Job 25 (BOKCV)
1 Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu: 2 “Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu;yeye huthibitisha amani katika mbingu juu. 3 Je, majeshi yake yaweza kuhesabika?Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake? 4 Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi? 5 Ikiwa hata mwezi sio mwangavunazo nyota si safi machoni pake, 6 sembuse mtu ambaye ni funza:mwanadamu ambaye ni buu tu!”