Isaiah 40 (BOKCV)

1 Wafarijini, wafarijini watu wangu,asema Mungu wenu. 2 Sema na Yerusalemu kwa upole,umtangaziekwamba kazi yake ngumu imekamilika,kwamba dhambi yake imefanyiwa fidia,kwamba amepokea kutoka mkononi mwa BWANAmaradufu kwa ajili ya dhambi zake zote. 3 Sauti ya mtu aliaye:“Itengenezeni jangwani njia ya BWANA,nyoosheni njia kuu nyikanikwa ajili ya Mungu wetu. 4 Kila bonde litainuliwa,kila mlima na kilima kitashushwa;penye mabonde patanyooshwa,napo palipoparuza patasawazishwa. 5 Utukufu wa BWANA utafunuliwa,nao wanadamu wote watauona pamoja.Kwa maana kinywa cha BWANA kimenena.” 6 Sauti husema, “Piga kelele.”Nami nikasema, “Nipige kelele gani?” “Wanadamu wote ni kama majani,nao utukufu wao woteni kama maua ya kondeni. 7 Majani hunyauka na maua huanguka,kwa sababu pumzi ya BWANA huyapuliza.Hakika wanadamu ni majani. 8 Majani hunyauka na maua huanguka,lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.” 9 Wewe uletaye habari njema Sayuni,panda juu ya mlima mrefu.Wewe uletaye habari njema Yerusalemu,inua sauti yako kwa kupiga kelele,inua sauti, usiogope;iambie miji ya Yuda,“Yuko hapa Mungu wenu!” 10 Tazameni, BWANA Mwenyezi anakuja na nguvu,nao mkono wake ndio utawalao kwa ajili yake.Tazameni, ujira wake u pamoja naye,nayo malipo yake yanafuatana naye. 11 Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo:Hukusanya wana-kondoo katika mikono yakena kuwachukua karibu na moyo wake,huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao. 12 Ni nani aliyepima maji ya baharikwenye konzi ya mkono wake,au kuzipima mbingu kwa shibiri yake?Ni nani aliyeyashika mavumbi ya dunia katika kikapu,au kupima milima kwenye kipimiona vilima kwenye mizani? 13 Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya BWANA,au kumfundisha akiwa kama mshauri wake? 14 Ni nani ambaye BWANA ametaka shauri kwake ili kumwelimisha,naye ni nani aliyemfundisha njia iliyo sawa?Ni nani aliyemfundisha maarifaau kumwonyesha mapito ya ufahamu? 15 Hakika mataifa ni kama tone ndani ya ndoo,ni kama vumbi jembamba juu ya mizani,huvipima visiwa kana kwamba vilikuwa vumbi laini. 16 Lebanoni hautoshi kwa moto wa madhabahuni,wala wanyama wake hawatoshi kwa sadaka za kuteketezwa. 17 Mbele yake mataifa yote ni kama si kitu,yanaonekana yasio na thamanina zaidi ya bure kabisa. 18 Basi, utamlinganisha Mungu na nani?Utamlinganisha na kitu gani? 19 Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu,naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabuna kuitengenezea mikufu ya fedha. 20 Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hiihuuchagua mti usiooza.Humtafuta fundi stadiwa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika. 21 Je, hujui?Je, hujasikia?Je, hujaambiwa tangu mwanzo?Je, hujafahamu tangu kuumbwa kwa dunia? 22 Anakaa kwenye kiti cha enzi juu ya duara ya dunia,nao watu wakaao ndani yake ni kama panzi.Huzitandaza mbingu kama chandarua,na kuzitandaza kama hema la kuishi. 23 Huwafanya wakuu kuwa si kitu,na kuwashusha watawala wa dunia hii kuwa kitu bure. 24 Mara baada ya kupandwa,mara baada ya kutiwa ardhini,mara baada ya kutoa mizizi yao ardhini,ndipo huwapulizia nao wakanyauka,nao upepo wa kisulisulihuwapeperusha kama makapi. 25 “Utanilinganisha mimi na nani?Au ni nani anayelingana nami?” asema yeye Aliye Mtakatifu. 26 Inueni macho yenu mtazame mbinguni:Ni nani aliyeumba hivi vyote?Ni yeye aletaye nje jeshi la nyota moja baada ya nyinginena kuziita kila moja kwa jina lake.Kwa sababu ya uweza wake mkuu na nguvu zake kuu,hakuna hata mojawapo inayokosekana. 27 Kwa nini unasema, ee Yakobo,nanyi ee Israeli, kulalamika,“Njia yangu imefichwa BWANA asiione,Mungu wangu hajali shauri langu?” 28 Je wewe, hufahamu?Je wewe, hujasikia? BWANA ni Mungu wa milele,Muumba wa miisho ya dunia.Hatachoka wala kulegea,wala hakuna hata mmojaawezaye kuupima ufahamu wake. 29 Huwapa nguvu waliolegeana huongeza nguvu za wadhaifu. 30 Hata vijana huchoka na kulegea,nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka, 31 bali wale wamtumainio BWANAatafanya upya nguvu zao.Watapaa juu kwa mbawa kama tai;watapiga mbio wala hawatachoka,watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

In Other Versions

Isaiah 40 in the ANGEFD

Isaiah 40 in the ANTPNG2D

Isaiah 40 in the AS21

Isaiah 40 in the BAGH

Isaiah 40 in the BBPNG

Isaiah 40 in the BBT1E

Isaiah 40 in the BDS

Isaiah 40 in the BEV

Isaiah 40 in the BHAD

Isaiah 40 in the BIB

Isaiah 40 in the BLPT

Isaiah 40 in the BNT

Isaiah 40 in the BNTABOOT

Isaiah 40 in the BNTLV

Isaiah 40 in the BOATCB

Isaiah 40 in the BOATCB2

Isaiah 40 in the BOBCV

Isaiah 40 in the BOCNT

Isaiah 40 in the BOECS

Isaiah 40 in the BOGWICC

Isaiah 40 in the BOHCB

Isaiah 40 in the BOHCV

Isaiah 40 in the BOHLNT

Isaiah 40 in the BOHNTLTAL

Isaiah 40 in the BOICB

Isaiah 40 in the BOILNTAP

Isaiah 40 in the BOITCV

Isaiah 40 in the BOKCV2

Isaiah 40 in the BOKHWOG

Isaiah 40 in the BOKSSV

Isaiah 40 in the BOLCB

Isaiah 40 in the BOLCB2

Isaiah 40 in the BOMCV

Isaiah 40 in the BONAV

Isaiah 40 in the BONCB

Isaiah 40 in the BONLT

Isaiah 40 in the BONUT2

Isaiah 40 in the BOPLNT

Isaiah 40 in the BOSCB

Isaiah 40 in the BOSNC

Isaiah 40 in the BOTLNT

Isaiah 40 in the BOVCB

Isaiah 40 in the BOYCB

Isaiah 40 in the BPBB

Isaiah 40 in the BPH

Isaiah 40 in the BSB

Isaiah 40 in the CCB

Isaiah 40 in the CUV

Isaiah 40 in the CUVS

Isaiah 40 in the DBT

Isaiah 40 in the DGDNT

Isaiah 40 in the DHNT

Isaiah 40 in the DNT

Isaiah 40 in the ELBE

Isaiah 40 in the EMTV

Isaiah 40 in the ESV

Isaiah 40 in the FBV

Isaiah 40 in the FEB

Isaiah 40 in the GGMNT

Isaiah 40 in the GNT

Isaiah 40 in the HARY

Isaiah 40 in the HNT

Isaiah 40 in the IRVA

Isaiah 40 in the IRVB

Isaiah 40 in the IRVG

Isaiah 40 in the IRVH

Isaiah 40 in the IRVK

Isaiah 40 in the IRVM

Isaiah 40 in the IRVM2

Isaiah 40 in the IRVO

Isaiah 40 in the IRVP

Isaiah 40 in the IRVT

Isaiah 40 in the IRVT2

Isaiah 40 in the IRVU

Isaiah 40 in the ISVN

Isaiah 40 in the JSNT

Isaiah 40 in the KAPI

Isaiah 40 in the KBT1ETNIK

Isaiah 40 in the KBV

Isaiah 40 in the KJV

Isaiah 40 in the KNFD

Isaiah 40 in the LBA

Isaiah 40 in the LBLA

Isaiah 40 in the LNT

Isaiah 40 in the LSV

Isaiah 40 in the MAAL

Isaiah 40 in the MBV

Isaiah 40 in the MBV2

Isaiah 40 in the MHNT

Isaiah 40 in the MKNFD

Isaiah 40 in the MNG

Isaiah 40 in the MNT

Isaiah 40 in the MNT2

Isaiah 40 in the MRS1T

Isaiah 40 in the NAA

Isaiah 40 in the NASB

Isaiah 40 in the NBLA

Isaiah 40 in the NBS

Isaiah 40 in the NBVTP

Isaiah 40 in the NET2

Isaiah 40 in the NIV11

Isaiah 40 in the NNT

Isaiah 40 in the NNT2

Isaiah 40 in the NNT3

Isaiah 40 in the PDDPT

Isaiah 40 in the PFNT

Isaiah 40 in the RMNT

Isaiah 40 in the SBIAS

Isaiah 40 in the SBIBS

Isaiah 40 in the SBIBS2

Isaiah 40 in the SBICS

Isaiah 40 in the SBIDS

Isaiah 40 in the SBIGS

Isaiah 40 in the SBIHS

Isaiah 40 in the SBIIS

Isaiah 40 in the SBIIS2

Isaiah 40 in the SBIIS3

Isaiah 40 in the SBIKS

Isaiah 40 in the SBIKS2

Isaiah 40 in the SBIMS

Isaiah 40 in the SBIOS

Isaiah 40 in the SBIPS

Isaiah 40 in the SBISS

Isaiah 40 in the SBITS

Isaiah 40 in the SBITS2

Isaiah 40 in the SBITS3

Isaiah 40 in the SBITS4

Isaiah 40 in the SBIUS

Isaiah 40 in the SBIVS

Isaiah 40 in the SBT

Isaiah 40 in the SBT1E

Isaiah 40 in the SCHL

Isaiah 40 in the SNT

Isaiah 40 in the SUSU

Isaiah 40 in the SUSU2

Isaiah 40 in the SYNO

Isaiah 40 in the TBIAOTANT

Isaiah 40 in the TBT1E

Isaiah 40 in the TBT1E2

Isaiah 40 in the TFTIP

Isaiah 40 in the TFTU

Isaiah 40 in the TGNTATF3T

Isaiah 40 in the THAI

Isaiah 40 in the TNFD

Isaiah 40 in the TNT

Isaiah 40 in the TNTIK

Isaiah 40 in the TNTIL

Isaiah 40 in the TNTIN

Isaiah 40 in the TNTIP

Isaiah 40 in the TNTIZ

Isaiah 40 in the TOMA

Isaiah 40 in the TTENT

Isaiah 40 in the UBG

Isaiah 40 in the UGV

Isaiah 40 in the UGV2

Isaiah 40 in the UGV3

Isaiah 40 in the VBL

Isaiah 40 in the VDCC

Isaiah 40 in the YALU

Isaiah 40 in the YAPE

Isaiah 40 in the YBVTP

Isaiah 40 in the ZBP