Ruth 3 (BOKCV)
1 Kisha Naomi akamwambia mkwewe, “Binti yangu, je, nisingelikutafutia pumziko ambako utatunzika vyema? 2 Je, Boazi, ambaye umekuwa pamoja na watumishi wake wasichana, si jamaa yetu wa karibu? Usiku wa leo atakuwa anapepeta ngano kwenye sakafu ya kupuria. 3 Basi oga na ukajipake marashi, ujivalie nguo zako nzuri. Kisha uende kwenye sakafu ya kupuria, lakini angalia asijue kwamba upo pale mpaka atakapomaliza kula na kunywa. 4 Atakapokwenda kulala, angalia mahali atakapolala. Kisha uende ufunue miguu yake, ulale. Naye atakuambia utakalofanya.” 5 Ruthu akajibu, “Lolote usemalo nitatenda.” 6 Basi akashuka mpaka kwenye sakafu ya kupuria, akafanya kila kitu mama mkwe wake alichomwambia kufanya. 7 Wakati Boazi alipomaliza kula na kunywa, naye akawa amejawa na furaha, alikwenda kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthu akanyemelea polepole, akafunua miguu yake, na akalala. 8 Usiku wa manane, kitu kilimshtua Boazi, akajigeuza, akagundua yupo mwanamke amelala miguuni pake. 9 Akauliza, “Wewe ni nani?”Akajibu, “Ni mimi Ruthu, mjakazi wako. Uitande nguo yako juu yangu, kwa sababu wewe ndiwe jamaa wa karibu wa kutukomboa.” 10 Akamwambia, “Binti yangu, ubarikiwe na BWANA. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonyesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini. 11 Sasa, binti yangu, usiogope. Nitakufanyia yote uliyoomba. Kwa maana mji wote wa watu wangu wanakujua ya kwamba wewe ni mwanamke mwenye tabia nzuri. 12 Ingawa ni kweli kwamba mimi ndiye jamaa aliye karibu, bado kuna mtu mwingine wa jamaa aliye karibu zaidi wa kukomboa kuliko mimi. 13 Wewe kaa hapa usiku huu, kisha asubuhi kama akikubali kukomboa, vyema na akomboe. La sivyo kama hayuko tayari, hakika kama BWANA aishivyo nitafanya hivyo. Lala hapa mpaka asubuhi.” 14 Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake mpaka asubuhi, akaondoka mapema pasipo mtu kuweza kumtambua mwenzake, maana Boazi alisema, “Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika kwenye sakafu ya kupuria.” 15 Pia akamwambia, “Leta shela yako uliyoivaa, uitandaze.” Naye alipoitandaza, akamimina vipimo sita vya shayiri, akamtwika. Kisha Ruthu akarudi zake mjini. 16 Basi Ruthu alipofika kwa mama mkwe wake Naomi, akamuuliza, “Je, binti yangu, ilikuwaje huko?”Ndipo akamwelezea kila kitu Boazi alichomfanyia. 17 Akaendelea kusema, “Amenipa shayiri vipimo sita akisema, ‘Usiende kwa mama mkwe wako mikono mitupu.’ ” 18 Kisha Naomi akasema, “Subiri binti yangu, mpaka utakapojua kwamba hili jambo limekwendaje. Kwa sababu mtu huyu hatatulia mpaka akamilishe jambo hili leo.”
In Other Versions
Ruth 3 in the ANGEFD
Ruth 3 in the ANTPNG2D
Ruth 3 in the AS21
Ruth 3 in the BAGH
Ruth 3 in the BBPNG
Ruth 3 in the BBT1E
Ruth 3 in the BDS
Ruth 3 in the BEV
Ruth 3 in the BHAD
Ruth 3 in the BIB
Ruth 3 in the BLPT
Ruth 3 in the BNT
Ruth 3 in the BNTABOOT
Ruth 3 in the BNTLV
Ruth 3 in the BOATCB
Ruth 3 in the BOATCB2
Ruth 3 in the BOBCV
Ruth 3 in the BOCNT
Ruth 3 in the BOECS
Ruth 3 in the BOGWICC
Ruth 3 in the BOHCB
Ruth 3 in the BOHCV
Ruth 3 in the BOHLNT
Ruth 3 in the BOHNTLTAL
Ruth 3 in the BOICB
Ruth 3 in the BOILNTAP
Ruth 3 in the BOITCV
Ruth 3 in the BOKCV2
Ruth 3 in the BOKHWOG
Ruth 3 in the BOKSSV
Ruth 3 in the BOLCB
Ruth 3 in the BOLCB2
Ruth 3 in the BOMCV
Ruth 3 in the BONAV
Ruth 3 in the BONCB
Ruth 3 in the BONLT
Ruth 3 in the BONUT2
Ruth 3 in the BOPLNT
Ruth 3 in the BOSCB
Ruth 3 in the BOSNC
Ruth 3 in the BOTLNT
Ruth 3 in the BOVCB
Ruth 3 in the BOYCB
Ruth 3 in the BPBB
Ruth 3 in the BPH
Ruth 3 in the BSB
Ruth 3 in the CCB
Ruth 3 in the CUV
Ruth 3 in the CUVS
Ruth 3 in the DBT
Ruth 3 in the DGDNT
Ruth 3 in the DHNT
Ruth 3 in the DNT
Ruth 3 in the ELBE
Ruth 3 in the EMTV
Ruth 3 in the ESV
Ruth 3 in the FBV
Ruth 3 in the FEB
Ruth 3 in the GGMNT
Ruth 3 in the GNT
Ruth 3 in the HARY
Ruth 3 in the HNT
Ruth 3 in the IRVA
Ruth 3 in the IRVB
Ruth 3 in the IRVG
Ruth 3 in the IRVH
Ruth 3 in the IRVK
Ruth 3 in the IRVM
Ruth 3 in the IRVM2
Ruth 3 in the IRVO
Ruth 3 in the IRVP
Ruth 3 in the IRVT
Ruth 3 in the IRVT2
Ruth 3 in the IRVU
Ruth 3 in the ISVN
Ruth 3 in the JSNT
Ruth 3 in the KAPI
Ruth 3 in the KBT1ETNIK
Ruth 3 in the KBV
Ruth 3 in the KJV
Ruth 3 in the KNFD
Ruth 3 in the LBA
Ruth 3 in the LBLA
Ruth 3 in the LNT
Ruth 3 in the LSV
Ruth 3 in the MAAL
Ruth 3 in the MBV
Ruth 3 in the MBV2
Ruth 3 in the MHNT
Ruth 3 in the MKNFD
Ruth 3 in the MNG
Ruth 3 in the MNT
Ruth 3 in the MNT2
Ruth 3 in the MRS1T
Ruth 3 in the NAA
Ruth 3 in the NASB
Ruth 3 in the NBLA
Ruth 3 in the NBS
Ruth 3 in the NBVTP
Ruth 3 in the NET2
Ruth 3 in the NIV11
Ruth 3 in the NNT
Ruth 3 in the NNT2
Ruth 3 in the NNT3
Ruth 3 in the PDDPT
Ruth 3 in the PFNT
Ruth 3 in the RMNT
Ruth 3 in the SBIAS
Ruth 3 in the SBIBS
Ruth 3 in the SBIBS2
Ruth 3 in the SBICS
Ruth 3 in the SBIDS
Ruth 3 in the SBIGS
Ruth 3 in the SBIHS
Ruth 3 in the SBIIS
Ruth 3 in the SBIIS2
Ruth 3 in the SBIIS3
Ruth 3 in the SBIKS
Ruth 3 in the SBIKS2
Ruth 3 in the SBIMS
Ruth 3 in the SBIOS
Ruth 3 in the SBIPS
Ruth 3 in the SBISS
Ruth 3 in the SBITS
Ruth 3 in the SBITS2
Ruth 3 in the SBITS3
Ruth 3 in the SBITS4
Ruth 3 in the SBIUS
Ruth 3 in the SBIVS
Ruth 3 in the SBT
Ruth 3 in the SBT1E
Ruth 3 in the SCHL
Ruth 3 in the SNT
Ruth 3 in the SUSU
Ruth 3 in the SUSU2
Ruth 3 in the SYNO
Ruth 3 in the TBIAOTANT
Ruth 3 in the TBT1E
Ruth 3 in the TBT1E2
Ruth 3 in the TFTIP
Ruth 3 in the TFTU
Ruth 3 in the TGNTATF3T
Ruth 3 in the THAI
Ruth 3 in the TNFD
Ruth 3 in the TNT
Ruth 3 in the TNTIK
Ruth 3 in the TNTIL
Ruth 3 in the TNTIN
Ruth 3 in the TNTIP
Ruth 3 in the TNTIZ
Ruth 3 in the TOMA
Ruth 3 in the TTENT
Ruth 3 in the UBG
Ruth 3 in the UGV
Ruth 3 in the UGV2
Ruth 3 in the UGV3
Ruth 3 in the VBL
Ruth 3 in the VDCC
Ruth 3 in the YALU
Ruth 3 in the YAPE
Ruth 3 in the YBVTP
Ruth 3 in the ZBP