Psalms 129 (BOKCV)
undefined Wimbo wa kwenda juu. 1 Wamenionea mno tangu ujana wangu;Israeli na aseme sasa: 2 wamenionea mno tangu ujana wangu,lakini bado hawajanishinda. 3 Wakulima wamelima mgongo wangu,na kufanya mifereji yao mirefu. 4 Lakini BWANA ni mwenye haki;amenifungua toka kamba za waovu. 5 Wale wote waichukiao Sayunina warudishwe nyuma kwa aibu. 6 Wawe kama majani juu ya paa,ambayo hunyauka kabla hayajakua; 7 kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,wala akusanyaye kujaza mikono yake. 8 Wale wapitao karibu na wasiseme,“Baraka ya BWANA iwe juu yako;tunakubariki katika jina la BWANA.”