Job 41 (BOKCV)
1 “Je, waweza kumvua Lewiathani kwa ndoano ya samaki,au kufunga ulimi wake kwa kamba? 2 Waweza kupitisha kamba puani mwake,au kutoboa taya lake kwa kulabu? 3 Je, ataendelea kukuomba umhurumie?Atasema nawe maneno ya upole? 4 Je, atafanya agano nawe ili umtwaeawe mtumishi wako maisha yake yote? 5 Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege,au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako? 6 Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake?Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara? 7 Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali,au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki? 8 Kama ukiweka mkono wako juu yake,utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena! 9 Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya;kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini. 10 Hakuna yeyote aliye mkali athubutuye kumchokoza.Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu? 11 Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa?Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu. 12 “Sitashindwa kunena juu ya maungo yake,nguvu zake na umbo lake zuri. 13 Ni nani awezaye kumvua gamba lake la nje?Ni nani awezaye kumsogelea na lijamu? 14 Nani athubutuye kuufungua mlango wa kinywa chake,kilichozungukwa na meno yake ya kutisha pande zote? 15 Mgongo wake una safu za ngaozilizoshikamanishwa imara pamoja; 16 kila moja iko karibu sana na mwenzake,wala hakuna hewa iwezayo kupita kati yake. 17 Zimeunganishwa imara kila moja na nyingine;zimengʼangʼaniana pamoja wala haziwezi kutenganishwa. 18 Akipiga chafya mwanga humetameta;macho yake ni kama mionzi ya mapambazuko. 19 Mienge iwakayo humiminika kutoka kinywani mwake;cheche za moto huruka nje. 20 Moshi hufuka kutoka puani mwake,kama kutoka kwenye chungu kinachotokota kwa moto wa matete. 21 Pumzi yake huwasha makaa ya mawe,nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake. 22 Nguvu hukaa katika shingo yake;utisho hutangulia mbele yake. 23 Mikunjo ya nyama yake imeshikamana imara pamoja;iko imara na haiwezi kuondolewa. 24 Kifua chake ni kigumu kama mwamba,kigumu kama jiwe la chini la kusagia. 25 Ainukapo, mashujaa wanaogopa;hurudi nyuma mbele yake anapokwenda kwa kishindo. 26 Upanga unaomfikia haumdhuru,wala mkuki au mshale wala fumo. 27 Chuma hukiona kama unyasi,na shaba kama mti uliooza. 28 Mishale haimfanyi yeye akimbie;mawe ya kombeo kwake ni kama makapi. 29 Rungu kwake huwa kama kipande cha jani kavu;hucheka sauti za kugongana kwa mkuki. 30 Sehemu zake za chini kwenye tumbozina menomeno na mapengo kama vigae vya chungu,zikiacha mburuzo kwenye matopekama chombo chenye meno cha kupuria. 31 Huvisukasuka vilindi kama sufuria kubwa ichemkayo,na kukoroga bahari kama chungu cha marhamu. 32 Anapopita nyuma yake huacha mkondo unaometameta;mtu angedhani vilindi vilikuwa na mvi. 33 Hakuna chochote duniani kinacholingana naye:yeye ni kiumbe kisicho na woga. 34 Yeye huwatazama chini wale wote wenye kujivuna;yeye ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.”
In Other Versions
Job 41 in the ANGEFD
Job 41 in the ANTPNG2D
Job 41 in the AS21
Job 41 in the BAGH
Job 41 in the BBPNG
Job 41 in the BBT1E
Job 41 in the BDS
Job 41 in the BEV
Job 41 in the BHAD
Job 41 in the BIB
Job 41 in the BLPT
Job 41 in the BNT
Job 41 in the BNTABOOT
Job 41 in the BNTLV
Job 41 in the BOATCB
Job 41 in the BOATCB2
Job 41 in the BOBCV
Job 41 in the BOCNT
Job 41 in the BOECS
Job 41 in the BOGWICC
Job 41 in the BOHCB
Job 41 in the BOHCV
Job 41 in the BOHLNT
Job 41 in the BOHNTLTAL
Job 41 in the BOICB
Job 41 in the BOILNTAP
Job 41 in the BOITCV
Job 41 in the BOKCV2
Job 41 in the BOKHWOG
Job 41 in the BOKSSV
Job 41 in the BOLCB
Job 41 in the BOLCB2
Job 41 in the BOMCV
Job 41 in the BONAV
Job 41 in the BONCB
Job 41 in the BONLT
Job 41 in the BONUT2
Job 41 in the BOPLNT
Job 41 in the BOSCB
Job 41 in the BOSNC
Job 41 in the BOTLNT
Job 41 in the BOVCB
Job 41 in the BOYCB
Job 41 in the BPBB
Job 41 in the BPH
Job 41 in the BSB
Job 41 in the CCB
Job 41 in the CUV
Job 41 in the CUVS
Job 41 in the DBT
Job 41 in the DGDNT
Job 41 in the DHNT
Job 41 in the DNT
Job 41 in the ELBE
Job 41 in the EMTV
Job 41 in the ESV
Job 41 in the FBV
Job 41 in the FEB
Job 41 in the GGMNT
Job 41 in the GNT
Job 41 in the HARY
Job 41 in the HNT
Job 41 in the IRVA
Job 41 in the IRVB
Job 41 in the IRVG
Job 41 in the IRVH
Job 41 in the IRVK
Job 41 in the IRVM
Job 41 in the IRVM2
Job 41 in the IRVO
Job 41 in the IRVP
Job 41 in the IRVT
Job 41 in the IRVT2
Job 41 in the IRVU
Job 41 in the ISVN
Job 41 in the JSNT
Job 41 in the KAPI
Job 41 in the KBT1ETNIK
Job 41 in the KBV
Job 41 in the KJV
Job 41 in the KNFD
Job 41 in the LBA
Job 41 in the LBLA
Job 41 in the LNT
Job 41 in the LSV
Job 41 in the MAAL
Job 41 in the MBV
Job 41 in the MBV2
Job 41 in the MHNT
Job 41 in the MKNFD
Job 41 in the MNG
Job 41 in the MNT
Job 41 in the MNT2
Job 41 in the MRS1T
Job 41 in the NAA
Job 41 in the NASB
Job 41 in the NBLA
Job 41 in the NBS
Job 41 in the NBVTP
Job 41 in the NET2
Job 41 in the NIV11
Job 41 in the NNT
Job 41 in the NNT2
Job 41 in the NNT3
Job 41 in the PDDPT
Job 41 in the PFNT
Job 41 in the RMNT
Job 41 in the SBIAS
Job 41 in the SBIBS
Job 41 in the SBIBS2
Job 41 in the SBICS
Job 41 in the SBIDS
Job 41 in the SBIGS
Job 41 in the SBIHS
Job 41 in the SBIIS
Job 41 in the SBIIS2
Job 41 in the SBIIS3
Job 41 in the SBIKS
Job 41 in the SBIKS2
Job 41 in the SBIMS
Job 41 in the SBIOS
Job 41 in the SBIPS
Job 41 in the SBISS
Job 41 in the SBITS
Job 41 in the SBITS2
Job 41 in the SBITS3
Job 41 in the SBITS4
Job 41 in the SBIUS
Job 41 in the SBIVS
Job 41 in the SBT
Job 41 in the SBT1E
Job 41 in the SCHL
Job 41 in the SNT
Job 41 in the SUSU
Job 41 in the SUSU2
Job 41 in the SYNO
Job 41 in the TBIAOTANT
Job 41 in the TBT1E
Job 41 in the TBT1E2
Job 41 in the TFTIP
Job 41 in the TFTU
Job 41 in the TGNTATF3T
Job 41 in the THAI
Job 41 in the TNFD
Job 41 in the TNT
Job 41 in the TNTIK
Job 41 in the TNTIL
Job 41 in the TNTIN
Job 41 in the TNTIP
Job 41 in the TNTIZ
Job 41 in the TOMA
Job 41 in the TTENT
Job 41 in the UBG
Job 41 in the UGV
Job 41 in the UGV2
Job 41 in the UGV3
Job 41 in the VBL
Job 41 in the VDCC
Job 41 in the YALU
Job 41 in the YAPE
Job 41 in the YBVTP
Job 41 in the ZBP