Psalms 125 (BOKCV)
undefined Wimbo wa kwenda juu. 1 Wale wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni,ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele. 2 Kama milima inavyozunguka Yerusalemu,ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wakesasa na hata milele. 3 Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchiwaliopewa wenye haki,ili wenye haki wasije wakatumiamikono yao kutenda ubaya. 4 Ee BWANA, watendee mema walio wema,wale walio wanyofu wa moyo. 5 Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka, BWANA atawafukuza pamoja na watenda mabaya. Amani iwe juu ya Israeli.