Job 30 (BOKCV)

1 “Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki,watu ambao baba zao ningekataa kwa dharaukuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo. 2 Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu,kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia? 3 Wakiwa wamekonda kutokana na kupungukiwa na kwa njaa,walizurura usiku katika nchi kame iliyo ukiwa. 4 Katika vichaka walikusanya mimea ya chumvi,nacho chakula chao kilikuwa mizizi ya mti wa mfagio. 5 Walifukuzwa mbali na watu wao,wakipigiwa kelele kama wevi. 6 Walilazimika kuishi katika mikondo ya vijito vilivyokauka,kwenye majabali na mahandaki. 7 Kwenye vichaka walilia kama punda,na walijisongasonga pamoja kwenye vichaka. 8 Wao ni watoto wa wapumbavu wenye asili ya ubaya,waliofukuzwa watoke katika nchi. 9 “Nao sasa wana wao wananidhihaki katika nyimbo;nimekuwa kitu cha dhihaka kwao. 10 Wananichukia sana na kujitenga nami,wala hawasiti kunitemea mate usoni. 11 Sasa kwa kuwa Mungu ameilegeza kamba ya upinde wangu na kunitesa,wamekuwa huru kunitendea waonavyo. 12 Kuume kwangu kundi linashambulia;wao huitegea miguu yangu tanzi,na kunizingira. 13 Huizuia njia yangu,nao hufanikiwa katika kuniletea maafa,nami sina yeyote wa kunisaidia. 14 Wananijia kama watu wapitao katika ufa mpana;katikati ya magofu huja na kunishambulia. 15 Vitisho vimenifunika;heshima yangu imetoweshwa kama kwa upepo,salama yangu imetoweka kama wingu. 16 “Sasa maisha yangu yamefikia mwisho;siku za mateso zimenikamata. 17 Usiku mifupa yangu inachoma;maumivu yanayonitafuna hayatulii kamwe. 18 Kwa uwezo wake mkuu Mungu huwa kwangu kama nguo;hushikamana nami kama ukosi wa vazi langu. 19 Yeye amenitupa kwenye matope,nami nimekuwa kama mavumbi na majivu. 20 “Ee BWANA, ninakulilia wewe lakini hunijibu;ninasimama, nawe unanitazama tu. 21 Wewe unanigeukia bila huruma;unanishambulia kwa nguvu za mkono wako. 22 Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo;umenirusha huku na huko kwenye dhoruba kali. 23 Ninajua utanileta mpaka kifoni,mahali ambapo wenye uhai wote wamewekewa. 24 “Hakika hakuna yeyote amshambuliaye mhitaji,anapoomba msaada katika shida yake. 25 Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu?Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini? 26 Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia;nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja. 27 Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii;siku za mateso zinanikabili. 28 Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua;ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada. 29 Nimekuwa ndugu wa mbweha,rafiki wa mabundi. 30 Ngozi yangu imekuwa nyeusi nayo inachunika;mifupa yangu inaungua kwa homa. 31 Kinubi changu kimegeuka kuwa maombolezo,nayo filimbi yangu imekuwa sauti ya kilio.

In Other Versions

Job 30 in the ANGEFD

Job 30 in the ANTPNG2D

Job 30 in the AS21

Job 30 in the BAGH

Job 30 in the BBPNG

Job 30 in the BBT1E

Job 30 in the BDS

Job 30 in the BEV

Job 30 in the BHAD

Job 30 in the BIB

Job 30 in the BLPT

Job 30 in the BNT

Job 30 in the BNTABOOT

Job 30 in the BNTLV

Job 30 in the BOATCB

Job 30 in the BOATCB2

Job 30 in the BOBCV

Job 30 in the BOCNT

Job 30 in the BOECS

Job 30 in the BOGWICC

Job 30 in the BOHCB

Job 30 in the BOHCV

Job 30 in the BOHLNT

Job 30 in the BOHNTLTAL

Job 30 in the BOICB

Job 30 in the BOILNTAP

Job 30 in the BOITCV

Job 30 in the BOKCV2

Job 30 in the BOKHWOG

Job 30 in the BOKSSV

Job 30 in the BOLCB

Job 30 in the BOLCB2

Job 30 in the BOMCV

Job 30 in the BONAV

Job 30 in the BONCB

Job 30 in the BONLT

Job 30 in the BONUT2

Job 30 in the BOPLNT

Job 30 in the BOSCB

Job 30 in the BOSNC

Job 30 in the BOTLNT

Job 30 in the BOVCB

Job 30 in the BOYCB

Job 30 in the BPBB

Job 30 in the BPH

Job 30 in the BSB

Job 30 in the CCB

Job 30 in the CUV

Job 30 in the CUVS

Job 30 in the DBT

Job 30 in the DGDNT

Job 30 in the DHNT

Job 30 in the DNT

Job 30 in the ELBE

Job 30 in the EMTV

Job 30 in the ESV

Job 30 in the FBV

Job 30 in the FEB

Job 30 in the GGMNT

Job 30 in the GNT

Job 30 in the HARY

Job 30 in the HNT

Job 30 in the IRVA

Job 30 in the IRVB

Job 30 in the IRVG

Job 30 in the IRVH

Job 30 in the IRVK

Job 30 in the IRVM

Job 30 in the IRVM2

Job 30 in the IRVO

Job 30 in the IRVP

Job 30 in the IRVT

Job 30 in the IRVT2

Job 30 in the IRVU

Job 30 in the ISVN

Job 30 in the JSNT

Job 30 in the KAPI

Job 30 in the KBT1ETNIK

Job 30 in the KBV

Job 30 in the KJV

Job 30 in the KNFD

Job 30 in the LBA

Job 30 in the LBLA

Job 30 in the LNT

Job 30 in the LSV

Job 30 in the MAAL

Job 30 in the MBV

Job 30 in the MBV2

Job 30 in the MHNT

Job 30 in the MKNFD

Job 30 in the MNG

Job 30 in the MNT

Job 30 in the MNT2

Job 30 in the MRS1T

Job 30 in the NAA

Job 30 in the NASB

Job 30 in the NBLA

Job 30 in the NBS

Job 30 in the NBVTP

Job 30 in the NET2

Job 30 in the NIV11

Job 30 in the NNT

Job 30 in the NNT2

Job 30 in the NNT3

Job 30 in the PDDPT

Job 30 in the PFNT

Job 30 in the RMNT

Job 30 in the SBIAS

Job 30 in the SBIBS

Job 30 in the SBIBS2

Job 30 in the SBICS

Job 30 in the SBIDS

Job 30 in the SBIGS

Job 30 in the SBIHS

Job 30 in the SBIIS

Job 30 in the SBIIS2

Job 30 in the SBIIS3

Job 30 in the SBIKS

Job 30 in the SBIKS2

Job 30 in the SBIMS

Job 30 in the SBIOS

Job 30 in the SBIPS

Job 30 in the SBISS

Job 30 in the SBITS

Job 30 in the SBITS2

Job 30 in the SBITS3

Job 30 in the SBITS4

Job 30 in the SBIUS

Job 30 in the SBIVS

Job 30 in the SBT

Job 30 in the SBT1E

Job 30 in the SCHL

Job 30 in the SNT

Job 30 in the SUSU

Job 30 in the SUSU2

Job 30 in the SYNO

Job 30 in the TBIAOTANT

Job 30 in the TBT1E

Job 30 in the TBT1E2

Job 30 in the TFTIP

Job 30 in the TFTU

Job 30 in the TGNTATF3T

Job 30 in the THAI

Job 30 in the TNFD

Job 30 in the TNT

Job 30 in the TNTIK

Job 30 in the TNTIL

Job 30 in the TNTIN

Job 30 in the TNTIP

Job 30 in the TNTIZ

Job 30 in the TOMA

Job 30 in the TTENT

Job 30 in the UBG

Job 30 in the UGV

Job 30 in the UGV2

Job 30 in the UGV3

Job 30 in the VBL

Job 30 in the VDCC

Job 30 in the YALU

Job 30 in the YAPE

Job 30 in the YBVTP

Job 30 in the ZBP