1 Chronicles 16 (BOKCV)

1 Wakaleta Sanduku la Mungu na kuliweka ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, na wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. 2 Baada ya Daudi kumaliza kutoa hizo sadaka za kuteketezwa na hizo sadaka za amani, akawabariki watu katika jina la BWANA. 3 Kisha akamgawia kila Mwisraeli mwanaume na mwanamke mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu. 4 Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la BWANA kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu BWANA, Mungu wa Israeli: 5 Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi, 6 nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio wangepiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu. 7 Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwa BWANA: 8 Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake;wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. 9 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa;waambieni matendo yake yote ya ajabu. 10 Lishangilieni jina lake takatifu;mioyo ya wale wamtafutao BWANA na ifurahi. 11 Mtafuteni BWANA na nguvu zake;utafuteni uso wake siku zote. 12 Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,miujiza yake na hukumu alizozitamka, 13 enyi wazao wa Israeli mtumishi wake,enyi wana wa Yakobo, wateule wake. 14 Yeye ndiye BWANA Mungu wetu;hukumu zake zimo duniani pote. 15 Hulikumbuka agano lake milele,neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu, 16 agano alilolifanya na Abrahamu,kiapo alichomwapia Isaki. 17 Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,kwa Israeli liwe agano la milele: 18 “Nitakupa wewe nchi ya Kanaanikuwa sehemu utakayoirithi.” 19 Walipokuwa wachache kwa idadi,wachache sana na wageni ndani yake, 20 walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,kutoka ufalme mmoja hadi mwingine. 21 Hakuruhusu mtu yeyote awaonee;kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema: 22 “Msiwaguse niliowatia mafuta;msiwadhuru manabii wangu.” 23 Mwimbieni BWANA dunia yote;tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. 24 Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. 25 Kwa kuwa BWANA ni mkuu,mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote;yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. 26 Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,lakini BWANA aliziumba mbingu. 27 Fahari na enzi viko mbele yake;nguvu na utukufu vimo patakatifu pake. 28 Mpeni BWANA, enyi jamaa za mataifa,mpeni BWANA utukufu na nguvu, 29 mpeni BWANA utukufuunaostahili jina lake.Leteni sadaka na mje katika nyua zake;mwabuduni BWANA katika uzuri wa utakatifu wake. 30 Dunia yote na itetemeke mbele zake!Ulimwengu ameuweka imara; hauwezi kusogezwa. 31 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;semeni katikati ya mataifa, “BWANA anatawala!” 32 Bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo ndani yake. 33 Kisha miti ya msituni itaimba,itaimba kwa furaha mbele za BWANA,kwa maana anakuja kuihukumu dunia. 34 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;upendo wake wadumu milele. 35 Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe.Tukusanye tena na utukomboe kutoka kwa mataifa,ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu,na kushangilia katika sifa zako.” 36 Atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli,tangu milele na hata milele.Nao watu wote wakasema, “Amen,” na “Msifuni BWANA.” 37 Daudi akamwacha Asafu na wenzake mbele ya Sanduku la Agano la BWANA ili wahudumu humo mara kwa mara, kulingana na mahitaji ya kila siku. 38 Pia akamwacha Obed-Edomu pamoja na wenzake sitini na wanane wahudumu pamoja nao. Obed-Edomu mwana wa Yeduthuni na pia Hosa walikuwa mabawabu wa lango. 39 Daudi akamwacha kuhani Sadoki pamoja na makuhani wenzake mbele ya hema ya ibada ya BWANA katika mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni 40 ili kutoa sadaka za kuteketezwa kwa BWANA kwenye madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mara kwa mara, asubuhi na jioni, sawasawa na kila kitu kilichoandikwa katika sheria ya BWANA ambayo alikuwa amempa Israeli. 41 Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpa BWANA shukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.” 42 Hemani na Yeduthuni walikuwa na wajibu wa kupiga tarumbeta, matoazi na kutumia vyombo vingine kwa ajili ya nyimbo za sifa kwa Mungu. Wana wa Yeduthuni waliwekwa langoni. 43 Kisha watu wote wakaondoka, kila mmoja akarudi nyumbani kwake, naye Daudi akarudi nyumbani kuibariki jamaa yake.

In Other Versions

1 Chronicles 16 in the ANGEFD

1 Chronicles 16 in the ANTPNG2D

1 Chronicles 16 in the AS21

1 Chronicles 16 in the BAGH

1 Chronicles 16 in the BBPNG

1 Chronicles 16 in the BBT1E

1 Chronicles 16 in the BDS

1 Chronicles 16 in the BEV

1 Chronicles 16 in the BHAD

1 Chronicles 16 in the BIB

1 Chronicles 16 in the BLPT

1 Chronicles 16 in the BNT

1 Chronicles 16 in the BNTABOOT

1 Chronicles 16 in the BNTLV

1 Chronicles 16 in the BOATCB

1 Chronicles 16 in the BOATCB2

1 Chronicles 16 in the BOBCV

1 Chronicles 16 in the BOCNT

1 Chronicles 16 in the BOECS

1 Chronicles 16 in the BOGWICC

1 Chronicles 16 in the BOHCB

1 Chronicles 16 in the BOHCV

1 Chronicles 16 in the BOHLNT

1 Chronicles 16 in the BOHNTLTAL

1 Chronicles 16 in the BOICB

1 Chronicles 16 in the BOILNTAP

1 Chronicles 16 in the BOITCV

1 Chronicles 16 in the BOKCV2

1 Chronicles 16 in the BOKHWOG

1 Chronicles 16 in the BOKSSV

1 Chronicles 16 in the BOLCB

1 Chronicles 16 in the BOLCB2

1 Chronicles 16 in the BOMCV

1 Chronicles 16 in the BONAV

1 Chronicles 16 in the BONCB

1 Chronicles 16 in the BONLT

1 Chronicles 16 in the BONUT2

1 Chronicles 16 in the BOPLNT

1 Chronicles 16 in the BOSCB

1 Chronicles 16 in the BOSNC

1 Chronicles 16 in the BOTLNT

1 Chronicles 16 in the BOVCB

1 Chronicles 16 in the BOYCB

1 Chronicles 16 in the BPBB

1 Chronicles 16 in the BPH

1 Chronicles 16 in the BSB

1 Chronicles 16 in the CCB

1 Chronicles 16 in the CUV

1 Chronicles 16 in the CUVS

1 Chronicles 16 in the DBT

1 Chronicles 16 in the DGDNT

1 Chronicles 16 in the DHNT

1 Chronicles 16 in the DNT

1 Chronicles 16 in the ELBE

1 Chronicles 16 in the EMTV

1 Chronicles 16 in the ESV

1 Chronicles 16 in the FBV

1 Chronicles 16 in the FEB

1 Chronicles 16 in the GGMNT

1 Chronicles 16 in the GNT

1 Chronicles 16 in the HARY

1 Chronicles 16 in the HNT

1 Chronicles 16 in the IRVA

1 Chronicles 16 in the IRVB

1 Chronicles 16 in the IRVG

1 Chronicles 16 in the IRVH

1 Chronicles 16 in the IRVK

1 Chronicles 16 in the IRVM

1 Chronicles 16 in the IRVM2

1 Chronicles 16 in the IRVO

1 Chronicles 16 in the IRVP

1 Chronicles 16 in the IRVT

1 Chronicles 16 in the IRVT2

1 Chronicles 16 in the IRVU

1 Chronicles 16 in the ISVN

1 Chronicles 16 in the JSNT

1 Chronicles 16 in the KAPI

1 Chronicles 16 in the KBT1ETNIK

1 Chronicles 16 in the KBV

1 Chronicles 16 in the KJV

1 Chronicles 16 in the KNFD

1 Chronicles 16 in the LBA

1 Chronicles 16 in the LBLA

1 Chronicles 16 in the LNT

1 Chronicles 16 in the LSV

1 Chronicles 16 in the MAAL

1 Chronicles 16 in the MBV

1 Chronicles 16 in the MBV2

1 Chronicles 16 in the MHNT

1 Chronicles 16 in the MKNFD

1 Chronicles 16 in the MNG

1 Chronicles 16 in the MNT

1 Chronicles 16 in the MNT2

1 Chronicles 16 in the MRS1T

1 Chronicles 16 in the NAA

1 Chronicles 16 in the NASB

1 Chronicles 16 in the NBLA

1 Chronicles 16 in the NBS

1 Chronicles 16 in the NBVTP

1 Chronicles 16 in the NET2

1 Chronicles 16 in the NIV11

1 Chronicles 16 in the NNT

1 Chronicles 16 in the NNT2

1 Chronicles 16 in the NNT3

1 Chronicles 16 in the PDDPT

1 Chronicles 16 in the PFNT

1 Chronicles 16 in the RMNT

1 Chronicles 16 in the SBIAS

1 Chronicles 16 in the SBIBS

1 Chronicles 16 in the SBIBS2

1 Chronicles 16 in the SBICS

1 Chronicles 16 in the SBIDS

1 Chronicles 16 in the SBIGS

1 Chronicles 16 in the SBIHS

1 Chronicles 16 in the SBIIS

1 Chronicles 16 in the SBIIS2

1 Chronicles 16 in the SBIIS3

1 Chronicles 16 in the SBIKS

1 Chronicles 16 in the SBIKS2

1 Chronicles 16 in the SBIMS

1 Chronicles 16 in the SBIOS

1 Chronicles 16 in the SBIPS

1 Chronicles 16 in the SBISS

1 Chronicles 16 in the SBITS

1 Chronicles 16 in the SBITS2

1 Chronicles 16 in the SBITS3

1 Chronicles 16 in the SBITS4

1 Chronicles 16 in the SBIUS

1 Chronicles 16 in the SBIVS

1 Chronicles 16 in the SBT

1 Chronicles 16 in the SBT1E

1 Chronicles 16 in the SCHL

1 Chronicles 16 in the SNT

1 Chronicles 16 in the SUSU

1 Chronicles 16 in the SUSU2

1 Chronicles 16 in the SYNO

1 Chronicles 16 in the TBIAOTANT

1 Chronicles 16 in the TBT1E

1 Chronicles 16 in the TBT1E2

1 Chronicles 16 in the TFTIP

1 Chronicles 16 in the TFTU

1 Chronicles 16 in the TGNTATF3T

1 Chronicles 16 in the THAI

1 Chronicles 16 in the TNFD

1 Chronicles 16 in the TNT

1 Chronicles 16 in the TNTIK

1 Chronicles 16 in the TNTIL

1 Chronicles 16 in the TNTIN

1 Chronicles 16 in the TNTIP

1 Chronicles 16 in the TNTIZ

1 Chronicles 16 in the TOMA

1 Chronicles 16 in the TTENT

1 Chronicles 16 in the UBG

1 Chronicles 16 in the UGV

1 Chronicles 16 in the UGV2

1 Chronicles 16 in the UGV3

1 Chronicles 16 in the VBL

1 Chronicles 16 in the VDCC

1 Chronicles 16 in the YALU

1 Chronicles 16 in the YAPE

1 Chronicles 16 in the YBVTP

1 Chronicles 16 in the ZBP