Psalms 126 (BOKCV)
undefined Wimbo wa kwenda juu. 1 BWANA alipowarejeza mateka Sayuni,tulikuwa kama watu walioota ndoto. 2 Vinywa vyetu vilijaa kicheko,ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,“BWANA amewatendea mambo makuu.” 3 BWANA ametutendea mambo makuu,nasi tumejaa furaha. 4 Ee BWANA, turejeshee watu wetu waliotekwa,kama vijito katika Negebu. 5 Wapandao kwa machoziwatavuna kwa nyimbo za shangwe. 6 Yeye azichukuaye mbegu zakekwenda kupanda, huku akilia,atarudi kwa nyimbo za shangwe,akichukua miganda ya mavuno yake.