Matthew 6 (BOKCV)

1 “Angalieni msitende wema wenu mbele ya watu ili wawaone. Kwa maana mkifanya hivyo, hamna thawabu kutoka kwa Baba yenu aliye mbinguni. 2 “Hivyo mnapowapa wahitaji, msipige panda mbele yenu kama wafanyavyo wanafiki katika masinagogi na mitaani, ili wasifiwe na watu. Amin nawaambia wao wamekwisha kupokea thawabu yao. 3 Lakini ninyi mtoapo sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kuume unachofanya, 4 ili sadaka yako iwe ni siri. Ndipo Baba yako wa mbinguni, yeye aonaye sirini atakupa thawabu kwa wazi. 5 “Nanyi msalipo, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Amin nawaambia, wao wamekwisha kupata thawabu yao. 6 Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Naye Baba yako aonaye sirini atakupa thawabu yako. 7 Nanyi mnaposali msiseme maneno kama wafanyavyo watu wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasikiwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao. 8 Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua kile mnachohitaji kabla hamjamwomba. 9 “Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba: “ ‘Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe. 10 Ufalme wako uje. Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni. 11 Utupatie riziki yetu ya kila siku. 12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tulivyokwisha kuwasamehe wadeni wetu. 13 Usitutie majaribuni, bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu [kwa kuwa Ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amen].’ 14 Kwa kuwa kama mkiwasamehe watu wengine wanapowakosea, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi pia. 15 Lakini msipowasamehe watu wengine makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. 16 “Mnapofunga, msiwe wenye huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kuwaonyesha wengine kwamba wamefunga. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha kupata thawabu yao kamilifu. 17 Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kunawa nyuso zenu 18 ili kufunga kwenu kusionekane na watu wengine ila Baba yenu aketiye mahali pa siri; naye Baba yenu aonaye sirini atawapa thawabu yenu kwa wazi. 19 “Msijiwekee hazina duniani, mahali ambapo nondo na kutu huharibu, nao wevi huvunja na kuiba. 20 Lakini jiwekeeni hazina mbinguni, mahali ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wevi hawavunji na kuiba. 21 Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo pia moyo wako utakapokuwa. 22 “Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni nyofu, mwili wako wote utajaa nuru. 23 Lakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote utajawa na giza. Kwa hiyo basi, kama nuru iliyomo ndani yako ni giza, hilo ni giza kuu namna gani! 24 “Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Kwa kuwa atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na Mali. 25 “Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini au mtakunywa nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa angani; wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani zaidi kuliko hao ndege? 27 Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake? 28 “Nanyi kwa nini mnajitaabisha kwa ajili ya mavazi? Fikirini maua ya shambani yameavyo. Hayafanyi kazi wala hayafumi. 29 Lakini nawaambia, hata Solomoni katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya hayo maua. 30 Basi ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya shambani, ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavika ninyi vizuri zaidi, enyi wa imani haba? 31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi, mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ 32 Watu wasiomjua Mungu ndio wanaoshindania hayo, lakini Baba yenu wa mbinguni anafahamu kuwa mnahitaji haya yote. 33 Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia. 34 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia yenyewe. Yatosha kwa siku masumbufu yake.

In Other Versions

Matthew 6 in the ANGEFD

Matthew 6 in the ANTPNG2D

Matthew 6 in the AS21

Matthew 6 in the BAGH

Matthew 6 in the BBPNG

Matthew 6 in the BBT1E

Matthew 6 in the BDS

Matthew 6 in the BEV

Matthew 6 in the BHAD

Matthew 6 in the BIB

Matthew 6 in the BLPT

Matthew 6 in the BNT

Matthew 6 in the BNTABOOT

Matthew 6 in the BNTLV

Matthew 6 in the BOATCB

Matthew 6 in the BOATCB2

Matthew 6 in the BOBCV

Matthew 6 in the BOCNT

Matthew 6 in the BOECS

Matthew 6 in the BOGWICC

Matthew 6 in the BOHCB

Matthew 6 in the BOHCV

Matthew 6 in the BOHLNT

Matthew 6 in the BOHNTLTAL

Matthew 6 in the BOICB

Matthew 6 in the BOILNTAP

Matthew 6 in the BOITCV

Matthew 6 in the BOKCV2

Matthew 6 in the BOKHWOG

Matthew 6 in the BOKSSV

Matthew 6 in the BOLCB

Matthew 6 in the BOLCB2

Matthew 6 in the BOMCV

Matthew 6 in the BONAV

Matthew 6 in the BONCB

Matthew 6 in the BONLT

Matthew 6 in the BONUT2

Matthew 6 in the BOPLNT

Matthew 6 in the BOSCB

Matthew 6 in the BOSNC

Matthew 6 in the BOTLNT

Matthew 6 in the BOVCB

Matthew 6 in the BOYCB

Matthew 6 in the BPBB

Matthew 6 in the BPH

Matthew 6 in the BSB

Matthew 6 in the CCB

Matthew 6 in the CUV

Matthew 6 in the CUVS

Matthew 6 in the DBT

Matthew 6 in the DGDNT

Matthew 6 in the DHNT

Matthew 6 in the DNT

Matthew 6 in the ELBE

Matthew 6 in the EMTV

Matthew 6 in the ESV

Matthew 6 in the FBV

Matthew 6 in the FEB

Matthew 6 in the GGMNT

Matthew 6 in the GNT

Matthew 6 in the HARY

Matthew 6 in the HNT

Matthew 6 in the IRVA

Matthew 6 in the IRVB

Matthew 6 in the IRVG

Matthew 6 in the IRVH

Matthew 6 in the IRVK

Matthew 6 in the IRVM

Matthew 6 in the IRVM2

Matthew 6 in the IRVO

Matthew 6 in the IRVP

Matthew 6 in the IRVT

Matthew 6 in the IRVT2

Matthew 6 in the IRVU

Matthew 6 in the ISVN

Matthew 6 in the JSNT

Matthew 6 in the KAPI

Matthew 6 in the KBT1ETNIK

Matthew 6 in the KBV

Matthew 6 in the KJV

Matthew 6 in the KNFD

Matthew 6 in the LBA

Matthew 6 in the LBLA

Matthew 6 in the LNT

Matthew 6 in the LSV

Matthew 6 in the MAAL

Matthew 6 in the MBV

Matthew 6 in the MBV2

Matthew 6 in the MHNT

Matthew 6 in the MKNFD

Matthew 6 in the MNG

Matthew 6 in the MNT

Matthew 6 in the MNT2

Matthew 6 in the MRS1T

Matthew 6 in the NAA

Matthew 6 in the NASB

Matthew 6 in the NBLA

Matthew 6 in the NBS

Matthew 6 in the NBVTP

Matthew 6 in the NET2

Matthew 6 in the NIV11

Matthew 6 in the NNT

Matthew 6 in the NNT2

Matthew 6 in the NNT3

Matthew 6 in the PDDPT

Matthew 6 in the PFNT

Matthew 6 in the RMNT

Matthew 6 in the SBIAS

Matthew 6 in the SBIBS

Matthew 6 in the SBIBS2

Matthew 6 in the SBICS

Matthew 6 in the SBIDS

Matthew 6 in the SBIGS

Matthew 6 in the SBIHS

Matthew 6 in the SBIIS

Matthew 6 in the SBIIS2

Matthew 6 in the SBIIS3

Matthew 6 in the SBIKS

Matthew 6 in the SBIKS2

Matthew 6 in the SBIMS

Matthew 6 in the SBIOS

Matthew 6 in the SBIPS

Matthew 6 in the SBISS

Matthew 6 in the SBITS

Matthew 6 in the SBITS2

Matthew 6 in the SBITS3

Matthew 6 in the SBITS4

Matthew 6 in the SBIUS

Matthew 6 in the SBIVS

Matthew 6 in the SBT

Matthew 6 in the SBT1E

Matthew 6 in the SCHL

Matthew 6 in the SNT

Matthew 6 in the SUSU

Matthew 6 in the SUSU2

Matthew 6 in the SYNO

Matthew 6 in the TBIAOTANT

Matthew 6 in the TBT1E

Matthew 6 in the TBT1E2

Matthew 6 in the TFTIP

Matthew 6 in the TFTU

Matthew 6 in the TGNTATF3T

Matthew 6 in the THAI

Matthew 6 in the TNFD

Matthew 6 in the TNT

Matthew 6 in the TNTIK

Matthew 6 in the TNTIL

Matthew 6 in the TNTIN

Matthew 6 in the TNTIP

Matthew 6 in the TNTIZ

Matthew 6 in the TOMA

Matthew 6 in the TTENT

Matthew 6 in the UBG

Matthew 6 in the UGV

Matthew 6 in the UGV2

Matthew 6 in the UGV3

Matthew 6 in the VBL

Matthew 6 in the VDCC

Matthew 6 in the YALU

Matthew 6 in the YAPE

Matthew 6 in the YBVTP

Matthew 6 in the ZBP