Deuteronomy 32 (BOKCV)

1 Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitasema;sikia, ee nchi, maneno ya kinywa changu. 2 Mafundisho yangu na yanyeshe kama mvua,na maneno yangu na yashuke kama umande,kama manyunyu juu ya majani mabichi,kama mvua tele juu ya mimea myororo. 3 Nitalitangaza jina la BWANA.Naam, sifuni ukuu wa Mungu wetu! 4 Yeye ni Mwamba, kazi zake ni kamilifu,njia zake zote ni haki.Mungu mwaminifu ambaye hakosei,yeye ni mnyofu na mwenye haki. 5 Wamefanya mambo ya upotovu mbele zake;kwa aibu yao, wao si watoto wake tena,lakini ni kizazi kilicho kiovu na kilichopotoka. 6 Je, hii ndiyo njia ya kumlipa BWANA,enyi watu wajinga na wasio na busara?Je, yeye siye Baba yenu, Muumba wenu,aliyewafanya ninyi na kuwaumba? 7 Kumbuka siku za kale;tafakari vizazi vya zamani vilivyopita.Uliza baba yako, naye atakuambia,wazee wako, nao watakueleza. 8 Aliye Juu Sana alipowapa mataifa urithi wao,alipogawanya wanadamu wote,aliweka mipaka kwa ajili ya mataifasawasawa na hesabu ya wana wa Israeli. 9 Kwa kuwa fungu la BWANA ni watu wake,Yakobo kura yake ya urithi. 10 Katika nchi ya jangwa alimkuta,katika nyika tupu ivumayo upepo.Alimhifadhi na kumtunza;akamlinda kama mboni ya jicho lake, 11 kama tai avurugaye kiota chake,na kurukaruka juu ya makinda yake,ambaye hutanda mabawa yake kuwadaka,na huwachukua kwenye mabawa yake. 12 BWANA peke yake alimwongoza;hakuwepo mungu mgeni pamoja naye. 13 Akamfanya apande sehemu zilizoinuka za nchi,akamlisha kwa mavuno ya mashamba.Akamlea kwa asali toka mwambani,na kwa mafuta kutoka mwamba mgumu, 14 kwa jibini na maziwa kutoka makundi ya ngʼombena kutoka makundi ya mbuzi,kwa mafuta ya wana-kondoo na mbuzi,kwa kondoo dume wazuri wa Bashani,na kwa ngano nzuri.Ukanywa damu ya zabibu inayotoa povu. 15 Yeshuruni alinenepa na kupiga teke;alikuwa na chakula tele,akawa mzito na akapendeza sana.Akamwacha Mungu aliyemuumba,na kumkataa Mwamba Mwokozi wake. 16 Wakamfanya Mungu kuwa na wivu kwa miungu yao migeni,na kumkasirisha kwa sanamu zaoza machukizo. 17 Wakatoa dhabihu kwa pepo, ambao si Mungu:miungu wasiyoijua,miungu iliyojitokeza siku za karibuni,miungu ambayo baba zenu hawakuiogopa. 18 Mkamwacha Mwamba, aliyewazaa ninyi;mkamsahau Mungu aliyewazaa. 19 BWANA akaona hili, akawakataa,kwa sababu alikasirishwana wanawe na binti zake. 20 Akasema, “Nitawaficha uso wangu,nami nione mwisho wao utakuwa nini,kwa kuwa wao ni kizazi kilichopotoka,watoto ambao si waaminifu. 21 Wamenifanya niwe na wivukwa kile ambacho si mungu,na kunikasirisha kwa sanamu zaozisizokuwa na thamani.Nitawafanya wawaonee wivu wale ambao si taifa.Nitawafanya wakasirishwena taifa lile lisilo na ufahamu. 22 Kwa maana moto umewashwa kwa hasira yangu,ule uwakao hadi kwenye vina vya mauti.Utateketeza dunia pamoja na mazao yake,na kuwasha moto katika misingi ya milima. 23 “Nitalundika majanga juu yaona kutumia mishale yangu dhidi yao. 24 Nitatuma njaa kali dhidi yao maradhi mabaya,yateketezayo na tauni ya kufisha;nitawapelekea meno makali ya wanyama mwitu,na sumu ya nyoka wale watambaao mavumbini. 25 Barabarani upanga utawakosesha watoto;nyumbani mwao hofu itatawala.Vijana wao wa kiume na wa kike wataangamia,pia watoto wachanga na wazee wenye mvi. 26 Nilisema ningewatawanyana kufuta kumbukumbu laokatika mwanadamu. 27 Lakini nilihofia dhihaka za adui,adui asije akashindwa kuelewa,na kusema, ‘Mikono yetu imeshinda; BWANA hakufanya yote haya.’ ” 28 Wao ni taifa lisilo na akili,hakuna busara ndani yao. 29 Laiti wangekuwa na hekima wangefahamu hili,na kutambua mwisho wao utakuwa aje! 30 Mtu mmoja angewezaje kufukuza elfu moja,au wawili kufukuza elfu kumi,kama si kwamba Mwamba wao amewauza,kama si kwamba BWANA amewaacha? 31 Kwa kuwa mwamba wao si kama Mwamba wetu,sawasawa na vile adui zetu wanavyokiri. 32 Mzabibu wao unatoka kwenye mzabibu wa Sodoma,na kutoka kwenye mashamba ya Gomora.Zabibu zake zimejaa sumu,na vishada vyake vimejaa uchungu. 33 Mvinyo wao ni sumu ya nyoka,sumu yenye kufisha ya swila. 34 “Je, hili sikuliweka akibana kulifungia kwenye vyumba vyangu vya hazina? 35 Ni juu yangu kulipiza kisasi; nitalipiza.Wakati utakapowadia, mguu wao utateleza;siku yao ya maafa ni karibu,na maangamizo yao yanawajia haraka.” 36 BWANA atawahukumu watu wake,na kuwahurumia watumishi wakeatakapoona nguvu zao zimekwishawala hakuna yeyote aliyebaki,mtumwa au aliye huru. 37 Atasema: “Sasa iko wapi miungu yao,mwamba walioukimbilia, 38 miungu wale waliokula mafuta ya dhabihu zaona kunywa mvinyo wa sadaka zao za vinywaji?Wainuke basi, wawasaidie!Wawapeni basi ulinzi! 39 “Tazama basi, Mimi mwenyewe, Mimi Ndiye!Hakuna mungu mwingine ila Mimi.Mimi ninaua na Mimi ninafufua,Mimi nimejeruhi na Mimi nitaponya,wala hakuna awezaye kuokoa kutoka mkononi mwangu. 40 Ninainua mkono wangu kuelekea mbinguni na kusema:Hakika kama niishivyo milele, 41 wakati ninapounoa upanga wangu unaometametana mkono wangu unapoushika ili kutoa hukumu,nitalipiza kisasi juu ya adui zanguna kuwalipiza wale wanaonichukia. 42 Nitailevya mishale yangu kwa damu,wakati upanga wangu ukitafuna nyama:damu ya waliochinjwa pamoja na mateka,vichwa vya viongozi wa adui.” 43 Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake,kwa kuwa atailipiza damu ya watumishi wake,atalipiza kisasi juu ya adui zakena kufanya upatanishokwa ajili ya nchi na watu wake. 44 Mose na Yoshua mwana wa Nuni wakaja, wakanena maneno yote ya wimbo watu wakiwa wanasikia. 45 Mose alipomaliza kuyasoma maneno haya yote kwa Israeli wote, 46 akawaambia, “Yawekeni moyoni maneno yote ambayo nimewatangazia kwa makini siku hii ya leo, ili kwamba mpate kuwaagiza watoto wenu wayatii kwa bidii maneno yote ya sheria hii. 47 Siyo maneno matupu tu kwenu, bali ni uzima wenu. Kwa hayo mtaishi maisha marefu katika nchi mnayovuka Yordani kuimiliki.” 48 Siku hiyo hiyo BWANA akamwambia Mose, 49 “Kwea katika mapangano ya Mlima Abarimu hadi kilima cha Nebo kilichoko Moabu, ngʼambo ya Yeriko, na uitazame Kanaani, nchi ninayowapa Waisraeli kama milki yao wenyewe. 50 Utafia kwenye mlima huo unaokwea na kukusanyika pamoja na watu wako, kama ndugu yako Aroni alivyofia juu ya Mlima Hori naye akakusanyika kwa watu wake. 51 Hii ni kwa sababu ninyi wawili mlivunja uaminifu nami mbele ya Waisraeli kwenye maji ya Meriba-Kadeshi katika Jangwa la Sini, na kwa sababu hamkuuinua utakatifu wangu miongoni mwa Waisraeli. 52 Kwa hiyo, utaiona tu nchi kwa mbali; wewe hutaingia nchi ninayowapa watu wa Israeli.”

In Other Versions

Deuteronomy 32 in the ANGEFD

Deuteronomy 32 in the ANTPNG2D

Deuteronomy 32 in the AS21

Deuteronomy 32 in the BAGH

Deuteronomy 32 in the BBPNG

Deuteronomy 32 in the BBT1E

Deuteronomy 32 in the BDS

Deuteronomy 32 in the BEV

Deuteronomy 32 in the BHAD

Deuteronomy 32 in the BIB

Deuteronomy 32 in the BLPT

Deuteronomy 32 in the BNT

Deuteronomy 32 in the BNTABOOT

Deuteronomy 32 in the BNTLV

Deuteronomy 32 in the BOATCB

Deuteronomy 32 in the BOATCB2

Deuteronomy 32 in the BOBCV

Deuteronomy 32 in the BOCNT

Deuteronomy 32 in the BOECS

Deuteronomy 32 in the BOGWICC

Deuteronomy 32 in the BOHCB

Deuteronomy 32 in the BOHCV

Deuteronomy 32 in the BOHLNT

Deuteronomy 32 in the BOHNTLTAL

Deuteronomy 32 in the BOICB

Deuteronomy 32 in the BOILNTAP

Deuteronomy 32 in the BOITCV

Deuteronomy 32 in the BOKCV2

Deuteronomy 32 in the BOKHWOG

Deuteronomy 32 in the BOKSSV

Deuteronomy 32 in the BOLCB

Deuteronomy 32 in the BOLCB2

Deuteronomy 32 in the BOMCV

Deuteronomy 32 in the BONAV

Deuteronomy 32 in the BONCB

Deuteronomy 32 in the BONLT

Deuteronomy 32 in the BONUT2

Deuteronomy 32 in the BOPLNT

Deuteronomy 32 in the BOSCB

Deuteronomy 32 in the BOSNC

Deuteronomy 32 in the BOTLNT

Deuteronomy 32 in the BOVCB

Deuteronomy 32 in the BOYCB

Deuteronomy 32 in the BPBB

Deuteronomy 32 in the BPH

Deuteronomy 32 in the BSB

Deuteronomy 32 in the CCB

Deuteronomy 32 in the CUV

Deuteronomy 32 in the CUVS

Deuteronomy 32 in the DBT

Deuteronomy 32 in the DGDNT

Deuteronomy 32 in the DHNT

Deuteronomy 32 in the DNT

Deuteronomy 32 in the ELBE

Deuteronomy 32 in the EMTV

Deuteronomy 32 in the ESV

Deuteronomy 32 in the FBV

Deuteronomy 32 in the FEB

Deuteronomy 32 in the GGMNT

Deuteronomy 32 in the GNT

Deuteronomy 32 in the HARY

Deuteronomy 32 in the HNT

Deuteronomy 32 in the IRVA

Deuteronomy 32 in the IRVB

Deuteronomy 32 in the IRVG

Deuteronomy 32 in the IRVH

Deuteronomy 32 in the IRVK

Deuteronomy 32 in the IRVM

Deuteronomy 32 in the IRVM2

Deuteronomy 32 in the IRVO

Deuteronomy 32 in the IRVP

Deuteronomy 32 in the IRVT

Deuteronomy 32 in the IRVT2

Deuteronomy 32 in the IRVU

Deuteronomy 32 in the ISVN

Deuteronomy 32 in the JSNT

Deuteronomy 32 in the KAPI

Deuteronomy 32 in the KBT1ETNIK

Deuteronomy 32 in the KBV

Deuteronomy 32 in the KJV

Deuteronomy 32 in the KNFD

Deuteronomy 32 in the LBA

Deuteronomy 32 in the LBLA

Deuteronomy 32 in the LNT

Deuteronomy 32 in the LSV

Deuteronomy 32 in the MAAL

Deuteronomy 32 in the MBV

Deuteronomy 32 in the MBV2

Deuteronomy 32 in the MHNT

Deuteronomy 32 in the MKNFD

Deuteronomy 32 in the MNG

Deuteronomy 32 in the MNT

Deuteronomy 32 in the MNT2

Deuteronomy 32 in the MRS1T

Deuteronomy 32 in the NAA

Deuteronomy 32 in the NASB

Deuteronomy 32 in the NBLA

Deuteronomy 32 in the NBS

Deuteronomy 32 in the NBVTP

Deuteronomy 32 in the NET2

Deuteronomy 32 in the NIV11

Deuteronomy 32 in the NNT

Deuteronomy 32 in the NNT2

Deuteronomy 32 in the NNT3

Deuteronomy 32 in the PDDPT

Deuteronomy 32 in the PFNT

Deuteronomy 32 in the RMNT

Deuteronomy 32 in the SBIAS

Deuteronomy 32 in the SBIBS

Deuteronomy 32 in the SBIBS2

Deuteronomy 32 in the SBICS

Deuteronomy 32 in the SBIDS

Deuteronomy 32 in the SBIGS

Deuteronomy 32 in the SBIHS

Deuteronomy 32 in the SBIIS

Deuteronomy 32 in the SBIIS2

Deuteronomy 32 in the SBIIS3

Deuteronomy 32 in the SBIKS

Deuteronomy 32 in the SBIKS2

Deuteronomy 32 in the SBIMS

Deuteronomy 32 in the SBIOS

Deuteronomy 32 in the SBIPS

Deuteronomy 32 in the SBISS

Deuteronomy 32 in the SBITS

Deuteronomy 32 in the SBITS2

Deuteronomy 32 in the SBITS3

Deuteronomy 32 in the SBITS4

Deuteronomy 32 in the SBIUS

Deuteronomy 32 in the SBIVS

Deuteronomy 32 in the SBT

Deuteronomy 32 in the SBT1E

Deuteronomy 32 in the SCHL

Deuteronomy 32 in the SNT

Deuteronomy 32 in the SUSU

Deuteronomy 32 in the SUSU2

Deuteronomy 32 in the SYNO

Deuteronomy 32 in the TBIAOTANT

Deuteronomy 32 in the TBT1E

Deuteronomy 32 in the TBT1E2

Deuteronomy 32 in the TFTIP

Deuteronomy 32 in the TFTU

Deuteronomy 32 in the TGNTATF3T

Deuteronomy 32 in the THAI

Deuteronomy 32 in the TNFD

Deuteronomy 32 in the TNT

Deuteronomy 32 in the TNTIK

Deuteronomy 32 in the TNTIL

Deuteronomy 32 in the TNTIN

Deuteronomy 32 in the TNTIP

Deuteronomy 32 in the TNTIZ

Deuteronomy 32 in the TOMA

Deuteronomy 32 in the TTENT

Deuteronomy 32 in the UBG

Deuteronomy 32 in the UGV

Deuteronomy 32 in the UGV2

Deuteronomy 32 in the UGV3

Deuteronomy 32 in the VBL

Deuteronomy 32 in the VDCC

Deuteronomy 32 in the YALU

Deuteronomy 32 in the YAPE

Deuteronomy 32 in the YBVTP

Deuteronomy 32 in the ZBP