Ezekiel 30 (BOKCV)

1 Neno la BWANA likanijia kusema: 2 “Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo:“ ‘Ombolezeni ninyi na mseme,“Ole wa siku ile!” 3 Kwa kuwa siku ile imekaribia,siku ya BWANA imekaribia,siku ya mawingu,siku ya maangamizi kwa mataifa. 4 Upanga utakuja dhidi ya Misri,nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia.Mauaji yatakapoangukia Misri,utajiri wake utachukuliwana misingi yake itabomolewa. 5 Kushi na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri. 6 “ ‘Hili ndilo BWANA asemalo:“ ‘Wale walioungana na Misri wataangukana kiburi cha nguvu zake kitashindwa.Kutoka Migdoli hadi Aswani,watauawa ndani yake kwa upanga,asema BWANA Mwenyezi. 7 “ ‘Hizo nchi zitakua ukiwamiongoni mwa nchi zilizo ukiwa,nayo miji yao itakuwa magofumiongoni mwa miji iliyo magofu. 8 Ndipo watakapojua kwamba mimi ndimi BWANA,nitakapoiwasha Misri motona wote wamsaidiao watapondwa. 9 “ ‘Siku hiyo wajumbe watatoka kwangu kwa merikebu, ili kuwatia hofu Ethiopia, wakiwa katika hali yao ya kuridhika. Maumivu makali yatawapata siku ya maangamizi ya Misri, kwa kuwa hakika itakuja. 10 “ ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo:“ ‘Nitakomesha makundi ya wajeuri ya Misrikwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli. 11 Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote,litaletwa ili kuangamiza nchi.Watafuta panga zao dhidi ya Misrina kuijaza nchi kwa waliouawa. 12 Nitakausha vijito vya Nailina nitaiuza nchi kwa watu waovu,kwa mkono wa wageni,nitaifanya nchi ukiwa na kila kitukilichomo ndani yake.Mimi BWANA nimenena haya. 13 “ ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo:“ ‘Nitaangamiza sanamuna kukomesha vinyago katika MemfisiHapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri,nami nitaeneza hofu katika nchi nzima. 14 Nitaifanya Pathrosi kuwa ukiwana kuitia moto Soani,nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi 15 Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,ngome ya Misri,nami nitakatilia mbalimakundi ya wajeuri wa Thebesi. 16 Nitaitia moto nchi ya Misri;Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu.Thebesi itachukuliwa na tufani,Memfisi itakuwa katika taabu daima. 17 Wanaume vijana wa Oni na wa Pi-Besethiwataanguka kwa upanganayo hiyo miji itatekwa. 18 Huko Tahpanhesi mchana utatiwa gizanitakapovunja kongwa la Misri;hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma.Atafunikwa na mawinguna vijiji vyake vitatekwa. 19 Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu,nao watajua kuwa Mimi ndimi BWANA.’ ” 20 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa kwanza, siku ya saba, neno la BWANA likanijia kusema: 21 “Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga. 22 Kwa hiyo hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na Farao mfalme wa Misri. Nitavunja mikono yake yote miwili, ule mkono ulio mzima pia na ule uliovunjika na kuufanya upanga uanguke toka mkononi mwake. 23 Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi zote. 24 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli na kuutia upanga wangu mkononi mwake, lakini nitavunja mikono ya Farao, naye atalia kwa huzuni mbele yake kama mtu aliyetiwa jeraha la kumfisha. 25 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, lakini mikono ya Farao italegea. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi BWANA, nitakapoutia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye ataunyoosha dhidi ya Misri. 26 Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi mbalimbali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi BWANA.”

In Other Versions

Ezekiel 30 in the ANGEFD

Ezekiel 30 in the ANTPNG2D

Ezekiel 30 in the AS21

Ezekiel 30 in the BAGH

Ezekiel 30 in the BBPNG

Ezekiel 30 in the BBT1E

Ezekiel 30 in the BDS

Ezekiel 30 in the BEV

Ezekiel 30 in the BHAD

Ezekiel 30 in the BIB

Ezekiel 30 in the BLPT

Ezekiel 30 in the BNT

Ezekiel 30 in the BNTABOOT

Ezekiel 30 in the BNTLV

Ezekiel 30 in the BOATCB

Ezekiel 30 in the BOATCB2

Ezekiel 30 in the BOBCV

Ezekiel 30 in the BOCNT

Ezekiel 30 in the BOECS

Ezekiel 30 in the BOGWICC

Ezekiel 30 in the BOHCB

Ezekiel 30 in the BOHCV

Ezekiel 30 in the BOHLNT

Ezekiel 30 in the BOHNTLTAL

Ezekiel 30 in the BOICB

Ezekiel 30 in the BOILNTAP

Ezekiel 30 in the BOITCV

Ezekiel 30 in the BOKCV2

Ezekiel 30 in the BOKHWOG

Ezekiel 30 in the BOKSSV

Ezekiel 30 in the BOLCB

Ezekiel 30 in the BOLCB2

Ezekiel 30 in the BOMCV

Ezekiel 30 in the BONAV

Ezekiel 30 in the BONCB

Ezekiel 30 in the BONLT

Ezekiel 30 in the BONUT2

Ezekiel 30 in the BOPLNT

Ezekiel 30 in the BOSCB

Ezekiel 30 in the BOSNC

Ezekiel 30 in the BOTLNT

Ezekiel 30 in the BOVCB

Ezekiel 30 in the BOYCB

Ezekiel 30 in the BPBB

Ezekiel 30 in the BPH

Ezekiel 30 in the BSB

Ezekiel 30 in the CCB

Ezekiel 30 in the CUV

Ezekiel 30 in the CUVS

Ezekiel 30 in the DBT

Ezekiel 30 in the DGDNT

Ezekiel 30 in the DHNT

Ezekiel 30 in the DNT

Ezekiel 30 in the ELBE

Ezekiel 30 in the EMTV

Ezekiel 30 in the ESV

Ezekiel 30 in the FBV

Ezekiel 30 in the FEB

Ezekiel 30 in the GGMNT

Ezekiel 30 in the GNT

Ezekiel 30 in the HARY

Ezekiel 30 in the HNT

Ezekiel 30 in the IRVA

Ezekiel 30 in the IRVB

Ezekiel 30 in the IRVG

Ezekiel 30 in the IRVH

Ezekiel 30 in the IRVK

Ezekiel 30 in the IRVM

Ezekiel 30 in the IRVM2

Ezekiel 30 in the IRVO

Ezekiel 30 in the IRVP

Ezekiel 30 in the IRVT

Ezekiel 30 in the IRVT2

Ezekiel 30 in the IRVU

Ezekiel 30 in the ISVN

Ezekiel 30 in the JSNT

Ezekiel 30 in the KAPI

Ezekiel 30 in the KBT1ETNIK

Ezekiel 30 in the KBV

Ezekiel 30 in the KJV

Ezekiel 30 in the KNFD

Ezekiel 30 in the LBA

Ezekiel 30 in the LBLA

Ezekiel 30 in the LNT

Ezekiel 30 in the LSV

Ezekiel 30 in the MAAL

Ezekiel 30 in the MBV

Ezekiel 30 in the MBV2

Ezekiel 30 in the MHNT

Ezekiel 30 in the MKNFD

Ezekiel 30 in the MNG

Ezekiel 30 in the MNT

Ezekiel 30 in the MNT2

Ezekiel 30 in the MRS1T

Ezekiel 30 in the NAA

Ezekiel 30 in the NASB

Ezekiel 30 in the NBLA

Ezekiel 30 in the NBS

Ezekiel 30 in the NBVTP

Ezekiel 30 in the NET2

Ezekiel 30 in the NIV11

Ezekiel 30 in the NNT

Ezekiel 30 in the NNT2

Ezekiel 30 in the NNT3

Ezekiel 30 in the PDDPT

Ezekiel 30 in the PFNT

Ezekiel 30 in the RMNT

Ezekiel 30 in the SBIAS

Ezekiel 30 in the SBIBS

Ezekiel 30 in the SBIBS2

Ezekiel 30 in the SBICS

Ezekiel 30 in the SBIDS

Ezekiel 30 in the SBIGS

Ezekiel 30 in the SBIHS

Ezekiel 30 in the SBIIS

Ezekiel 30 in the SBIIS2

Ezekiel 30 in the SBIIS3

Ezekiel 30 in the SBIKS

Ezekiel 30 in the SBIKS2

Ezekiel 30 in the SBIMS

Ezekiel 30 in the SBIOS

Ezekiel 30 in the SBIPS

Ezekiel 30 in the SBISS

Ezekiel 30 in the SBITS

Ezekiel 30 in the SBITS2

Ezekiel 30 in the SBITS3

Ezekiel 30 in the SBITS4

Ezekiel 30 in the SBIUS

Ezekiel 30 in the SBIVS

Ezekiel 30 in the SBT

Ezekiel 30 in the SBT1E

Ezekiel 30 in the SCHL

Ezekiel 30 in the SNT

Ezekiel 30 in the SUSU

Ezekiel 30 in the SUSU2

Ezekiel 30 in the SYNO

Ezekiel 30 in the TBIAOTANT

Ezekiel 30 in the TBT1E

Ezekiel 30 in the TBT1E2

Ezekiel 30 in the TFTIP

Ezekiel 30 in the TFTU

Ezekiel 30 in the TGNTATF3T

Ezekiel 30 in the THAI

Ezekiel 30 in the TNFD

Ezekiel 30 in the TNT

Ezekiel 30 in the TNTIK

Ezekiel 30 in the TNTIL

Ezekiel 30 in the TNTIN

Ezekiel 30 in the TNTIP

Ezekiel 30 in the TNTIZ

Ezekiel 30 in the TOMA

Ezekiel 30 in the TTENT

Ezekiel 30 in the UBG

Ezekiel 30 in the UGV

Ezekiel 30 in the UGV2

Ezekiel 30 in the UGV3

Ezekiel 30 in the VBL

Ezekiel 30 in the VDCC

Ezekiel 30 in the YALU

Ezekiel 30 in the YAPE

Ezekiel 30 in the YBVTP

Ezekiel 30 in the ZBP