John 2 (BOKCV)
1 Siku ya tatu kulikuwa na arusi katika mji wa Kana ya Galilaya, naye mama yake Yesu alikuwepo pale. 2 Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. 3 Divai ilipokwisha, mama yake Yesu akamwambia, “Wameishiwa na divai.” 4 Yesu akamwambia, “Mwanamke, nina nini nawe? Saa yangu haijawadia.” 5 Mama yake akawaambia wale watumishi, “Lolote atakalowaambia, fanyeni.” 6 Basi ilikuwepo mitungi sita ya kuhifadhia maji iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu. 7 Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni hiyo mitungi maji.” Nao wakaijaza ile mitungi mpaka juu. 8 Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kidogo, mpelekeeni mkuu wa meza.”Hivyo wakachota, wakampelekea. 9 Yule mkuu wa meza akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yamebadilika kuwa divai. Hakujua divai hiyo ilikotoka ingawa wale watumishi waliochota yale maji wao walifahamu. Basi akamwita bwana arusi kando 10 akamwambia, “Watu wote hutoa kwanza divai nzuri, kisha huleta ile divai hafifu wageni wakisha kunywa vya kutosha, lakini wewe umeiweka ile nzuri kupita zote mpaka sasa.” 11 Huu, ndio uliokuwa muujiza wa kwanza Yesu aliofanya Kana ya Galilaya. Hivyo Yesu alidhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. 12 Baada ya hayo, Yesu pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, walishuka mpaka Kapernaumu, wakakaa huko siku chache. 13 Ilipokaribia wakati wa Pasaka ya Wayahudi, Yesu alipanda kwenda Yerusalemu. 14 Huko Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ngʼombe, kondoo na njiwa, nao wengine walikuwa wameketi mezani wakibadili fedha. 15 Akatengeneza mjeledi kutokana na kamba, akawafukuza wote kutoka kwenye eneo la Hekalu, pamoja na kondoo na ngʼombe. Akazipindua meza za wale wabadili fedha na kuzimwaga fedha zao. 16 Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, “Waondoeni hapa! Mnathubutuje kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa biashara?” 17 Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa imeandikwa: “Wivu wa nyumba yako utanila.” 18 Ndipo Wayahudi wakamuuliza, “Unaweza kutuonyesha ishara gani ili kuthibitisha mamlaka uliyo nayo ya kufanya mambo haya?” 19 Yesu akawajibu, “Libomoeni hili Hekalu, nami nitalijenga tena kwa siku tatu!” 20 Wale Wayahudi wakamjibu, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita, nawe wasema utalijenga kwa siku tatu?” 21 Lakini yeye Hekalu alilozungumzia ni mwili wake. 22 Baada ya kufufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka yale aliyokuwa amesema. Ndipo wakayaamini Maandiko na yale maneno Yesu aliyokuwa amesema. 23 Ikawa Yesu alipokuwa Yerusalemu kwenye Sikukuu ya Pasaka, watu wengi waliona ishara na miujiza aliyokuwa akifanya, wakaamini katika jina lake. 24 Lakini Yesu hakujiaminisha kwao kwa sababu aliwajua wanadamu wote. 25 Hakuhitaji ushuhuda wa mtu yeyote kuhusu mtu, kwa kuwa alijua yote yaliyokuwa moyoni mwa mtu.
In Other Versions
John 2 in the ANGEFD
John 2 in the ANTPNG2D
John 2 in the AS21
John 2 in the BAGH
John 2 in the BBPNG
John 2 in the BBT1E
John 2 in the BDS
John 2 in the BEV
John 2 in the BHAD
John 2 in the BIB
John 2 in the BLPT
John 2 in the BNT
John 2 in the BNTABOOT
John 2 in the BNTLV
John 2 in the BOATCB
John 2 in the BOATCB2
John 2 in the BOBCV
John 2 in the BOCNT
John 2 in the BOECS
John 2 in the BOGWICC
John 2 in the BOHCB
John 2 in the BOHCV
John 2 in the BOHLNT
John 2 in the BOHNTLTAL
John 2 in the BOICB
John 2 in the BOILNTAP
John 2 in the BOITCV
John 2 in the BOKCV2
John 2 in the BOKHWOG
John 2 in the BOKSSV
John 2 in the BOLCB
John 2 in the BOLCB2
John 2 in the BOMCV
John 2 in the BONAV
John 2 in the BONCB
John 2 in the BONLT
John 2 in the BONUT2
John 2 in the BOPLNT
John 2 in the BOSCB
John 2 in the BOSNC
John 2 in the BOTLNT
John 2 in the BOVCB
John 2 in the BOYCB
John 2 in the BPBB
John 2 in the BPH
John 2 in the BSB
John 2 in the CCB
John 2 in the CUV
John 2 in the CUVS
John 2 in the DBT
John 2 in the DGDNT
John 2 in the DHNT
John 2 in the DNT
John 2 in the ELBE
John 2 in the EMTV
John 2 in the ESV
John 2 in the FBV
John 2 in the FEB
John 2 in the GGMNT
John 2 in the GNT
John 2 in the HARY
John 2 in the HNT
John 2 in the IRVA
John 2 in the IRVB
John 2 in the IRVG
John 2 in the IRVH
John 2 in the IRVK
John 2 in the IRVM
John 2 in the IRVM2
John 2 in the IRVO
John 2 in the IRVP
John 2 in the IRVT
John 2 in the IRVT2
John 2 in the IRVU
John 2 in the ISVN
John 2 in the JSNT
John 2 in the KAPI
John 2 in the KBT1ETNIK
John 2 in the KBV
John 2 in the KJV
John 2 in the KNFD
John 2 in the LBA
John 2 in the LBLA
John 2 in the LNT
John 2 in the LSV
John 2 in the MAAL
John 2 in the MBV
John 2 in the MBV2
John 2 in the MHNT
John 2 in the MKNFD
John 2 in the MNG
John 2 in the MNT
John 2 in the MNT2
John 2 in the MRS1T
John 2 in the NAA
John 2 in the NASB
John 2 in the NBLA
John 2 in the NBS
John 2 in the NBVTP
John 2 in the NET2
John 2 in the NIV11
John 2 in the NNT
John 2 in the NNT2
John 2 in the NNT3
John 2 in the PDDPT
John 2 in the PFNT
John 2 in the RMNT
John 2 in the SBIAS
John 2 in the SBIBS
John 2 in the SBIBS2
John 2 in the SBICS
John 2 in the SBIDS
John 2 in the SBIGS
John 2 in the SBIHS
John 2 in the SBIIS
John 2 in the SBIIS2
John 2 in the SBIIS3
John 2 in the SBIKS
John 2 in the SBIKS2
John 2 in the SBIMS
John 2 in the SBIOS
John 2 in the SBIPS
John 2 in the SBISS
John 2 in the SBITS
John 2 in the SBITS2
John 2 in the SBITS3
John 2 in the SBITS4
John 2 in the SBIUS
John 2 in the SBIVS
John 2 in the SBT
John 2 in the SBT1E
John 2 in the SCHL
John 2 in the SNT
John 2 in the SUSU
John 2 in the SUSU2
John 2 in the SYNO
John 2 in the TBIAOTANT
John 2 in the TBT1E
John 2 in the TBT1E2
John 2 in the TFTIP
John 2 in the TFTU
John 2 in the TGNTATF3T
John 2 in the THAI
John 2 in the TNFD
John 2 in the TNT
John 2 in the TNTIK
John 2 in the TNTIL
John 2 in the TNTIN
John 2 in the TNTIP
John 2 in the TNTIZ
John 2 in the TOMA
John 2 in the TTENT
John 2 in the UBG
John 2 in the UGV
John 2 in the UGV2
John 2 in the UGV3
John 2 in the VBL
John 2 in the VDCC
John 2 in the YALU
John 2 in the YAPE
John 2 in the YBVTP
John 2 in the ZBP