Genesis 46 (BOKCV)
1 Hivyo Israeli akaondoka na vyote vilivyokuwa mali yake, naye alipofika Beer-Sheba, akamtolea dhabihu Mungu wa Isaki baba yake. 2 Mungu akanena na Israeli katika maono usiku na kusema, “Yakobo! Yakobo!”Akajibu, “Mimi hapa.” 3 Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako, usiogope kushuka Misri, kwa maana huko nitakufanya taifa kubwa. 4 Nitashuka Misri pamoja nawe, nami hakika nitakurudisha tena Kanaani. Mikono ya Yosefu mwenyewe ndiyo itakayofunga macho yako.” 5 Ndipo Yakobo akaondoka Beer-Sheba nao wana wa Israeli wakamchukua baba yao Yakobo na watoto wao na wake zao katika magari ya kukokotwa yale Farao aliyokuwa amempelekea kumsafirisha. 6 Wakachukua pia mifugo yao na mali walizokuwa wamezipata Kanaani, Yakobo na uzao wake wote wakashuka Misri. 7 Akawachukua wanawe na binti zake, wajukuu wake wa kiume na wa kike, yaani uzao wake wote mpaka Misri. 8 Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli (Yakobo na wazao wake), waliokwenda Misri: Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. 9 Wana wa Reubeni ni:Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi. 10 Wana wa Simeoni ni:Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. 11 Wana wa Lawi ni:Gershoni, Kohathi na Merari. 12 Wana wa Yuda ni:Eri, Onani, Shela, Peresi na Zera (lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani).Wana wa Peresi ni:Hesroni na Hamuli. 13 Wana wa Isakari ni:Tola, Puva, Yashubu na Shimroni. 14 Wana wa Zabuloni ni:Seredi, Eloni na Yaleeli. 15 Hawa ndio wana wa Lea aliomzalia Yakobo huko Padan-Aramu pamoja na binti yake Dina. Jumla ya wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu. 16 Wana wa Gadi ni:Sefoni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi na Areli. 17 Wana wa Asheri ni:Imna, Ishva, Ishvi na Beria.Dada yao alikuwa Sera.Wana wa Beria ni:Heberi na Malkieli. 18 Hawa ndio watoto Zilpa aliomzalia Yakobo, ambao Labani alimpa binti yake Lea; jumla yao walikuwa kumi na sita. 19 Wana wa Raheli mke wa Yakobo ni:Yosefu na Benyamini. 20 Huko Misri, Asenathi binti wa Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni, alimzalia Yosefu wana wawili, Manase na Efraimu. 21 Wana wa Benyamini ni:Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu na Ardi. 22 Hawa ndio wana wa Raheli aliomzalia Yakobo; jumla yao ni kumi na wanne. 23 Mwana wa Dani ni:Hushimu. 24 Wana wa Naftali ni:Yaseeli, Guni, Yeseri na Shilemu. 25 Hawa walikuwa wana wa Bilha aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alikuwa amempa Raheli binti yake; jumla yao walikuwa saba. 26 Wote waliokwenda Misri pamoja na Yakobo, waliokuwa wazao wake hasa pasipo kuhesabu wakwe zake, walikuwa watu sitini na sita. 27 Pamoja na wana wawili waliozaliwa na Yosefu huko Misri, jumla yote ya jamaa ya Yakobo, waliokwenda Misri, walikuwa sabini. 28 Basi Yakobo akamtanguliza Yuda aende kwa Yosefu ili amwelekeze njia ya Gosheni. Walipofika nchi ya Gosheni, 29 gari kubwa zuri la Yosefu liliandaliwa, naye akaenda Gosheni kumlaki baba yake Israeli. Mara Yosefu alipofika mbele yake, alimkumbatia baba yake, akalia kwa muda mrefu. 30 Israeli akamwambia Yosefu, “Sasa niko tayari kufa, kwa kuwa nimejionea mwenyewe kwamba bado uko hai.” 31 Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, “Nitapanda kwa Farao na kumwambia, ‘Ndugu zangu na watu wa nyumbani mwa baba yangu, waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, wamekuja kwangu. 32 Watu hao ni wachunga mifugo, huchunga mifugo, wamekuja na makundi ya kondoo, mbuzi na ngʼombe pamoja na kila kitu walicho nacho.’ 33 Farao atakapowaita na kuwaulizeni, ‘Kazi yenu ni nini?’ 34 Mjibuni, ‘Watumwa wako wamekuwa wachunga mifugo tangu ujana wetu mpaka sasa, kama baba zetu walivyofanya.’ Ndipo mtakaporuhusiwa kukaa katika nchi ya Gosheni, kwa kuwa wachunga mifugo wote ni chukizo kwa Wamisri.”
In Other Versions
Genesis 46 in the ANGEFD
Genesis 46 in the ANTPNG2D
Genesis 46 in the AS21
Genesis 46 in the BAGH
Genesis 46 in the BBPNG
Genesis 46 in the BBT1E
Genesis 46 in the BDS
Genesis 46 in the BEV
Genesis 46 in the BHAD
Genesis 46 in the BIB
Genesis 46 in the BLPT
Genesis 46 in the BNT
Genesis 46 in the BNTABOOT
Genesis 46 in the BNTLV
Genesis 46 in the BOATCB
Genesis 46 in the BOATCB2
Genesis 46 in the BOBCV
Genesis 46 in the BOCNT
Genesis 46 in the BOECS
Genesis 46 in the BOGWICC
Genesis 46 in the BOHCB
Genesis 46 in the BOHCV
Genesis 46 in the BOHLNT
Genesis 46 in the BOHNTLTAL
Genesis 46 in the BOICB
Genesis 46 in the BOILNTAP
Genesis 46 in the BOITCV
Genesis 46 in the BOKCV2
Genesis 46 in the BOKHWOG
Genesis 46 in the BOKSSV
Genesis 46 in the BOLCB
Genesis 46 in the BOLCB2
Genesis 46 in the BOMCV
Genesis 46 in the BONAV
Genesis 46 in the BONCB
Genesis 46 in the BONLT
Genesis 46 in the BONUT2
Genesis 46 in the BOPLNT
Genesis 46 in the BOSCB
Genesis 46 in the BOSNC
Genesis 46 in the BOTLNT
Genesis 46 in the BOVCB
Genesis 46 in the BOYCB
Genesis 46 in the BPBB
Genesis 46 in the BPH
Genesis 46 in the BSB
Genesis 46 in the CCB
Genesis 46 in the CUV
Genesis 46 in the CUVS
Genesis 46 in the DBT
Genesis 46 in the DGDNT
Genesis 46 in the DHNT
Genesis 46 in the DNT
Genesis 46 in the ELBE
Genesis 46 in the EMTV
Genesis 46 in the ESV
Genesis 46 in the FBV
Genesis 46 in the FEB
Genesis 46 in the GGMNT
Genesis 46 in the GNT
Genesis 46 in the HARY
Genesis 46 in the HNT
Genesis 46 in the IRVA
Genesis 46 in the IRVB
Genesis 46 in the IRVG
Genesis 46 in the IRVH
Genesis 46 in the IRVK
Genesis 46 in the IRVM
Genesis 46 in the IRVM2
Genesis 46 in the IRVO
Genesis 46 in the IRVP
Genesis 46 in the IRVT
Genesis 46 in the IRVT2
Genesis 46 in the IRVU
Genesis 46 in the ISVN
Genesis 46 in the JSNT
Genesis 46 in the KAPI
Genesis 46 in the KBT1ETNIK
Genesis 46 in the KBV
Genesis 46 in the KJV
Genesis 46 in the KNFD
Genesis 46 in the LBA
Genesis 46 in the LBLA
Genesis 46 in the LNT
Genesis 46 in the LSV
Genesis 46 in the MAAL
Genesis 46 in the MBV
Genesis 46 in the MBV2
Genesis 46 in the MHNT
Genesis 46 in the MKNFD
Genesis 46 in the MNG
Genesis 46 in the MNT
Genesis 46 in the MNT2
Genesis 46 in the MRS1T
Genesis 46 in the NAA
Genesis 46 in the NASB
Genesis 46 in the NBLA
Genesis 46 in the NBS
Genesis 46 in the NBVTP
Genesis 46 in the NET2
Genesis 46 in the NIV11
Genesis 46 in the NNT
Genesis 46 in the NNT2
Genesis 46 in the NNT3
Genesis 46 in the PDDPT
Genesis 46 in the PFNT
Genesis 46 in the RMNT
Genesis 46 in the SBIAS
Genesis 46 in the SBIBS
Genesis 46 in the SBIBS2
Genesis 46 in the SBICS
Genesis 46 in the SBIDS
Genesis 46 in the SBIGS
Genesis 46 in the SBIHS
Genesis 46 in the SBIIS
Genesis 46 in the SBIIS2
Genesis 46 in the SBIIS3
Genesis 46 in the SBIKS
Genesis 46 in the SBIKS2
Genesis 46 in the SBIMS
Genesis 46 in the SBIOS
Genesis 46 in the SBIPS
Genesis 46 in the SBISS
Genesis 46 in the SBITS
Genesis 46 in the SBITS2
Genesis 46 in the SBITS3
Genesis 46 in the SBITS4
Genesis 46 in the SBIUS
Genesis 46 in the SBIVS
Genesis 46 in the SBT
Genesis 46 in the SBT1E
Genesis 46 in the SCHL
Genesis 46 in the SNT
Genesis 46 in the SUSU
Genesis 46 in the SUSU2
Genesis 46 in the SYNO
Genesis 46 in the TBIAOTANT
Genesis 46 in the TBT1E
Genesis 46 in the TBT1E2
Genesis 46 in the TFTIP
Genesis 46 in the TFTU
Genesis 46 in the TGNTATF3T
Genesis 46 in the THAI
Genesis 46 in the TNFD
Genesis 46 in the TNT
Genesis 46 in the TNTIK
Genesis 46 in the TNTIL
Genesis 46 in the TNTIN
Genesis 46 in the TNTIP
Genesis 46 in the TNTIZ
Genesis 46 in the TOMA
Genesis 46 in the TTENT
Genesis 46 in the UBG
Genesis 46 in the UGV
Genesis 46 in the UGV2
Genesis 46 in the UGV3
Genesis 46 in the VBL
Genesis 46 in the VDCC
Genesis 46 in the YALU
Genesis 46 in the YAPE
Genesis 46 in the YBVTP
Genesis 46 in the ZBP