Job 36 (BOKCV)
1 Elihu akaendelea kusema: 2 “Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyeshakwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu. 3 Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali,nami nitamhesabia haki Muumba wangu. 4 Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo;mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe. 5 “Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu;ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake. 6 Hawaachi waovu waendelee kuishi,bali huwapa walioteswa haki yao. 7 Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki;huwaketisha penye viti vya enzi pamoja na wafalmena kuwatukuza milele. 8 Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo,wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso, 9 huwaonyesha yale waliyoyatenda,kwamba wametenda dhambi kwa majivuno. 10 Huwafanya wao kusikia maonyo,na huwaagiza kutubu uovu wao. 11 Kama wakitii na kumtumikia,wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio,na miaka yao katika utoshelevu. 12 Lakini wasiposikiliza,wataangamia kwa upanga,nao watakufa pasipo maarifa. 13 “Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki;hata anapowafunga, hawamwombi msaada. 14 Wanakufa wangali vijana,miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu. 15 Bali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao,na kuzungumza nao katika dhiki zao. 16 “Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki,ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi,hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri. 17 Lakini sasa umelemewa na hukumu kwa ajili ya uovu;hukumu na haki vimekukamata. 18 Uwe mwangalifu ili yeyote asikushawishi kwa utajiri;usipotoshwe kwa fungu kubwa la rushwa. 19 Je, utajiri wako hata nguvu zako nyingivinaweza kukusaidia usiingie kwenye dhiki? 20 Usiutamani usiku uje,ili uwaburute watu mbali na nyumba zao. 21 Jihadhari usigeukie uovu,ambao unaupenda zaidi kuliko mateso. 22 “Mungu ametukuzwa katika nguvu zake.Ni nani aliye mwalimu kama yeye? 23 Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake,au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’? 24 Kumbuka kuzitukuza kazi zake,ambazo watu wamezisifu katika wimbo. 25 Wanadamu wote wameiona;watu wanaikazia macho kwa mbali. 26 Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu,kupita ufahamu wetu!Hesabu ya miaka yake haitafutiki. 27 “Yeye huvuta juu matone ya maji,ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito; 28 mawingu huangusha chini maji yake,nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu. 29 Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu,jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake. 30 Tazama jinsi anavyotandaza umeme wa radi kumzunguka,naye huvifunika vilindi vya bahari. 31 Hivi ndivyo atawalavyo mataifa,na kuwapa chakula kwa wingi. 32 Huujaza mkono wake kwa umeme wa radi,na kuuagiza kulenga shabaha yake. 33 Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja;hata mifugo hujulisha kukaribia kwake.
In Other Versions
Job 36 in the ANGEFD
Job 36 in the ANTPNG2D
Job 36 in the AS21
Job 36 in the BAGH
Job 36 in the BBPNG
Job 36 in the BBT1E
Job 36 in the BDS
Job 36 in the BEV
Job 36 in the BHAD
Job 36 in the BIB
Job 36 in the BLPT
Job 36 in the BNT
Job 36 in the BNTABOOT
Job 36 in the BNTLV
Job 36 in the BOATCB
Job 36 in the BOATCB2
Job 36 in the BOBCV
Job 36 in the BOCNT
Job 36 in the BOECS
Job 36 in the BOGWICC
Job 36 in the BOHCB
Job 36 in the BOHCV
Job 36 in the BOHLNT
Job 36 in the BOHNTLTAL
Job 36 in the BOICB
Job 36 in the BOILNTAP
Job 36 in the BOITCV
Job 36 in the BOKCV2
Job 36 in the BOKHWOG
Job 36 in the BOKSSV
Job 36 in the BOLCB
Job 36 in the BOLCB2
Job 36 in the BOMCV
Job 36 in the BONAV
Job 36 in the BONCB
Job 36 in the BONLT
Job 36 in the BONUT2
Job 36 in the BOPLNT
Job 36 in the BOSCB
Job 36 in the BOSNC
Job 36 in the BOTLNT
Job 36 in the BOVCB
Job 36 in the BOYCB
Job 36 in the BPBB
Job 36 in the BPH
Job 36 in the BSB
Job 36 in the CCB
Job 36 in the CUV
Job 36 in the CUVS
Job 36 in the DBT
Job 36 in the DGDNT
Job 36 in the DHNT
Job 36 in the DNT
Job 36 in the ELBE
Job 36 in the EMTV
Job 36 in the ESV
Job 36 in the FBV
Job 36 in the FEB
Job 36 in the GGMNT
Job 36 in the GNT
Job 36 in the HARY
Job 36 in the HNT
Job 36 in the IRVA
Job 36 in the IRVB
Job 36 in the IRVG
Job 36 in the IRVH
Job 36 in the IRVK
Job 36 in the IRVM
Job 36 in the IRVM2
Job 36 in the IRVO
Job 36 in the IRVP
Job 36 in the IRVT
Job 36 in the IRVT2
Job 36 in the IRVU
Job 36 in the ISVN
Job 36 in the JSNT
Job 36 in the KAPI
Job 36 in the KBT1ETNIK
Job 36 in the KBV
Job 36 in the KJV
Job 36 in the KNFD
Job 36 in the LBA
Job 36 in the LBLA
Job 36 in the LNT
Job 36 in the LSV
Job 36 in the MAAL
Job 36 in the MBV
Job 36 in the MBV2
Job 36 in the MHNT
Job 36 in the MKNFD
Job 36 in the MNG
Job 36 in the MNT
Job 36 in the MNT2
Job 36 in the MRS1T
Job 36 in the NAA
Job 36 in the NASB
Job 36 in the NBLA
Job 36 in the NBS
Job 36 in the NBVTP
Job 36 in the NET2
Job 36 in the NIV11
Job 36 in the NNT
Job 36 in the NNT2
Job 36 in the NNT3
Job 36 in the PDDPT
Job 36 in the PFNT
Job 36 in the RMNT
Job 36 in the SBIAS
Job 36 in the SBIBS
Job 36 in the SBIBS2
Job 36 in the SBICS
Job 36 in the SBIDS
Job 36 in the SBIGS
Job 36 in the SBIHS
Job 36 in the SBIIS
Job 36 in the SBIIS2
Job 36 in the SBIIS3
Job 36 in the SBIKS
Job 36 in the SBIKS2
Job 36 in the SBIMS
Job 36 in the SBIOS
Job 36 in the SBIPS
Job 36 in the SBISS
Job 36 in the SBITS
Job 36 in the SBITS2
Job 36 in the SBITS3
Job 36 in the SBITS4
Job 36 in the SBIUS
Job 36 in the SBIVS
Job 36 in the SBT
Job 36 in the SBT1E
Job 36 in the SCHL
Job 36 in the SNT
Job 36 in the SUSU
Job 36 in the SUSU2
Job 36 in the SYNO
Job 36 in the TBIAOTANT
Job 36 in the TBT1E
Job 36 in the TBT1E2
Job 36 in the TFTIP
Job 36 in the TFTU
Job 36 in the TGNTATF3T
Job 36 in the THAI
Job 36 in the TNFD
Job 36 in the TNT
Job 36 in the TNTIK
Job 36 in the TNTIL
Job 36 in the TNTIN
Job 36 in the TNTIP
Job 36 in the TNTIZ
Job 36 in the TOMA
Job 36 in the TTENT
Job 36 in the UBG
Job 36 in the UGV
Job 36 in the UGV2
Job 36 in the UGV3
Job 36 in the VBL
Job 36 in the VDCC
Job 36 in the YALU
Job 36 in the YAPE
Job 36 in the YBVTP
Job 36 in the ZBP