Isaiah 14 (BOKCV)

1 BWANA atamhurumia Yakobo,atamchagua Israeli tena,na kuwakalisha katika nchi yao wenyewe.Wageni wataungana naona kujiunga na nyumba ya Yakobo. 2 Mataifa watawachukuana kuwaleta mahali pao wenyewe.Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifakama watumishi na wajakazi katika nchi ya BWANA.Watawafanya watekaji wao kuwa mateka,na kutawala juu ya wale waliowaonea. 3 Katika siku BWANA atakapokuondolea mateso, udhia na utumwa wa kikatili, 4 utaichukua dhihaka hii dhidi ya mfalme wa Babeli:Tazama jinsi mtesi alivyofikia mwisho!Tazama jinsi ghadhabu yake kali ilivyokoma! 5 BWANA amevunja fimbo ya mwovu,fimbo ya utawala ya watawala, 6 ambayo kwa hasira waliyapiga mataifakwa mapigo yasiyo na kikomo,nao kwa ghadhabu kali waliwatiisha mataifakwa jeuri pasipo huruma. 7 Nchi zote ziko kwenye mapumziko na kwenye amani,wanabubujika kwa kuimba. 8 Hata misunobari na mierezi ya Lebanoniinashangilia mbele yako na kusema,“Basi kwa sababu umeangushwa chini,hakuna mkata miti atakayekuja kutukata.” 9 Kuzimu kote kumetaharukikukulaki unapokuja,kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea,wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu,kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme:wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa. 10 Wote wataitikia,watakuambia,“Wewe pia umekuwa dhaifu, kama sisi tulivyo;wewe umekuwa kama sisi.” 11 Majivuno yako yote yameshushwa mpaka kuzimu,pamoja na kelele ya vinubi vyako,mafunza yametanda chini yako,na minyoo imekufunika. 12 Tazama jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni,ewe nyota ya asubuhi, mwana wa mapambazuko!Umetupwa chini duniani,wewe uliyepata kuangusha mataifa! 13 Ulisema moyoni mwako,“Nitapanda juu hadi mbinguni,nitakiinua kiti changu cha enzijuu ya nyota za Mungu,nitaketi nimetawazwajuu ya mlima wa kusanyiko,kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu. 14 Nitapaa juu kupita mawingu,nitajifanya kama Yeye Aliye Juu Sana.” 15 Lakini umeshushwa chini hadi kuzimu,hadi kwenye vina vya shimo. 16 Wale wanaokuona wanakukazia macho,wanatafakari hatima yako:“Je, huyu ndiye yule aliyetikisa duniana kufanya falme zitetemeke, 17 yule aliyeifanya dunia kuwa jangwa,aliyeipindua miji yake,na ambaye hakuwaachia mateka wakewaende nyumbani?” 18 Wafalme wote wa mataifa wamelala kwa heshimakila mmoja katika kaburi lake. 19 Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lakokama tawi lililokataliwa,umefunikwa na waliouawapamoja na wale waliochomwa kwa upanga,wale washukao mpakakwenye mawe ya shimo.Kama mzoga uliokanyagwa chini ya nyayo, 20 Hutajumuika nao kwenye mazishi,kwa kuwa umeharibu nchi yakona kuwaua watu wako. Mzao wa mwovuhatatajwa tena kamwe. 21 Andaa mahali pa kuwachinjia wanawekwa ajili ya dhambi za baba zao,wasije wakainuka ili kuirithi nchina kuijaza dunia kwa miji yao. 22 BWANA Mwenye Nguvu Zote asema,“Nitainuka dhidi yao,nitalikatilia mbali jina lake kutoka Babeli pamoja na watu wake walionusurika,watoto wake na wazao wake,”asema BWANA. 23 “Nitaifanya kuwa mahali pa bundi,na kuwa nchi ya matope;nitaifagia kwa ufagio wa maangamizi,”asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. 24 BWANA Mwenye Nguvu Zote ameapa,“Hakika, kama vile nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa,nami kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyosimama. 25 Nitamponda Mwashuru katika nchi yangu,juu ya milima yangu nitawakanyagia chini.Nira yake itaondolewa kutoka kwa watu wangu,nao mzigo wake utaondolewa kutoka mabegani mwao.” 26 Huu ndio mpango uliokusudiwa kwa ajili ya ulimwengu wote,huu ni mkono ulionyooshwa juu ya mataifa yote. 27 Kwa kuwa BWANA Mwenye Nguvu Zote amekusudia,ni nani awezaye kumzuia?Mkono wake umenyooshwa,ni nani awezaye kuurudisha? 28 Neno hili lilikuja mwaka ule Mfalme Ahazi alipofariki: 29 Msifurahi, enyi Wafilisti wote,kwamba fimbo iliyowapiga imevunjika;kutoka mzizi wa huyo nyokaatachipuka nyoka mwenye sumu kali,uzao wake utakuwa joka lirukalo,lenye sumu kali. 30 Maskini kuliko maskini wote watapata malisho,nao wahitaji watalala salama.Lakini mzizi wako nitauangamiza kwa njaa,nayo njaa itawaua walionusurika. 31 Piga yowe, ee lango! Bweka, ee mji!Yeyukeni, enyi Wafilisti wote!Wingu la moshi linakuja toka kaskazini,wala hakuna atakayechelewa katika safu zake. 32 Ni jibu gani litakalotolewakwa wajumbe wa taifa hilo?“BWANA ameifanya imara Sayuni,nako ndani yake watu wake walioonewa watapata kimbilio.”

In Other Versions

Isaiah 14 in the ANGEFD

Isaiah 14 in the ANTPNG2D

Isaiah 14 in the AS21

Isaiah 14 in the BAGH

Isaiah 14 in the BBPNG

Isaiah 14 in the BBT1E

Isaiah 14 in the BDS

Isaiah 14 in the BEV

Isaiah 14 in the BHAD

Isaiah 14 in the BIB

Isaiah 14 in the BLPT

Isaiah 14 in the BNT

Isaiah 14 in the BNTABOOT

Isaiah 14 in the BNTLV

Isaiah 14 in the BOATCB

Isaiah 14 in the BOATCB2

Isaiah 14 in the BOBCV

Isaiah 14 in the BOCNT

Isaiah 14 in the BOECS

Isaiah 14 in the BOGWICC

Isaiah 14 in the BOHCB

Isaiah 14 in the BOHCV

Isaiah 14 in the BOHLNT

Isaiah 14 in the BOHNTLTAL

Isaiah 14 in the BOICB

Isaiah 14 in the BOILNTAP

Isaiah 14 in the BOITCV

Isaiah 14 in the BOKCV2

Isaiah 14 in the BOKHWOG

Isaiah 14 in the BOKSSV

Isaiah 14 in the BOLCB

Isaiah 14 in the BOLCB2

Isaiah 14 in the BOMCV

Isaiah 14 in the BONAV

Isaiah 14 in the BONCB

Isaiah 14 in the BONLT

Isaiah 14 in the BONUT2

Isaiah 14 in the BOPLNT

Isaiah 14 in the BOSCB

Isaiah 14 in the BOSNC

Isaiah 14 in the BOTLNT

Isaiah 14 in the BOVCB

Isaiah 14 in the BOYCB

Isaiah 14 in the BPBB

Isaiah 14 in the BPH

Isaiah 14 in the BSB

Isaiah 14 in the CCB

Isaiah 14 in the CUV

Isaiah 14 in the CUVS

Isaiah 14 in the DBT

Isaiah 14 in the DGDNT

Isaiah 14 in the DHNT

Isaiah 14 in the DNT

Isaiah 14 in the ELBE

Isaiah 14 in the EMTV

Isaiah 14 in the ESV

Isaiah 14 in the FBV

Isaiah 14 in the FEB

Isaiah 14 in the GGMNT

Isaiah 14 in the GNT

Isaiah 14 in the HARY

Isaiah 14 in the HNT

Isaiah 14 in the IRVA

Isaiah 14 in the IRVB

Isaiah 14 in the IRVG

Isaiah 14 in the IRVH

Isaiah 14 in the IRVK

Isaiah 14 in the IRVM

Isaiah 14 in the IRVM2

Isaiah 14 in the IRVO

Isaiah 14 in the IRVP

Isaiah 14 in the IRVT

Isaiah 14 in the IRVT2

Isaiah 14 in the IRVU

Isaiah 14 in the ISVN

Isaiah 14 in the JSNT

Isaiah 14 in the KAPI

Isaiah 14 in the KBT1ETNIK

Isaiah 14 in the KBV

Isaiah 14 in the KJV

Isaiah 14 in the KNFD

Isaiah 14 in the LBA

Isaiah 14 in the LBLA

Isaiah 14 in the LNT

Isaiah 14 in the LSV

Isaiah 14 in the MAAL

Isaiah 14 in the MBV

Isaiah 14 in the MBV2

Isaiah 14 in the MHNT

Isaiah 14 in the MKNFD

Isaiah 14 in the MNG

Isaiah 14 in the MNT

Isaiah 14 in the MNT2

Isaiah 14 in the MRS1T

Isaiah 14 in the NAA

Isaiah 14 in the NASB

Isaiah 14 in the NBLA

Isaiah 14 in the NBS

Isaiah 14 in the NBVTP

Isaiah 14 in the NET2

Isaiah 14 in the NIV11

Isaiah 14 in the NNT

Isaiah 14 in the NNT2

Isaiah 14 in the NNT3

Isaiah 14 in the PDDPT

Isaiah 14 in the PFNT

Isaiah 14 in the RMNT

Isaiah 14 in the SBIAS

Isaiah 14 in the SBIBS

Isaiah 14 in the SBIBS2

Isaiah 14 in the SBICS

Isaiah 14 in the SBIDS

Isaiah 14 in the SBIGS

Isaiah 14 in the SBIHS

Isaiah 14 in the SBIIS

Isaiah 14 in the SBIIS2

Isaiah 14 in the SBIIS3

Isaiah 14 in the SBIKS

Isaiah 14 in the SBIKS2

Isaiah 14 in the SBIMS

Isaiah 14 in the SBIOS

Isaiah 14 in the SBIPS

Isaiah 14 in the SBISS

Isaiah 14 in the SBITS

Isaiah 14 in the SBITS2

Isaiah 14 in the SBITS3

Isaiah 14 in the SBITS4

Isaiah 14 in the SBIUS

Isaiah 14 in the SBIVS

Isaiah 14 in the SBT

Isaiah 14 in the SBT1E

Isaiah 14 in the SCHL

Isaiah 14 in the SNT

Isaiah 14 in the SUSU

Isaiah 14 in the SUSU2

Isaiah 14 in the SYNO

Isaiah 14 in the TBIAOTANT

Isaiah 14 in the TBT1E

Isaiah 14 in the TBT1E2

Isaiah 14 in the TFTIP

Isaiah 14 in the TFTU

Isaiah 14 in the TGNTATF3T

Isaiah 14 in the THAI

Isaiah 14 in the TNFD

Isaiah 14 in the TNT

Isaiah 14 in the TNTIK

Isaiah 14 in the TNTIL

Isaiah 14 in the TNTIN

Isaiah 14 in the TNTIP

Isaiah 14 in the TNTIZ

Isaiah 14 in the TOMA

Isaiah 14 in the TTENT

Isaiah 14 in the UBG

Isaiah 14 in the UGV

Isaiah 14 in the UGV2

Isaiah 14 in the UGV3

Isaiah 14 in the VBL

Isaiah 14 in the VDCC

Isaiah 14 in the YALU

Isaiah 14 in the YAPE

Isaiah 14 in the YBVTP

Isaiah 14 in the ZBP