Numbers 20 (BOKCV)
1 Katika mwezi wa kwanza jumuiya yote ya Kiisraeli ilifika kwenye Jangwa la Sini, nao wakakaa Kadeshi. Miriamu akafa huko na kuzikwa. 2 Mahali hapo hapakuwa na maji kwa ajili ya jumuiya hiyo, nao wakakusanyika ili kumpinga Mose na Aroni. 3 Watu wakagombana na Mose, na kusema, “Laiti tungelikufa wakati ndugu zetu walipoanguka na kufa mbele za BWANA! 4 Kwa nini mmeileta jumuiya ya BWANA kwenye jangwa hili, ili tufe humu, sisi na mifugo yetu? 5 Kwa nini mmetupandisha kutoka Misri mpaka mahali hapa pa kutisha? Hapa hakuna nafaka wala tini, zabibu au makomamanga. Wala hapa hakuna maji ya kunywa!” 6 Mose na Aroni wakaondoka pale kwenye kusanyiko mpaka kwenye mlango wa Hema la Kukutania na kuanguka kifudifudi, nao utukufu wa BWANA ukawatokea. 7 BWANA akamwambia Mose, 8 “Chukua ile fimbo, na wewe na ndugu yako Aroni mkusanye kusanyiko pamoja. Nena na ule mwamba mbele ya macho yao, nao utatoa maji yake. Utatoa maji kutoka huo mwamba kwa ajili ya jumuiya ili wao na mifugo yao waweze kunywa.” 9 Kwa hiyo Mose akaichukua hiyo fimbo kutoka pale ilipokuwa mbele za BWANA kama alivyomwagiza. 10 Mose na Aroni wakakusanya kusanyiko pamoja mbele ya huo mwamba, naye Mose akawaambia, “Sikilizeni, enyi waasi. Je, ni lazima tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?” 11 Ndipo Mose akainua mkono wake na kuupiga mwamba mara mbili kwa fimbo yake. Maji yakabubujika, nayo jumuiya na mifugo yao wakanywa. 12 Lakini BWANA akamwambia Mose na Aroni, “Kwa sababu hamkuniamini mimi kiasi cha kuniheshimu kama mtakatifu machoni pa Waisraeli, hamtaiingiza jumuiya hii katika nchi ninayowapa.” 13 Haya yalikuwa maji ya Meriba, mahali pale ambapo Waisraeli waligombana na BWANA, naye akajionyesha mwenyewe huko kuwa mtakatifu katikati yao. 14 Mose akawatuma wajumbe kutoka Kadeshi kwenda kwa mfalme wa Edomu, akisema:“Hili ndilo ndugu yako Israeli asemalo: Wewe unafahamu juu ya taabu zote ambazo zimetupata. 15 Baba zetu walishuka Misri, nasi tumeishi huko miaka mingi. Wamisri walitutesa sisi na baba zetu, 16 lakini tulipomlilia BWANA, alisikia kilio chetu na akamtuma malaika akatutoa Misri.“Sasa tupo hapa Kadeshi, mji ulio mpakani mwa nchi yako. 17 Tafadhali turuhusu tupite katika nchi yako. Hatutapita katika shamba lolote, wala shamba la mizabibu, au kunywa maji kutoka kwenye kisima chochote. Tutasafiri kufuata njia kuu ya mfalme, na hatutageuka kulia wala kushoto mpaka tuwe tumeshapita nchi yako.” 18 Lakini mfalme wa Edomu akajibu:“Hamtapita hapa; kama mkijaribu kupita, tutatoka na kuwashambulia kwa upanga.” 19 Waisraeli wakajibu:“Sisi tutafuata njia kuu; tena ikiwa sisi au mifugo yetu tutakunywa tone la maji yenu, tutalilipia. Sisi tunataka tu kupita kwa miguu, wala si kitu kingine chochote.” 20 Watu wa Edomu wakajibu tena:“Hamwezi kupita hapa.”Ndipo watu wa Edomu wakatoka dhidi ya Waisraeli, jeshi kubwa lenye nguvu. 21 Kwa kuwa Waedomu waliwakatalia Waisraeli kupita katika nchi yao, Israeli wakageuka, wakawaacha. 22 Jumuiya yote ya Kiisraeli ikaondoka kutoka Kadeshi, wakafika kwenye Mlima Hori. 23 Kwenye Mlima Hori, karibu na mpaka wa Edomu, BWANA akamwambia Mose na Aroni, 24 “Aroni atakusanywa pamoja na watu wake. Hataingia katika nchi ninayowapa Waisraeli, kwa sababu ninyi wawili mliasi dhidi ya agizo langu kwenye maji ya Meriba. 25 Watwae Aroni na Eleazari mwanawe, na uwapandishe juu katika Mlima wa Hori. 26 Mvue Aroni mavazi yake, na umvike Eleazari mwanawe, kwa maana Aroni atakusanywa pamoja na watu wake; atakufa huko.” 27 Mose akafanya kama BWANA alivyomwagiza: Wakapanda Mlima Hori mbele ya macho ya jumuiya yote ya Kiisraeli. 28 Mose akamvua Aroni mavazi yake na kumvika mwanawe Eleazari mavazi hayo. Naye Aroni akafia pale juu ya mlima. Kisha Mose na Eleazari wakateremka kutoka mlimani. 29 Jumuiya yote ilipofahamu kwamba Aroni amekufa, jamaa yote ya Kiisraeli wakamwomboleza kwa siku thelathini.
In Other Versions
Numbers 20 in the ANGEFD
Numbers 20 in the ANTPNG2D
Numbers 20 in the AS21
Numbers 20 in the BAGH
Numbers 20 in the BBPNG
Numbers 20 in the BBT1E
Numbers 20 in the BDS
Numbers 20 in the BEV
Numbers 20 in the BHAD
Numbers 20 in the BIB
Numbers 20 in the BLPT
Numbers 20 in the BNT
Numbers 20 in the BNTABOOT
Numbers 20 in the BNTLV
Numbers 20 in the BOATCB
Numbers 20 in the BOATCB2
Numbers 20 in the BOBCV
Numbers 20 in the BOCNT
Numbers 20 in the BOECS
Numbers 20 in the BOGWICC
Numbers 20 in the BOHCB
Numbers 20 in the BOHCV
Numbers 20 in the BOHLNT
Numbers 20 in the BOHNTLTAL
Numbers 20 in the BOICB
Numbers 20 in the BOILNTAP
Numbers 20 in the BOITCV
Numbers 20 in the BOKCV2
Numbers 20 in the BOKHWOG
Numbers 20 in the BOKSSV
Numbers 20 in the BOLCB
Numbers 20 in the BOLCB2
Numbers 20 in the BOMCV
Numbers 20 in the BONAV
Numbers 20 in the BONCB
Numbers 20 in the BONLT
Numbers 20 in the BONUT2
Numbers 20 in the BOPLNT
Numbers 20 in the BOSCB
Numbers 20 in the BOSNC
Numbers 20 in the BOTLNT
Numbers 20 in the BOVCB
Numbers 20 in the BOYCB
Numbers 20 in the BPBB
Numbers 20 in the BPH
Numbers 20 in the BSB
Numbers 20 in the CCB
Numbers 20 in the CUV
Numbers 20 in the CUVS
Numbers 20 in the DBT
Numbers 20 in the DGDNT
Numbers 20 in the DHNT
Numbers 20 in the DNT
Numbers 20 in the ELBE
Numbers 20 in the EMTV
Numbers 20 in the ESV
Numbers 20 in the FBV
Numbers 20 in the FEB
Numbers 20 in the GGMNT
Numbers 20 in the GNT
Numbers 20 in the HARY
Numbers 20 in the HNT
Numbers 20 in the IRVA
Numbers 20 in the IRVB
Numbers 20 in the IRVG
Numbers 20 in the IRVH
Numbers 20 in the IRVK
Numbers 20 in the IRVM
Numbers 20 in the IRVM2
Numbers 20 in the IRVO
Numbers 20 in the IRVP
Numbers 20 in the IRVT
Numbers 20 in the IRVT2
Numbers 20 in the IRVU
Numbers 20 in the ISVN
Numbers 20 in the JSNT
Numbers 20 in the KAPI
Numbers 20 in the KBT1ETNIK
Numbers 20 in the KBV
Numbers 20 in the KJV
Numbers 20 in the KNFD
Numbers 20 in the LBA
Numbers 20 in the LBLA
Numbers 20 in the LNT
Numbers 20 in the LSV
Numbers 20 in the MAAL
Numbers 20 in the MBV
Numbers 20 in the MBV2
Numbers 20 in the MHNT
Numbers 20 in the MKNFD
Numbers 20 in the MNG
Numbers 20 in the MNT
Numbers 20 in the MNT2
Numbers 20 in the MRS1T
Numbers 20 in the NAA
Numbers 20 in the NASB
Numbers 20 in the NBLA
Numbers 20 in the NBS
Numbers 20 in the NBVTP
Numbers 20 in the NET2
Numbers 20 in the NIV11
Numbers 20 in the NNT
Numbers 20 in the NNT2
Numbers 20 in the NNT3
Numbers 20 in the PDDPT
Numbers 20 in the PFNT
Numbers 20 in the RMNT
Numbers 20 in the SBIAS
Numbers 20 in the SBIBS
Numbers 20 in the SBIBS2
Numbers 20 in the SBICS
Numbers 20 in the SBIDS
Numbers 20 in the SBIGS
Numbers 20 in the SBIHS
Numbers 20 in the SBIIS
Numbers 20 in the SBIIS2
Numbers 20 in the SBIIS3
Numbers 20 in the SBIKS
Numbers 20 in the SBIKS2
Numbers 20 in the SBIMS
Numbers 20 in the SBIOS
Numbers 20 in the SBIPS
Numbers 20 in the SBISS
Numbers 20 in the SBITS
Numbers 20 in the SBITS2
Numbers 20 in the SBITS3
Numbers 20 in the SBITS4
Numbers 20 in the SBIUS
Numbers 20 in the SBIVS
Numbers 20 in the SBT
Numbers 20 in the SBT1E
Numbers 20 in the SCHL
Numbers 20 in the SNT
Numbers 20 in the SUSU
Numbers 20 in the SUSU2
Numbers 20 in the SYNO
Numbers 20 in the TBIAOTANT
Numbers 20 in the TBT1E
Numbers 20 in the TBT1E2
Numbers 20 in the TFTIP
Numbers 20 in the TFTU
Numbers 20 in the TGNTATF3T
Numbers 20 in the THAI
Numbers 20 in the TNFD
Numbers 20 in the TNT
Numbers 20 in the TNTIK
Numbers 20 in the TNTIL
Numbers 20 in the TNTIN
Numbers 20 in the TNTIP
Numbers 20 in the TNTIZ
Numbers 20 in the TOMA
Numbers 20 in the TTENT
Numbers 20 in the UBG
Numbers 20 in the UGV
Numbers 20 in the UGV2
Numbers 20 in the UGV3
Numbers 20 in the VBL
Numbers 20 in the VDCC
Numbers 20 in the YALU
Numbers 20 in the YAPE
Numbers 20 in the YBVTP
Numbers 20 in the ZBP