Isaiah 42 (BOKCV)
1 “Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza,mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye;nitaweka Roho yangu juu yake,naye ataleta haki kwa mataifa. 2 Hatapaza sauti wala kupiga kelele,wala hataiinua sauti yake barabarani. 3 Mwanzi uliopondeka hatauvunja,na utambi unaofuka moshi hatauzima.Kwa uaminifu ataleta haki, 4 hatazimia roho wala kukata tamaa,mpaka atakaposimamisha haki juu ya dunia.Visiwa vitaweka tumaini lao katika sheria yake.” 5 Hili ndilo asemalo Mungu, BWANA,yeye aliyeziumba mbingu na kuzitanda,aliyeitandaza dunia na vyote vitokavyo humo,awapaye watu wake pumzi,na uzima kwa wale waendao humo: 6 “Mimi, BWANA, nimekuita katika haki;nitakushika mkono wako.Nitakulinda na kukufanyakuwa Agano kwa ajili ya watuna nuru kwa Mataifa, 7 kuwafungua macho wale wasioona,kuwaacha huru kutoka kifungoni waliofungwa jela,na kuwafungua kutoka gerezaniwale wanaokaa gizani. 8 “Mimi ndimi BWANA; hilo ndilo Jina langu!Sitampa mwingine utukufu wanguwala sanamu sifa zangu. 9 Tazama, mambo ya kwanza yametokea,nami natangaza mambo mapya;kabla hayajatokeanawatangazia habari zake.” 10 Mwimbieni BWANA wimbo mpya,sifa zake toka miisho ya dunia,ninyi mshukao chini baharini,na vyote vilivyomo ndani yake,enyi visiwa na wote wakaao ndani yake. 11 Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao;makao anamoishi Kedari na yashangilie.Watu wa Sela waimbe kwa furaha,na wapige kelele kutoka vilele vya milima. 12 Wampe BWANA utukufu,na kutangaza sifa zake katika visiwa. 13 BWANA ataenda kama mtu mwenye nguvu,kama shujaa atachochea shauku yake,kwa kelele ataamsha kilio cha vita,naye atashinda adui zake. 14 “Kwa muda mrefu nimenyamaza kimya,nimekaa kimya na kujizuia.Lakini sasa, kama mwanamke wakati wa kujifungua,ninapiga kelele, ninatweta na kushusha pumzi. 15 Nitaharibu milima na vilimana kukausha mimea yako yote;nitafanya mito kuwa visiwana kukausha mabwawa. 16 Nitawaongoza vipofu kwenye njia ambayo hawajaijua,kwenye mapito wasiyoyazoea nitawaongoza;nitafanya giza kuwa nuru mbele yao,na kufanya mahali palipoparuza kuwa laini.Haya ndiyo mambo nitakayofanya;mimi sitawaacha. 17 Lakini wale wanaotumaini sanamu,wanaoviambia vinyago, ‘Ninyi ndio miungu yetu,’watarudishwa nyuma kwa aibu kubwa. 18 “Sikieni, enyi viziwi;tazameni, enyi vipofu, mpate kuona! 19 Ni nani aliye kipofu isipokuwa mtumishi wangu,na kiziwi kama mjumbe ninayemtuma?Ni nani aliye kipofu kama yeye aliyejitoa kwangu,aliye kipofu kama mtumishi wa BWANA? 20 Mmeona vitu vingi, lakini hamkuzingatia;masikio yenu yako wazi, lakini hamsikii chochote.” 21 Ilimpendeza BWANAkwa ajili ya haki yakekufanya sheria yake kuwa kuu na tukufu. 22 Lakini hili ni taifa lililoibwa na kutekwa nyara,wote wamenaswa katika mashimo,au wamefichwa katika magereza.Wamekuwa nyara,wala hapana yeyote awaokoaye.Wamefanywa mateka,wala hapana yeyote asemaye, “Warudishe.” 23 Ni nani miongoni mwenu atakayesikiliza hili,au atakayezingatia kwa makini katika wakati ujao? 24 Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka,na Israeli kwa wateka nyara?Je, hakuwa yeye, BWANA,ambaye tumetenda dhambi dhidi yake?Kwa kuwa hawakufuata njia zake,hawakutii sheria zake. 25 Hivyo akawamwagia hasira yake inayowaka,ukali wa vita.Iliwazunguka kwa miali ya moto, lakini hata hivyo hawakuelewa;iliwateketeza, lakini hawakuyatia moyoni.
In Other Versions
Isaiah 42 in the ANGEFD
Isaiah 42 in the ANTPNG2D
Isaiah 42 in the AS21
Isaiah 42 in the BAGH
Isaiah 42 in the BBPNG
Isaiah 42 in the BBT1E
Isaiah 42 in the BDS
Isaiah 42 in the BEV
Isaiah 42 in the BHAD
Isaiah 42 in the BIB
Isaiah 42 in the BLPT
Isaiah 42 in the BNT
Isaiah 42 in the BNTABOOT
Isaiah 42 in the BNTLV
Isaiah 42 in the BOATCB
Isaiah 42 in the BOATCB2
Isaiah 42 in the BOBCV
Isaiah 42 in the BOCNT
Isaiah 42 in the BOECS
Isaiah 42 in the BOGWICC
Isaiah 42 in the BOHCB
Isaiah 42 in the BOHCV
Isaiah 42 in the BOHLNT
Isaiah 42 in the BOHNTLTAL
Isaiah 42 in the BOICB
Isaiah 42 in the BOILNTAP
Isaiah 42 in the BOITCV
Isaiah 42 in the BOKCV2
Isaiah 42 in the BOKHWOG
Isaiah 42 in the BOKSSV
Isaiah 42 in the BOLCB
Isaiah 42 in the BOLCB2
Isaiah 42 in the BOMCV
Isaiah 42 in the BONAV
Isaiah 42 in the BONCB
Isaiah 42 in the BONLT
Isaiah 42 in the BONUT2
Isaiah 42 in the BOPLNT
Isaiah 42 in the BOSCB
Isaiah 42 in the BOSNC
Isaiah 42 in the BOTLNT
Isaiah 42 in the BOVCB
Isaiah 42 in the BOYCB
Isaiah 42 in the BPBB
Isaiah 42 in the BPH
Isaiah 42 in the BSB
Isaiah 42 in the CCB
Isaiah 42 in the CUV
Isaiah 42 in the CUVS
Isaiah 42 in the DBT
Isaiah 42 in the DGDNT
Isaiah 42 in the DHNT
Isaiah 42 in the DNT
Isaiah 42 in the ELBE
Isaiah 42 in the EMTV
Isaiah 42 in the ESV
Isaiah 42 in the FBV
Isaiah 42 in the FEB
Isaiah 42 in the GGMNT
Isaiah 42 in the GNT
Isaiah 42 in the HARY
Isaiah 42 in the HNT
Isaiah 42 in the IRVA
Isaiah 42 in the IRVB
Isaiah 42 in the IRVG
Isaiah 42 in the IRVH
Isaiah 42 in the IRVK
Isaiah 42 in the IRVM
Isaiah 42 in the IRVM2
Isaiah 42 in the IRVO
Isaiah 42 in the IRVP
Isaiah 42 in the IRVT
Isaiah 42 in the IRVT2
Isaiah 42 in the IRVU
Isaiah 42 in the ISVN
Isaiah 42 in the JSNT
Isaiah 42 in the KAPI
Isaiah 42 in the KBT1ETNIK
Isaiah 42 in the KBV
Isaiah 42 in the KJV
Isaiah 42 in the KNFD
Isaiah 42 in the LBA
Isaiah 42 in the LBLA
Isaiah 42 in the LNT
Isaiah 42 in the LSV
Isaiah 42 in the MAAL
Isaiah 42 in the MBV
Isaiah 42 in the MBV2
Isaiah 42 in the MHNT
Isaiah 42 in the MKNFD
Isaiah 42 in the MNG
Isaiah 42 in the MNT
Isaiah 42 in the MNT2
Isaiah 42 in the MRS1T
Isaiah 42 in the NAA
Isaiah 42 in the NASB
Isaiah 42 in the NBLA
Isaiah 42 in the NBS
Isaiah 42 in the NBVTP
Isaiah 42 in the NET2
Isaiah 42 in the NIV11
Isaiah 42 in the NNT
Isaiah 42 in the NNT2
Isaiah 42 in the NNT3
Isaiah 42 in the PDDPT
Isaiah 42 in the PFNT
Isaiah 42 in the RMNT
Isaiah 42 in the SBIAS
Isaiah 42 in the SBIBS
Isaiah 42 in the SBIBS2
Isaiah 42 in the SBICS
Isaiah 42 in the SBIDS
Isaiah 42 in the SBIGS
Isaiah 42 in the SBIHS
Isaiah 42 in the SBIIS
Isaiah 42 in the SBIIS2
Isaiah 42 in the SBIIS3
Isaiah 42 in the SBIKS
Isaiah 42 in the SBIKS2
Isaiah 42 in the SBIMS
Isaiah 42 in the SBIOS
Isaiah 42 in the SBIPS
Isaiah 42 in the SBISS
Isaiah 42 in the SBITS
Isaiah 42 in the SBITS2
Isaiah 42 in the SBITS3
Isaiah 42 in the SBITS4
Isaiah 42 in the SBIUS
Isaiah 42 in the SBIVS
Isaiah 42 in the SBT
Isaiah 42 in the SBT1E
Isaiah 42 in the SCHL
Isaiah 42 in the SNT
Isaiah 42 in the SUSU
Isaiah 42 in the SUSU2
Isaiah 42 in the SYNO
Isaiah 42 in the TBIAOTANT
Isaiah 42 in the TBT1E
Isaiah 42 in the TBT1E2
Isaiah 42 in the TFTIP
Isaiah 42 in the TFTU
Isaiah 42 in the TGNTATF3T
Isaiah 42 in the THAI
Isaiah 42 in the TNFD
Isaiah 42 in the TNT
Isaiah 42 in the TNTIK
Isaiah 42 in the TNTIL
Isaiah 42 in the TNTIN
Isaiah 42 in the TNTIP
Isaiah 42 in the TNTIZ
Isaiah 42 in the TOMA
Isaiah 42 in the TTENT
Isaiah 42 in the UBG
Isaiah 42 in the UGV
Isaiah 42 in the UGV2
Isaiah 42 in the UGV3
Isaiah 42 in the VBL
Isaiah 42 in the VDCC
Isaiah 42 in the YALU
Isaiah 42 in the YAPE
Isaiah 42 in the YBVTP
Isaiah 42 in the ZBP