1 Samuel 12 (BOKCV)
1 Samweli akawaambia Israeli wote, “Nimesikiliza kila kitu mlichoniambia nami nimewawekea mfalme juu yenu. 2 Sasa mnaye mfalme kama kiongozi wenu. Lakini kwa habari yangu mimi ni mzee na nina mvi, nao wanangu wapo hapa pamoja nanyi. Nimekuwa kiongozi wenu tangu ujana wangu mpaka siku hii ya leo. 3 Mimi ninasimama hapa. Shuhudieni juu yangu mbele za BWANA na mpakwa mafuta wake. Nimechukua maksai wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimepata kumdanganya? Ni nani nimepata kumwonea? Ni kutoka kwenye mkono wa nani nimepokea rushwa ili kunifanya nifumbe macho yangu? Kama nimefanya chochote katika hivi, mimi nitawarudishia.” 4 Wakajibu, “Hujatudanganya wala kutuonea. Hujapokea chochote kutoka kwenye mkono wa mtu awaye yote.” 5 Samweli akawaambia, “BWANA ni shahidi juu yenu, pia mpakwa mafuta wake ni shahidi siku hii ya leo, kwamba hamkukuta chochote mkononi mwangu.”Wakasema, “Yeye ni shahidi.” 6 Kisha Samweli akawaambia watu, “BWANA ndiye alimchagua Mose na Aroni, na kuwaleta baba zenu akiwapandisha kutoka Misri. 7 Sasa basi, simameni hapa, kwa sababu nitakabiliana nanyi kwa ushahidi mbele za BWANA wa matendo yote ya haki yaliyofanywa na BWANA kwenu na kwa baba zenu. 8 “Baada ya Yakobo kuingia Misri, walimlilia BWANA kwa ajili ya msaada, naye BWANA akawatuma Mose na Aroni, ambao waliwatoa baba zenu kutoka Misri na kuwakalisha mahali hapa. 9 “Lakini wakamsahau BWANA Mungu wao, hivyo Mungu akawauza katika mkono wa Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori na katika mikono ya Wafilisti na mfalme wa Moabu, ambaye alipigana dhidi yao. 10 Wakamlilia BWANA na kusema, ‘Tumetenda dhambi; tumemwacha BWANA na kutumikia Mabaali na Maashtorethi. Lakini sasa tuokoe kutoka mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia.’ 11 Ndipo BWANA akawatuma Yerub-Baali, Baraka, Yefta na Samweli, naye akawaokoa kutoka mikononi mwa adui zenu kila upande, ili ninyi mpate kukaa salama. 12 “Lakini mlipomwona yule Nahashi mfalme wa Waamoni anakuja dhidi yenu, mliniambia, ‘Hapana, tunataka mfalme atutawale,’ hata ingawa BWANA Mungu wenu alikuwa mfalme wenu. 13 Sasa huyu hapa ndiye mfalme mliyemchagua, yule mliyeomba; tazameni, BWANA amemweka mfalme juu yenu. 14 Kama mkimcha BWANA na kumtumikia na kumtii nanyi msipoasi dhidi ya amri zake, ninyi pamoja na mfalme anayetawala juu yenu mkimfuata BWANA, Mungu wenu, mambo yatakuwa mema kwenu! 15 Lakini kama hamkumtii BWANA, nanyi kama mkiasi dhidi ya amri zake, mkono wake utakuwa dhidi yenu, kama ulivyokuwa dhidi ya baba zenu. 16 “Sasa basi, simameni kimya mkaone jambo hili kubwa ambalo BWANA anakwenda kulifanya mbele ya macho yenu! 17 Je, sasa si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA ili alete ngurumo na mvua. Nanyi mtatambua jambo hili lilivyo baya mlilolifanya mbele za macho ya BWANA mlipoomba mfalme.” 18 Kisha Samweli akamwomba BWANA, na siku ile ile BWANA akatuma ngurumo na mvua. Hivyo watu wote wakamwogopa sana BWANA na Samweli. 19 Watu wote wakamwambia Samweli, “Mwombe BWANA Mungu wako kwa ajili ya watumishi wako, ili tusije tukafa, kwa kuwa tumeongeza uovu juu ya dhambi zetu nyingine kwa kuomba mfalme.” 20 Samweli akajibu, “Msiogope, mmefanya uovu huu wote; hata hivyo msimwache BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa moyo wenu wote. 21 Msigeukie sanamu zisizofaa. Haziwezi kuwatendea jema, wala haziwezi kuwaokoa kwa sababu hazina maana. 22 Kwa ajili ya jina lake kuu BWANA hatawakataa watu wake, kwa sababu ilimpendeza BWANA kuwafanya kuwa wake mwenyewe. 23 Kwa habari yangu, iwe mbali nami kutenda dhambi dhidi ya BWANA kwa kushindwa kuwaombea. Mimi nitawafundisha njia iliyo njema na ya kunyooka. 24 Lakini hakikisheni mnamcha BWANA na kumtumikia kwa uaminifu kwa moyo wenu wote; tafakarini mambo makubwa aliyoyatenda kwa ajili yenu. 25 Hata hivyo mkiendelea kufanya uovu, ninyi na mfalme wenu mtafutiliwa mbali!”
In Other Versions
1 Samuel 12 in the ANGEFD
1 Samuel 12 in the ANTPNG2D
1 Samuel 12 in the AS21
1 Samuel 12 in the BAGH
1 Samuel 12 in the BBPNG
1 Samuel 12 in the BBT1E
1 Samuel 12 in the BDS
1 Samuel 12 in the BEV
1 Samuel 12 in the BHAD
1 Samuel 12 in the BIB
1 Samuel 12 in the BLPT
1 Samuel 12 in the BNT
1 Samuel 12 in the BNTABOOT
1 Samuel 12 in the BNTLV
1 Samuel 12 in the BOATCB
1 Samuel 12 in the BOATCB2
1 Samuel 12 in the BOBCV
1 Samuel 12 in the BOCNT
1 Samuel 12 in the BOECS
1 Samuel 12 in the BOGWICC
1 Samuel 12 in the BOHCB
1 Samuel 12 in the BOHCV
1 Samuel 12 in the BOHLNT
1 Samuel 12 in the BOHNTLTAL
1 Samuel 12 in the BOICB
1 Samuel 12 in the BOILNTAP
1 Samuel 12 in the BOITCV
1 Samuel 12 in the BOKCV2
1 Samuel 12 in the BOKHWOG
1 Samuel 12 in the BOKSSV
1 Samuel 12 in the BOLCB
1 Samuel 12 in the BOLCB2
1 Samuel 12 in the BOMCV
1 Samuel 12 in the BONAV
1 Samuel 12 in the BONCB
1 Samuel 12 in the BONLT
1 Samuel 12 in the BONUT2
1 Samuel 12 in the BOPLNT
1 Samuel 12 in the BOSCB
1 Samuel 12 in the BOSNC
1 Samuel 12 in the BOTLNT
1 Samuel 12 in the BOVCB
1 Samuel 12 in the BOYCB
1 Samuel 12 in the BPBB
1 Samuel 12 in the BPH
1 Samuel 12 in the BSB
1 Samuel 12 in the CCB
1 Samuel 12 in the CUV
1 Samuel 12 in the CUVS
1 Samuel 12 in the DBT
1 Samuel 12 in the DGDNT
1 Samuel 12 in the DHNT
1 Samuel 12 in the DNT
1 Samuel 12 in the ELBE
1 Samuel 12 in the EMTV
1 Samuel 12 in the ESV
1 Samuel 12 in the FBV
1 Samuel 12 in the FEB
1 Samuel 12 in the GGMNT
1 Samuel 12 in the GNT
1 Samuel 12 in the HARY
1 Samuel 12 in the HNT
1 Samuel 12 in the IRVA
1 Samuel 12 in the IRVB
1 Samuel 12 in the IRVG
1 Samuel 12 in the IRVH
1 Samuel 12 in the IRVK
1 Samuel 12 in the IRVM
1 Samuel 12 in the IRVM2
1 Samuel 12 in the IRVO
1 Samuel 12 in the IRVP
1 Samuel 12 in the IRVT
1 Samuel 12 in the IRVT2
1 Samuel 12 in the IRVU
1 Samuel 12 in the ISVN
1 Samuel 12 in the JSNT
1 Samuel 12 in the KAPI
1 Samuel 12 in the KBT1ETNIK
1 Samuel 12 in the KBV
1 Samuel 12 in the KJV
1 Samuel 12 in the KNFD
1 Samuel 12 in the LBA
1 Samuel 12 in the LBLA
1 Samuel 12 in the LNT
1 Samuel 12 in the LSV
1 Samuel 12 in the MAAL
1 Samuel 12 in the MBV
1 Samuel 12 in the MBV2
1 Samuel 12 in the MHNT
1 Samuel 12 in the MKNFD
1 Samuel 12 in the MNG
1 Samuel 12 in the MNT
1 Samuel 12 in the MNT2
1 Samuel 12 in the MRS1T
1 Samuel 12 in the NAA
1 Samuel 12 in the NASB
1 Samuel 12 in the NBLA
1 Samuel 12 in the NBS
1 Samuel 12 in the NBVTP
1 Samuel 12 in the NET2
1 Samuel 12 in the NIV11
1 Samuel 12 in the NNT
1 Samuel 12 in the NNT2
1 Samuel 12 in the NNT3
1 Samuel 12 in the PDDPT
1 Samuel 12 in the PFNT
1 Samuel 12 in the RMNT
1 Samuel 12 in the SBIAS
1 Samuel 12 in the SBIBS
1 Samuel 12 in the SBIBS2
1 Samuel 12 in the SBICS
1 Samuel 12 in the SBIDS
1 Samuel 12 in the SBIGS
1 Samuel 12 in the SBIHS
1 Samuel 12 in the SBIIS
1 Samuel 12 in the SBIIS2
1 Samuel 12 in the SBIIS3
1 Samuel 12 in the SBIKS
1 Samuel 12 in the SBIKS2
1 Samuel 12 in the SBIMS
1 Samuel 12 in the SBIOS
1 Samuel 12 in the SBIPS
1 Samuel 12 in the SBISS
1 Samuel 12 in the SBITS
1 Samuel 12 in the SBITS2
1 Samuel 12 in the SBITS3
1 Samuel 12 in the SBITS4
1 Samuel 12 in the SBIUS
1 Samuel 12 in the SBIVS
1 Samuel 12 in the SBT
1 Samuel 12 in the SBT1E
1 Samuel 12 in the SCHL
1 Samuel 12 in the SNT
1 Samuel 12 in the SUSU
1 Samuel 12 in the SUSU2
1 Samuel 12 in the SYNO
1 Samuel 12 in the TBIAOTANT
1 Samuel 12 in the TBT1E
1 Samuel 12 in the TBT1E2
1 Samuel 12 in the TFTIP
1 Samuel 12 in the TFTU
1 Samuel 12 in the TGNTATF3T
1 Samuel 12 in the THAI
1 Samuel 12 in the TNFD
1 Samuel 12 in the TNT
1 Samuel 12 in the TNTIK
1 Samuel 12 in the TNTIL
1 Samuel 12 in the TNTIN
1 Samuel 12 in the TNTIP
1 Samuel 12 in the TNTIZ
1 Samuel 12 in the TOMA
1 Samuel 12 in the TTENT
1 Samuel 12 in the UBG
1 Samuel 12 in the UGV
1 Samuel 12 in the UGV2
1 Samuel 12 in the UGV3
1 Samuel 12 in the VBL
1 Samuel 12 in the VDCC
1 Samuel 12 in the YALU
1 Samuel 12 in the YAPE
1 Samuel 12 in the YBVTP
1 Samuel 12 in the ZBP