA

Job 34 in the LNT

Job 34 in the LSV

Job 34 in the MAAL

Job 34 in the MBV

Job 34 in the MBV2

Job 34 in the MHNT

Job 34 in the MKNFD

Job 34 in the MNG

Job 34 in the MNT

Job 34 in the MNT2

Job 34 in the MRS1T

Job 34 in the NAA

Job 34 in the NASB

Job 34 in the NBLA

Job 34 in the NBS

Job 34 in the NBVTP

Job 34 in the NET2

Job 34 in the NIV11

Job 34 in the NNT

Job 34 in the NNT2

Job 34 in the NNT3

Job 34 in the PDDPT

Job 34 in the PFNT

Job 34 in the RMNT

Job 34 in the SBIAS

Job 34 in the SBIBS

Job 34 in the SBIBS2

Job 34 in the SBICS

Job 34 in the SBIDS

Job 34 in the SBIGS

Job 34 in the SBIHS

Job 34 in the SBIIS

Job 34 in the SBIIS2

Job 34 in the SBIIS3

Job 34 in the SBIKS

Job 34 in the SBIKS2

Job 34 in the SBIMS

Job 34 in the SBIOS

Job 34 in the SBIPS

Job 34 in the SBISS

Job 34 in the SBITS

Job 34 in the SBITS2

Job 34 in the SBITS3

Job 34 in the SBITS4

Job 34 in the SBIUS

Job 34 in the SBIVS

Job 34 in the SBT

Job 34 in the SBT1E

Job 34 in the SCHL

Job 34 in the SNT

Job 34 in the SUSU

Job 34 in the SUSU2

Job 34 in the SYNO

Job 34 in the TBIAOTANT

Job 34 in the TBT1E

Job 34 in the TBT1E2

Job 34 in the TFTIP

Job 34 in the TFTU

Job 34 in the TGNTATF3T

Job 34 in the THAI

Job 34 in the TNFD

Job 34 in the TNT

Job 34 in the TNTIK

Job 34 in the TNTIL

Job 34 in the TNTIN

Job 34 in the TNTIP

Job 34 in the TNTIZ

Job 34 in the TOMA

Job 34 in the TTENT

Job 34 in the UBG

Job 34 in the UGV

Job 34 in the UGV2

Job 34 in the UGV3

Job 34 in the VBL

Job 34 in the VDCC

Job 34 in the YALU

Job 34 in the YAPE

Job 34 in the YBVTP

Job 34 in the ZBP