Psalms 69 (BOKCV)

undefined Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi.” Zaburi ya Daudi. 1 Ee Mungu, niokoe,kwa maana maji yamenifika shingoni. 2 Ninazama kwenye vilindi vya matope,pasipo mahali pa kukanyaga,Nimefika kwenye maji makuu,mafuriko yamenigharikisha. 3 Nimechoka kwa kuomba msaada,koo langu limekauka.Macho yangu yanafifia,nikimtafuta Mungu wangu. 4 Wale wanaonichukia bila sababuni wengi kuliko nywele za kichwa changu;wengi ni adui kwangu bila sababu,wale wanaotafuta kuniangamiza.Ninalazimishwa kurudishakitu ambacho sikuiba. 5 Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu,wala hatia yangu haikufichika kwako. 6 Ee Bwana, ewe BWANA Mwenye Nguvu Zote,wakutumainio wasiaibishwekwa ajili yangu;wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu,Ee Mungu wa Israeli. 7 Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako,aibu imefunika uso wangu. 8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu,mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe. 9 Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila,matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia. 10 Ninapolia na kufunga,lazima nivumilie matusi. 11 Ninapovaa nguo ya gunia,watu hunidharau. 12 Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga,nimekuwa wimbo wa walevi. 13 Lakini Ee BWANA, ninakuomba,kwa wakati ukupendezao;katika upendo wako mkuu, Ee Mungu,unijibu kwa wokovu wako wa hakika. 14 Uniokoe katika matope,usiniache nizame;niokoe na hao wanichukiao,kutoka kwenye vilindi vya maji. 15 Usiache mafuriko yanigharikisheau vilindi vinimeze,au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu. 16 Ee BWANA, unijibu, kwa wema wa upendo wako;kwa huruma zako nyingi unigeukie. 17 Usimfiche mtumishi wako uso wako,uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida. 18 Njoo karibu uniokoe,nikomboe kwa sababu ya adui zangu. 19 Unajua jinsi ninavyodharauliwa,kufedheheshwa na kuaibishwa,adui zangu wote unawajua. 20 Dharau zimenivunja moyona nimekata tamaa,nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata,wa kunituliza, lakini sikumpata. 21 Waliweka nyongo katika chakula changuna walinipa siki nilipokuwa na kiu. 22 Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego,nayo iwe upatilizo na tanzi. 23 Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona,nayo migongo yao iinamishwe daima. 24 Uwamwagie ghadhabu yako,hasira yako kali na iwapate. 25 Mahali pao na pawe ukiwa,wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao. 26 Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi,na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza. 27 Walipize uovu juu ya uovu,usiwaache washiriki katika wokovu wako. 28 Wafutwe kutoka kitabu cha uzimana wasiorodheshwe pamoja na wenye haki. 29 Mimi niko katika maumivu na dhiki;Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi. 30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani. 31 Hili litampendeza BWANA kuliko ngʼombe dume,zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake. 32 Maskini wataona na kufurahi:ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi! 33 BWANA huwasikia wahitajiwala hadharau watu wake waliotekwa. 34 Mbingu na dunia zimsifu,bahari na vyote viendavyo ndani yake, 35 kwa maana Mungu ataiokoa Sayunina kuijenga tena miji ya Yuda.Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki, 36 watoto wa watumishi wake watairithina wale wote walipendao jina lakewataishi humo.

In Other Versions

Psalms 69 in the ANGEFD

Psalms 69 in the ANTPNG2D

Psalms 69 in the AS21

Psalms 69 in the BAGH

Psalms 69 in the BBPNG

Psalms 69 in the BBT1E

Psalms 69 in the BDS

Psalms 69 in the BEV

Psalms 69 in the BHAD

Psalms 69 in the BIB

Psalms 69 in the BLPT

Psalms 69 in the BNT

Psalms 69 in the BNTABOOT

Psalms 69 in the BNTLV

Psalms 69 in the BOATCB

Psalms 69 in the BOATCB2

Psalms 69 in the BOBCV

Psalms 69 in the BOCNT

Psalms 69 in the BOECS

Psalms 69 in the BOGWICC

Psalms 69 in the BOHCB

Psalms 69 in the BOHCV

Psalms 69 in the BOHLNT

Psalms 69 in the BOHNTLTAL

Psalms 69 in the BOICB

Psalms 69 in the BOILNTAP

Psalms 69 in the BOITCV

Psalms 69 in the BOKCV2

Psalms 69 in the BOKHWOG

Psalms 69 in the BOKSSV

Psalms 69 in the BOLCB

Psalms 69 in the BOLCB2

Psalms 69 in the BOMCV

Psalms 69 in the BONAV

Psalms 69 in the BONCB

Psalms 69 in the BONLT

Psalms 69 in the BONUT2

Psalms 69 in the BOPLNT

Psalms 69 in the BOSCB

Psalms 69 in the BOSNC

Psalms 69 in the BOTLNT

Psalms 69 in the BOVCB

Psalms 69 in the BOYCB

Psalms 69 in the BPBB

Psalms 69 in the BPH

Psalms 69 in the BSB

Psalms 69 in the CCB

Psalms 69 in the CUV

Psalms 69 in the CUVS

Psalms 69 in the DBT

Psalms 69 in the DGDNT

Psalms 69 in the DHNT

Psalms 69 in the DNT

Psalms 69 in the ELBE

Psalms 69 in the EMTV

Psalms 69 in the ESV

Psalms 69 in the FBV

Psalms 69 in the FEB

Psalms 69 in the GGMNT

Psalms 69 in the GNT

Psalms 69 in the HARY

Psalms 69 in the HNT

Psalms 69 in the IRVA

Psalms 69 in the IRVB

Psalms 69 in the IRVG

Psalms 69 in the IRVH

Psalms 69 in the IRVK

Psalms 69 in the IRVM

Psalms 69 in the IRVM2

Psalms 69 in the IRVO

Psalms 69 in the IRVP

Psalms 69 in the IRVT

Psalms 69 in the IRVT2

Psalms 69 in the IRVU

Psalms 69 in the ISVN

Psalms 69 in the JSNT

Psalms 69 in the KAPI

Psalms 69 in the KBT1ETNIK

Psalms 69 in the KBV

Psalms 69 in the KJV

Psalms 69 in the KNFD

Psalms 69 in the LBA

Psalms 69 in the LBLA

Psalms 69 in the LNT

Psalms 69 in the LSV

Psalms 69 in the MAAL

Psalms 69 in the MBV

Psalms 69 in the MBV2

Psalms 69 in the MHNT

Psalms 69 in the MKNFD

Psalms 69 in the MNG

Psalms 69 in the MNT

Psalms 69 in the MNT2

Psalms 69 in the MRS1T

Psalms 69 in the NAA

Psalms 69 in the NASB

Psalms 69 in the NBLA

Psalms 69 in the NBS

Psalms 69 in the NBVTP

Psalms 69 in the NET2

Psalms 69 in the NIV11

Psalms 69 in the NNT

Psalms 69 in the NNT2

Psalms 69 in the NNT3

Psalms 69 in the PDDPT

Psalms 69 in the PFNT

Psalms 69 in the RMNT

Psalms 69 in the SBIAS

Psalms 69 in the SBIBS

Psalms 69 in the SBIBS2

Psalms 69 in the SBICS

Psalms 69 in the SBIDS

Psalms 69 in the SBIGS

Psalms 69 in the SBIHS

Psalms 69 in the SBIIS

Psalms 69 in the SBIIS2

Psalms 69 in the SBIIS3

Psalms 69 in the SBIKS

Psalms 69 in the SBIKS2

Psalms 69 in the SBIMS

Psalms 69 in the SBIOS

Psalms 69 in the SBIPS

Psalms 69 in the SBISS

Psalms 69 in the SBITS

Psalms 69 in the SBITS2

Psalms 69 in the SBITS3

Psalms 69 in the SBITS4

Psalms 69 in the SBIUS

Psalms 69 in the SBIVS

Psalms 69 in the SBT

Psalms 69 in the SBT1E

Psalms 69 in the SCHL

Psalms 69 in the SNT

Psalms 69 in the SUSU

Psalms 69 in the SUSU2

Psalms 69 in the SYNO

Psalms 69 in the TBIAOTANT

Psalms 69 in the TBT1E

Psalms 69 in the TBT1E2

Psalms 69 in the TFTIP

Psalms 69 in the TFTU

Psalms 69 in the TGNTATF3T

Psalms 69 in the THAI

Psalms 69 in the TNFD

Psalms 69 in the TNT

Psalms 69 in the TNTIK

Psalms 69 in the TNTIL

Psalms 69 in the TNTIN

Psalms 69 in the TNTIP

Psalms 69 in the TNTIZ

Psalms 69 in the TOMA

Psalms 69 in the TTENT

Psalms 69 in the UBG

Psalms 69 in the UGV

Psalms 69 in the UGV2

Psalms 69 in the UGV3

Psalms 69 in the VBL

Psalms 69 in the VDCC

Psalms 69 in the YALU

Psalms 69 in the YAPE

Psalms 69 in the YBVTP

Psalms 69 in the ZBP