Psalms 13 (BOKCV)
undefined Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Mpaka lini, Ee BWANA? Je, utanisahau milele?Utanificha uso wako mpaka lini? 2 Nitapambana na mawazo yangu mpaka lini,na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu?Adui zangu watanishinda mpaka lini? 3 Nitazame, unijibu, Ee BWANA Mungu wangu.Yatie nuru macho yangu,ama sivyo nitalala usingizi wa mauti. 4 Adui yangu atasema, “Nimemshinda,”nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka. 5 Lakini ninategemea upendo wako usiokoma;moyo wangu unashangilia katika wokovu wako. 6 Nitamwimbia BWANA,kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.