Proverbs 10 (BOKCV)
1 Mithali za Solomoni:Mwana mwenye hekimahuleta furaha kwa baba yake,lakini mwana mpumbavuhuleta huzuni kwa mama yake. 2 Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai,lakini uadilifu huokoa kutoka mautini. 3 BWANA hawaachi waadilifu kukaa njaa,lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu. 4 Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskinilakini mikono yenye bidii huleta utajiri. 5 Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazini mwana mwenye hekima,lakini yeye alalaye wakati wa mavunoni mwana mwenye kuaibisha. 6 Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki,lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. 7 Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka,lakini jina la mwovu litaoza. 8 Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo,lakini mpumbavu apayukaye huangamia. 9 Mtu mwadilifu hutembea salama,lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa. 10 Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni,naye mpumbavu apayukaye huangamia. 11 Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima,lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. 12 Chuki huchochea faraka,lakini upendo husitiri mabaya yote. 13 Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua,lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu. 14 Wenye hekima huhifadhi maarifa,bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi. 15 Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome,bali ufukara ni maangamizi ya maskini. 16 Ujira wa wenye haki huwaletea uzima,lakini mapato ya waovu huwaletea adhabu. 17 Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima,lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine. 18 Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo,na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu. 19 Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani,lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara. 20 Ulimi wa mwenye haki ni fedha iliyo bora,bali moyo wa mwovu una thamani ndogo. 21 Midomo ya mwenye haki hulisha wengi,lakini wapumbavu hufa kwa kukosa ufahamu. 22 Baraka ya BWANA hutajirisha,wala haichanganyi huzuni. 23 Mpumbavu hufurahia tabia mbaya,lakini mtu mwenye ufahamu hupendezwa na hekima. 24 Kile anachoogopa mwovu ndicho kitakachompata;kile anachoonea shauku mwenye haki atapewa. 25 Tufani inapopita, waovu hutoweka,lakini wenye haki husimama imara milele. 26 Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho,ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma. 27 Kumcha BWANA huongeza urefu wa maisha,lakini miaka ya mwovu inafupishwa. 28 Tarajio la mwenye haki ni furaha,bali matumaini ya mwovu huwa si kitu. 29 Njia ya BWANA ni kimbilio kwa wenye haki,lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya. 30 Kamwe wenye haki hawataondolewa,bali waovu hawatasalia katika nchi. 31 Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima,bali ulimi wa upotovu utakatwa. 32 Midomo ya wenye haki inajua kile kinachofaa,bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu.
In Other Versions
Proverbs 10 in the ANGEFD
Proverbs 10 in the ANTPNG2D
Proverbs 10 in the AS21
Proverbs 10 in the BAGH
Proverbs 10 in the BBPNG
Proverbs 10 in the BBT1E
Proverbs 10 in the BDS
Proverbs 10 in the BEV
Proverbs 10 in the BHAD
Proverbs 10 in the BIB
Proverbs 10 in the BLPT
Proverbs 10 in the BNT
Proverbs 10 in the BNTABOOT
Proverbs 10 in the BNTLV
Proverbs 10 in the BOATCB
Proverbs 10 in the BOATCB2
Proverbs 10 in the BOBCV
Proverbs 10 in the BOCNT
Proverbs 10 in the BOECS
Proverbs 10 in the BOGWICC
Proverbs 10 in the BOHCB
Proverbs 10 in the BOHCV
Proverbs 10 in the BOHLNT
Proverbs 10 in the BOHNTLTAL
Proverbs 10 in the BOICB
Proverbs 10 in the BOILNTAP
Proverbs 10 in the BOITCV
Proverbs 10 in the BOKCV2
Proverbs 10 in the BOKHWOG
Proverbs 10 in the BOKSSV
Proverbs 10 in the BOLCB
Proverbs 10 in the BOLCB2
Proverbs 10 in the BOMCV
Proverbs 10 in the BONAV
Proverbs 10 in the BONCB
Proverbs 10 in the BONLT
Proverbs 10 in the BONUT2
Proverbs 10 in the BOPLNT
Proverbs 10 in the BOSCB
Proverbs 10 in the BOSNC
Proverbs 10 in the BOTLNT
Proverbs 10 in the BOVCB
Proverbs 10 in the BOYCB
Proverbs 10 in the BPBB
Proverbs 10 in the BPH
Proverbs 10 in the BSB
Proverbs 10 in the CCB
Proverbs 10 in the CUV
Proverbs 10 in the CUVS
Proverbs 10 in the DBT
Proverbs 10 in the DGDNT
Proverbs 10 in the DHNT
Proverbs 10 in the DNT
Proverbs 10 in the ELBE
Proverbs 10 in the EMTV
Proverbs 10 in the ESV
Proverbs 10 in the FBV
Proverbs 10 in the FEB
Proverbs 10 in the GGMNT
Proverbs 10 in the GNT
Proverbs 10 in the HARY
Proverbs 10 in the HNT
Proverbs 10 in the IRVA
Proverbs 10 in the IRVB
Proverbs 10 in the IRVG
Proverbs 10 in the IRVH
Proverbs 10 in the IRVK
Proverbs 10 in the IRVM
Proverbs 10 in the IRVM2
Proverbs 10 in the IRVO
Proverbs 10 in the IRVP
Proverbs 10 in the IRVT
Proverbs 10 in the IRVT2
Proverbs 10 in the IRVU
Proverbs 10 in the ISVN
Proverbs 10 in the JSNT
Proverbs 10 in the KAPI
Proverbs 10 in the KBT1ETNIK
Proverbs 10 in the KBV
Proverbs 10 in the KJV
Proverbs 10 in the KNFD
Proverbs 10 in the LBA
Proverbs 10 in the LBLA
Proverbs 10 in the LNT
Proverbs 10 in the LSV
Proverbs 10 in the MAAL
Proverbs 10 in the MBV
Proverbs 10 in the MBV2
Proverbs 10 in the MHNT
Proverbs 10 in the MKNFD
Proverbs 10 in the MNG
Proverbs 10 in the MNT
Proverbs 10 in the MNT2
Proverbs 10 in the MRS1T
Proverbs 10 in the NAA
Proverbs 10 in the NASB
Proverbs 10 in the NBLA
Proverbs 10 in the NBS
Proverbs 10 in the NBVTP
Proverbs 10 in the NET2
Proverbs 10 in the NIV11
Proverbs 10 in the NNT
Proverbs 10 in the NNT2
Proverbs 10 in the NNT3
Proverbs 10 in the PDDPT
Proverbs 10 in the PFNT
Proverbs 10 in the RMNT
Proverbs 10 in the SBIAS
Proverbs 10 in the SBIBS
Proverbs 10 in the SBIBS2
Proverbs 10 in the SBICS
Proverbs 10 in the SBIDS
Proverbs 10 in the SBIGS
Proverbs 10 in the SBIHS
Proverbs 10 in the SBIIS
Proverbs 10 in the SBIIS2
Proverbs 10 in the SBIIS3
Proverbs 10 in the SBIKS
Proverbs 10 in the SBIKS2
Proverbs 10 in the SBIMS
Proverbs 10 in the SBIOS
Proverbs 10 in the SBIPS
Proverbs 10 in the SBISS
Proverbs 10 in the SBITS
Proverbs 10 in the SBITS2
Proverbs 10 in the SBITS3
Proverbs 10 in the SBITS4
Proverbs 10 in the SBIUS
Proverbs 10 in the SBIVS
Proverbs 10 in the SBT
Proverbs 10 in the SBT1E
Proverbs 10 in the SCHL
Proverbs 10 in the SNT
Proverbs 10 in the SUSU
Proverbs 10 in the SUSU2
Proverbs 10 in the SYNO
Proverbs 10 in the TBIAOTANT
Proverbs 10 in the TBT1E
Proverbs 10 in the TBT1E2
Proverbs 10 in the TFTIP
Proverbs 10 in the TFTU
Proverbs 10 in the TGNTATF3T
Proverbs 10 in the THAI
Proverbs 10 in the TNFD
Proverbs 10 in the TNT
Proverbs 10 in the TNTIK
Proverbs 10 in the TNTIL
Proverbs 10 in the TNTIN
Proverbs 10 in the TNTIP
Proverbs 10 in the TNTIZ
Proverbs 10 in the TOMA
Proverbs 10 in the TTENT
Proverbs 10 in the UBG
Proverbs 10 in the UGV
Proverbs 10 in the UGV2
Proverbs 10 in the UGV3
Proverbs 10 in the VBL
Proverbs 10 in the VDCC
Proverbs 10 in the YALU
Proverbs 10 in the YAPE
Proverbs 10 in the YBVTP
Proverbs 10 in the ZBP