Deuteronomy 29 (BOKCV)
1 Haya ndiyo maneno ya Agano BWANA aliyomwagiza Mose kufanya na Waisraeli huko Moabu, kuwa nyongeza ya Agano alilofanya nao huko Horebu. 2 Mose akawaita Waisraeli wote akawaambia: Macho yenu yameona yale yote BWANA aliyofanya kwa Mfalme Farao huko Misri, kwa maafisa wake wote na kwa nchi yake yote. 3 Kwa macho yenu wenyewe mliona yale majaribu makubwa, ishara zile za miujiza na maajabu makubwa. 4 Lakini mpaka leo BWANA hajawapa akili ya kuelewa au macho yanayoona au masikio yanayosikia. 5 Kwa muda wa miaka arobaini niliyowaongoza jangwani, nguo zenu hazikuchakaa, wala viatu miguuni mwenu. 6 Hamkula mkate na hamkunywa divai wala kileo chochote. Nilifanya hivi ili mpate kujua kuwa mimi ndimi BWANA Mungu wenu. 7 Wakati mlipofika mahali hapa, Sihoni mfalme wa Heshboni na Ogu mfalme wa Bashani walikuja kupigana dhidi yetu, lakini tuliwashinda. 8 Tuliichukua nchi yao na kuwapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kama urithi wao. 9 Fuateni kwa bidii masharti ya Agano hili, ili kwamba mweze kustawi katika kila kitu mnachofanya. 10 Ninyi nyote leo mnasimama mbele za BWANA Mungu wenu; mkiwa viongozi na wakuu wenu, wazee na maafisa wenu, na wanaume wengine wote wa Israeli, 11 pamoja na watoto wenu, wake zenu na pia wageni waishio katika kambi zenu wanaowapasulia kuni na kuwachotea maji. 12 Mnasimama hapa ili kufanya Agano na BWANA Mungu wenu, Agano ambalo Mungu analifanya nanyi siku hii ya leo na kulitia muhuri kwa kiapo, 13 kuwathibitisha ninyi siku hii ya leo kama taifa lake, ili aweze kuwa Mungu wenu kama alivyowaahidi na kama alivyowaapia baba zenu Abrahamu, Isaki na Yakobo. 14 Ninafanya Agano hili pamoja na kiapo chake, sio na ninyi tu 15 mnaosimama hapa na sisi leo mbele za BWANA Mungu wetu, bali pia pamoja na wale ambao hawapo hapa leo. 16 Ninyi wenyewe mnajua jinsi tulivyoishi nchini Misri na jinsi tulivyopita katikati ya nchi mpaka tukafika hapa. 17 Mliona miongoni mwao vinyago vyao vya kuchukiza na sanamu za miti na mawe, za fedha na dhahabu. 18 Hakikisheni kwamba hakuna mwanaume au mwanamke, ukoo au kabila miongoni mwenu leo ambalo moyo wake utamwacha BWANA Mungu wetu, kwenda kuabudu miungu ya mataifa hayo. Hakikisheni hakuna mzizi miongoni mwenu unaotoa sumu chungu ya namna hii. 19 Wakati mtu wa namna hii asikiapo maneno ya kiapo hiki, hujibariki mwenyewe na kisha hufikiri, “Nitakuwa salama, hata kama nikiendelea kuifuata njia yangu mwenyewe.” Hili litaleta maafa juu ya nchi iliyonyeshewa sawasawa na nchi kame. 20 BWANA kamwe hatakuwa radhi kumsamehe, ghadhabu na wivu wa Mungu vitawaka dhidi ya mtu huyo. Laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamwangukia na BWANA atafuta jina lake chini ya mbingu. 21 BWANA atamtwaa peke yake kutoka makabila ya Israeli kwa maangamizo, kulingana na laana zote za Agano zilizoandikwa kwenye Kitabu hiki cha Sheria. 22 Watoto wako watakaofuata baada yako katika vizazi vya baadaye na wageni ambao watakuja kutoka nchi za mbali, wataona maafa, yaliyoipata nchi na magonjwa ambayo BWANA aliyaleta juu yake. 23 Nchi yote itakuwa jaa linaloungua la chumvi na kiberiti: hakutakuwa kilichopandwa, hakutakuwa kinachochipua, wala hakutakuwa mimea inayoota juu yake. Itakuwa kama maangamizo ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, ambazo BWANA aliangamiza kwa hasira kali. 24 Mataifa yote yatauliza: “Kwa nini BWANA amefanya hivi juu ya nchi hii? Kwa nini hasira hii kali ikawaka?” 25 Na jibu litakuwa: “Ni kwa sababu watu hawa waliacha Agano la BWANA, Mungu wa baba zao, Agano alilofanya nao wakati alipowatoa katika nchi ya Misri. 26 Walienda zao na kuabudu miungu mingine na kuisujudia, miungu wasioijua, miungu ambayo Mungu hakuwapa. 27 Kwa hiyo hasira ya BWANA ikawaka dhidi ya nchi hii, hivyo Mungu akaleta juu yake laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki. 28 Katika hasira kali na katika ghadhabu kuu BWANA aliwangʼoa kutoka nchi yao na kuwasukumia katika nchi nyingine, kama ilivyo sasa.” 29 Mambo ya siri ni ya BWANA Mungu wetu, bali yaliyofunuliwa ni yetu na watoto wetu milele, ili tuweze kuyafanya maneno yote ya sheria hii.
In Other Versions
Deuteronomy 29 in the ANGEFD
Deuteronomy 29 in the ANTPNG2D
Deuteronomy 29 in the AS21
Deuteronomy 29 in the BAGH
Deuteronomy 29 in the BBPNG
Deuteronomy 29 in the BBT1E
Deuteronomy 29 in the BDS
Deuteronomy 29 in the BEV
Deuteronomy 29 in the BHAD
Deuteronomy 29 in the BIB
Deuteronomy 29 in the BLPT
Deuteronomy 29 in the BNT
Deuteronomy 29 in the BNTABOOT
Deuteronomy 29 in the BNTLV
Deuteronomy 29 in the BOATCB
Deuteronomy 29 in the BOATCB2
Deuteronomy 29 in the BOBCV
Deuteronomy 29 in the BOCNT
Deuteronomy 29 in the BOECS
Deuteronomy 29 in the BOGWICC
Deuteronomy 29 in the BOHCB
Deuteronomy 29 in the BOHCV
Deuteronomy 29 in the BOHLNT
Deuteronomy 29 in the BOHNTLTAL
Deuteronomy 29 in the BOICB
Deuteronomy 29 in the BOILNTAP
Deuteronomy 29 in the BOITCV
Deuteronomy 29 in the BOKCV2
Deuteronomy 29 in the BOKHWOG
Deuteronomy 29 in the BOKSSV
Deuteronomy 29 in the BOLCB
Deuteronomy 29 in the BOLCB2
Deuteronomy 29 in the BOMCV
Deuteronomy 29 in the BONAV
Deuteronomy 29 in the BONCB
Deuteronomy 29 in the BONLT
Deuteronomy 29 in the BONUT2
Deuteronomy 29 in the BOPLNT
Deuteronomy 29 in the BOSCB
Deuteronomy 29 in the BOSNC
Deuteronomy 29 in the BOTLNT
Deuteronomy 29 in the BOVCB
Deuteronomy 29 in the BOYCB
Deuteronomy 29 in the BPBB
Deuteronomy 29 in the BPH
Deuteronomy 29 in the BSB
Deuteronomy 29 in the CCB
Deuteronomy 29 in the CUV
Deuteronomy 29 in the CUVS
Deuteronomy 29 in the DBT
Deuteronomy 29 in the DGDNT
Deuteronomy 29 in the DHNT
Deuteronomy 29 in the DNT
Deuteronomy 29 in the ELBE
Deuteronomy 29 in the EMTV
Deuteronomy 29 in the ESV
Deuteronomy 29 in the FBV
Deuteronomy 29 in the FEB
Deuteronomy 29 in the GGMNT
Deuteronomy 29 in the GNT
Deuteronomy 29 in the HARY
Deuteronomy 29 in the HNT
Deuteronomy 29 in the IRVA
Deuteronomy 29 in the IRVB
Deuteronomy 29 in the IRVG
Deuteronomy 29 in the IRVH
Deuteronomy 29 in the IRVK
Deuteronomy 29 in the IRVM
Deuteronomy 29 in the IRVM2
Deuteronomy 29 in the IRVO
Deuteronomy 29 in the IRVP
Deuteronomy 29 in the IRVT
Deuteronomy 29 in the IRVT2
Deuteronomy 29 in the IRVU
Deuteronomy 29 in the ISVN
Deuteronomy 29 in the JSNT
Deuteronomy 29 in the KAPI
Deuteronomy 29 in the KBT1ETNIK
Deuteronomy 29 in the KBV
Deuteronomy 29 in the KJV
Deuteronomy 29 in the KNFD
Deuteronomy 29 in the LBA
Deuteronomy 29 in the LBLA
Deuteronomy 29 in the LNT
Deuteronomy 29 in the LSV
Deuteronomy 29 in the MAAL
Deuteronomy 29 in the MBV
Deuteronomy 29 in the MBV2
Deuteronomy 29 in the MHNT
Deuteronomy 29 in the MKNFD
Deuteronomy 29 in the MNG
Deuteronomy 29 in the MNT
Deuteronomy 29 in the MNT2
Deuteronomy 29 in the MRS1T
Deuteronomy 29 in the NAA
Deuteronomy 29 in the NASB
Deuteronomy 29 in the NBLA
Deuteronomy 29 in the NBS
Deuteronomy 29 in the NBVTP
Deuteronomy 29 in the NET2
Deuteronomy 29 in the NIV11
Deuteronomy 29 in the NNT
Deuteronomy 29 in the NNT2
Deuteronomy 29 in the NNT3
Deuteronomy 29 in the PDDPT
Deuteronomy 29 in the PFNT
Deuteronomy 29 in the RMNT
Deuteronomy 29 in the SBIAS
Deuteronomy 29 in the SBIBS
Deuteronomy 29 in the SBIBS2
Deuteronomy 29 in the SBICS
Deuteronomy 29 in the SBIDS
Deuteronomy 29 in the SBIGS
Deuteronomy 29 in the SBIHS
Deuteronomy 29 in the SBIIS
Deuteronomy 29 in the SBIIS2
Deuteronomy 29 in the SBIIS3
Deuteronomy 29 in the SBIKS
Deuteronomy 29 in the SBIKS2
Deuteronomy 29 in the SBIMS
Deuteronomy 29 in the SBIOS
Deuteronomy 29 in the SBIPS
Deuteronomy 29 in the SBISS
Deuteronomy 29 in the SBITS
Deuteronomy 29 in the SBITS2
Deuteronomy 29 in the SBITS3
Deuteronomy 29 in the SBITS4
Deuteronomy 29 in the SBIUS
Deuteronomy 29 in the SBIVS
Deuteronomy 29 in the SBT
Deuteronomy 29 in the SBT1E
Deuteronomy 29 in the SCHL
Deuteronomy 29 in the SNT
Deuteronomy 29 in the SUSU
Deuteronomy 29 in the SUSU2
Deuteronomy 29 in the SYNO
Deuteronomy 29 in the TBIAOTANT
Deuteronomy 29 in the TBT1E
Deuteronomy 29 in the TBT1E2
Deuteronomy 29 in the TFTIP
Deuteronomy 29 in the TFTU
Deuteronomy 29 in the TGNTATF3T
Deuteronomy 29 in the THAI
Deuteronomy 29 in the TNFD
Deuteronomy 29 in the TNT
Deuteronomy 29 in the TNTIK
Deuteronomy 29 in the TNTIL
Deuteronomy 29 in the TNTIN
Deuteronomy 29 in the TNTIP
Deuteronomy 29 in the TNTIZ
Deuteronomy 29 in the TOMA
Deuteronomy 29 in the TTENT
Deuteronomy 29 in the UBG
Deuteronomy 29 in the UGV
Deuteronomy 29 in the UGV2
Deuteronomy 29 in the UGV3
Deuteronomy 29 in the VBL
Deuteronomy 29 in the VDCC
Deuteronomy 29 in the YALU
Deuteronomy 29 in the YAPE
Deuteronomy 29 in the YBVTP
Deuteronomy 29 in the ZBP