Romans 3 (BOKCV)
1 Basi kuna faida gani kuwa Myahudi? Au kuna thamani gani katika tohara? 2 Kuna faida kubwa kwa kila namna! Kwanza kabisa, Wayahudi wamekabidhiwa lile Neno halisi la Mungu. 3 Ingekuwaje kama wengine hawakuwa na imani? Je, kutokuamini kwao kungebatilisha uaminifu wa Mungu? 4 La hasha! Mungu na aonekane mwenye haki, na kila mwanadamu kuwa mwongo, kama ilivyoandikwa:“Ili uthibitike kuwa wa kweli unaponena,na ukashinde utoapo hukumu.” 5 Ikiwa uovu wetu unathibitisha haki ya Mungu waziwazi, tuseme nini basi? Je, Mungu kuileta ghadhabu yake juu yetu ni kwamba yeye si mwenye haki? (Nanena kibinadamu.) 6 La hasha! Kama hivyo ndivyo ilivyo, Mungu angehukumuje ulimwengu? 7 Mtu aweza kuuliza, “Kama uongo wangu unasaidia kuonyesha kweli ya Mungu na kuzidisha utukufu wake, kwa nini basi mimi nahukumiwa kuwa mwenye dhambi?” 8 Nasi kwa nini tusiseme, kama wengine wanavyotusingizia kuwa tunasema, “Tutende maovu ili mema yapate kuja?” Wao wanastahili hukumu yao. 9 Tusemeje basi? Je, sisi ni bora kuwaliko wao? La hasha! Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyovyote kwamba Wayahudi na watu wa Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi. 10 Kama ilivyoandikwa:“Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja. 11 Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu,hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu. 12 Wote wamepotoka,wote wameoza pamoja;hakuna atendaye mema,naam, hakuna hata mmoja.” 13 “Makoo yao ni makaburi wazi;kwa ndimi zao wao hufanya udanganyifu.”“Sumu ya nyoka iko midomoni mwao.” 14 “Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.” 15 “Miguu yao ina haraka kumwaga damu; 16 maangamizi na taabu viko katika njia zao, 17 wala njia ya amani hawaijui.” 18 “Hakuna hofu ya Mungu machoni pao.” 19 Basi tunajua ya kwamba chochote sheria inachosema, inawaambia wale walio chini ya sheria ili kila kinywa kinyamazishwe na ulimwengu wote uwajibike kwa Mungu. 20 Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa matendo ya sheria, kwa maana sheria hutufanya tuitambue dhambi. 21 Lakini sasa, haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa pasipo sheria, ambayo Sheria na Manabii wanaishuhudia. 22 Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Yesu Kristo kwa wote wamwaminio. Kwa maana hapo hakuna tofauti, 23 kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, 24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu. 25 Yeye ambaye Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwa sababu kwa ustahimili wake aliziachilia zile dhambi zilizotangulia kufanywa. 26 Alifanya hivyo ili kuonyesha haki yake wakati huu, ili yeye awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yule anayemwamini Yesu. 27 Basi, kujivuna kuko wapi? Kumewekwa mbali. Kwa sheria gani? Je, ni kwa ile ya matendo? La hasha, bali kwa ile sheria ya imani. 28 Kwa maana twaona kwamba mwanadamu huhesabiwa haki kwa njia ya imani wala si kwa matendo ya sheria. 29 Je, Mungu ni Mungu wa Wayahudi peke yao? Je, yeye si Mungu wa watu wa Mataifa pia? Naam, yeye ni Mungu wa watu wa Mataifa pia. 30 Basi kwa kuwa tuna Mungu mmoja tu, atawahesabia haki wale waliotahiriwa kwa imani na wale wasiotahiriwa kwa imani iyo hiyo. 31 Je, basi ni kwamba tunaibatilisha sheria kwa imani hii? La, hasha! Badala yake tunaithibitisha sheria.
In Other Versions
Romans 3 in the ANGEFD
Romans 3 in the ANTPNG2D
Romans 3 in the AS21
Romans 3 in the BAGH
Romans 3 in the BBPNG
Romans 3 in the BBT1E
Romans 3 in the BDS
Romans 3 in the BEV
Romans 3 in the BHAD
Romans 3 in the BIB
Romans 3 in the BLPT
Romans 3 in the BNT
Romans 3 in the BNTABOOT
Romans 3 in the BNTLV
Romans 3 in the BOATCB
Romans 3 in the BOATCB2
Romans 3 in the BOBCV
Romans 3 in the BOCNT
Romans 3 in the BOECS
Romans 3 in the BOGWICC
Romans 3 in the BOHCB
Romans 3 in the BOHCV
Romans 3 in the BOHLNT
Romans 3 in the BOHNTLTAL
Romans 3 in the BOICB
Romans 3 in the BOILNTAP
Romans 3 in the BOITCV
Romans 3 in the BOKCV2
Romans 3 in the BOKHWOG
Romans 3 in the BOKSSV
Romans 3 in the BOLCB
Romans 3 in the BOLCB2
Romans 3 in the BOMCV
Romans 3 in the BONAV
Romans 3 in the BONCB
Romans 3 in the BONLT
Romans 3 in the BONUT2
Romans 3 in the BOPLNT
Romans 3 in the BOSCB
Romans 3 in the BOSNC
Romans 3 in the BOTLNT
Romans 3 in the BOVCB
Romans 3 in the BOYCB
Romans 3 in the BPBB
Romans 3 in the BPH
Romans 3 in the BSB
Romans 3 in the CCB
Romans 3 in the CUV
Romans 3 in the CUVS
Romans 3 in the DBT
Romans 3 in the DGDNT
Romans 3 in the DHNT
Romans 3 in the DNT
Romans 3 in the ELBE
Romans 3 in the EMTV
Romans 3 in the ESV
Romans 3 in the FBV
Romans 3 in the FEB
Romans 3 in the GGMNT
Romans 3 in the GNT
Romans 3 in the HARY
Romans 3 in the HNT
Romans 3 in the IRVA
Romans 3 in the IRVB
Romans 3 in the IRVG
Romans 3 in the IRVH
Romans 3 in the IRVK
Romans 3 in the IRVM
Romans 3 in the IRVM2
Romans 3 in the IRVO
Romans 3 in the IRVP
Romans 3 in the IRVT
Romans 3 in the IRVT2
Romans 3 in the IRVU
Romans 3 in the ISVN
Romans 3 in the JSNT
Romans 3 in the KAPI
Romans 3 in the KBT1ETNIK
Romans 3 in the KBV
Romans 3 in the KJV
Romans 3 in the KNFD
Romans 3 in the LBA
Romans 3 in the LBLA
Romans 3 in the LNT
Romans 3 in the LSV
Romans 3 in the MAAL
Romans 3 in the MBV
Romans 3 in the MBV2
Romans 3 in the MHNT
Romans 3 in the MKNFD
Romans 3 in the MNG
Romans 3 in the MNT
Romans 3 in the MNT2
Romans 3 in the MRS1T
Romans 3 in the NAA
Romans 3 in the NASB
Romans 3 in the NBLA
Romans 3 in the NBS
Romans 3 in the NBVTP
Romans 3 in the NET2
Romans 3 in the NIV11
Romans 3 in the NNT
Romans 3 in the NNT2
Romans 3 in the NNT3
Romans 3 in the PDDPT
Romans 3 in the PFNT
Romans 3 in the RMNT
Romans 3 in the SBIAS
Romans 3 in the SBIBS
Romans 3 in the SBIBS2
Romans 3 in the SBICS
Romans 3 in the SBIDS
Romans 3 in the SBIGS
Romans 3 in the SBIHS
Romans 3 in the SBIIS
Romans 3 in the SBIIS2
Romans 3 in the SBIIS3
Romans 3 in the SBIKS
Romans 3 in the SBIKS2
Romans 3 in the SBIMS
Romans 3 in the SBIOS
Romans 3 in the SBIPS
Romans 3 in the SBISS
Romans 3 in the SBITS
Romans 3 in the SBITS2
Romans 3 in the SBITS3
Romans 3 in the SBITS4
Romans 3 in the SBIUS
Romans 3 in the SBIVS
Romans 3 in the SBT
Romans 3 in the SBT1E
Romans 3 in the SCHL
Romans 3 in the SNT
Romans 3 in the SUSU
Romans 3 in the SUSU2
Romans 3 in the SYNO
Romans 3 in the TBIAOTANT
Romans 3 in the TBT1E
Romans 3 in the TBT1E2
Romans 3 in the TFTIP
Romans 3 in the TFTU
Romans 3 in the TGNTATF3T
Romans 3 in the THAI
Romans 3 in the TNFD
Romans 3 in the TNT
Romans 3 in the TNTIK
Romans 3 in the TNTIL
Romans 3 in the TNTIN
Romans 3 in the TNTIP
Romans 3 in the TNTIZ
Romans 3 in the TOMA
Romans 3 in the TTENT
Romans 3 in the UBG
Romans 3 in the UGV
Romans 3 in the UGV2
Romans 3 in the UGV3
Romans 3 in the VBL
Romans 3 in the VDCC
Romans 3 in the YALU
Romans 3 in the YAPE
Romans 3 in the YBVTP
Romans 3 in the ZBP