Job 38 (BOKCV)

1 Kisha BWANA akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema: 2 “Nani huyu atiaye mashauri yangu gizakwa maneno yasiyo na maarifa? 3 Jikaze kama mwanaume;nitakuuliza swali,nawe unijibu. 4 “Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia?Niambie, kama unafahamu. 5 Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake?Hakika wewe unajua!Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake? 6 Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini,au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni, 7 wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,na malaika wote walipokuwa wakipiga kelele kwa furaha? 8 “Ni nani aliyeifungia bahari milangoilipopasuka kutoka tumbo, 9 nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake,na kuyafungia katika giza nene, 10 nilipoamuru mipaka yake,na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake, 11 niliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi;hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’? 12 “Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke,au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake, 13 yapate kushika miisho ya dunia,na kuwakungʼuta waovu waliomo? 14 Dunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya lakiri;sura yake hukaa kama ile ya vazi. 15 Waovu huzuiliwa nuru yao,nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa. 16 “Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari?Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi? 17 Umewahi kuonyeshwa malango ya mauti?Umewahi kuiona milango ya uvuli wa mauti? 18 Je, wewe unafahamu ukubwa wa dunia?Niambie kama unajua haya yote. 19 “Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi?Nako maskani mwa giza ni wapi? 20 Je, unaweza kuvirudisha kwenye makao yake?Unajua njia za kufika maskani mwake? 21 Hakika unajua, kwa kuwa ulikuwa umeshazaliwa!Kwani umeishi miaka mingi! 22 “Je, umeshawahi kuingia katika ghala za theluji,au kuona ghala za mvua ya mawe, 23 ambazo nimeziweka akiba kwa ajili ya wakati wa taabu,na kwa ajili ya wakati wa vita na mapigano? 24 Ni ipi njia iendayo mahali umeme wa radi unapotawanyiwa,au mahali upepo wa mashariki unaposambaziwa juu ya dunia? 25 Ni nani aliyepasua mifereji kwa ajili ya maji mengi ya mvua yaendayo kasina njia ya umeme wa radi, 26 ili kusababisha mvua kunyeshea mahali pasipokaliwa na mtu,jangwa lisilo na yeyote ndani yake, 27 ili kuitosheleza nchi ya ukiwa na jangwa,na majani yaanze kumea ndani yake? 28 Je, mvua ina baba?Ni nani baba azaaye matone ya umande? 29 Barafu inatoka tumbo la nani?Ni nani azaaye ukungu kutoka mbinguni, 30 wakati maji yawapo magumu kama jiwe,wakati uso wa vilindi vya maji unapoganda? 31 “Je, waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia?Waweza kulegeza kamba za Orioni? 32 Waweza kuyaongoza makundi ya nyota kwa majira yake,au kuongoza Dubu na watoto wake? 33 Je, unajua sheria zinazotawala mbingu?Waweza kuweka utawala wa Mungu duniani? 34 “Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni,na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji? 35 Je, wewe hutuma umeme wa radi kwenye njia zake?Je, hutoa taarifa kwako kukuambia, ‘Sisi tuko hapa’? 36 Ni nani aliyeujalia moyo hekimaau kuzipa akili ufahamu? 37 Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu?Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni 38 wakati mavumbi yawapo magumu,na mabonge ya udongo kushikamana pamoja? 39 “Je, utamwindia simba jike mawindo,na kuwashibisha simba wenye njaa 40 wakati wao wamejikunyata mapangoni mwao,au wakivizia kichakani? 41 Ni nani ampaye kunguru chakulawakati makinda yake yanamlilia Mungu,yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula?

In Other Versions

Job 38 in the ANGEFD

Job 38 in the ANTPNG2D

Job 38 in the AS21

Job 38 in the BAGH

Job 38 in the BBPNG

Job 38 in the BBT1E

Job 38 in the BDS

Job 38 in the BEV

Job 38 in the BHAD

Job 38 in the BIB

Job 38 in the BLPT

Job 38 in the BNT

Job 38 in the BNTABOOT

Job 38 in the BNTLV

Job 38 in the BOATCB

Job 38 in the BOATCB2

Job 38 in the BOBCV

Job 38 in the BOCNT

Job 38 in the BOECS

Job 38 in the BOGWICC

Job 38 in the BOHCB

Job 38 in the BOHCV

Job 38 in the BOHLNT

Job 38 in the BOHNTLTAL

Job 38 in the BOICB

Job 38 in the BOILNTAP

Job 38 in the BOITCV

Job 38 in the BOKCV2

Job 38 in the BOKHWOG

Job 38 in the BOKSSV

Job 38 in the BOLCB

Job 38 in the BOLCB2

Job 38 in the BOMCV

Job 38 in the BONAV

Job 38 in the BONCB

Job 38 in the BONLT

Job 38 in the BONUT2

Job 38 in the BOPLNT

Job 38 in the BOSCB

Job 38 in the BOSNC

Job 38 in the BOTLNT

Job 38 in the BOVCB

Job 38 in the BOYCB

Job 38 in the BPBB

Job 38 in the BPH

Job 38 in the BSB

Job 38 in the CCB

Job 38 in the CUV

Job 38 in the CUVS

Job 38 in the DBT

Job 38 in the DGDNT

Job 38 in the DHNT

Job 38 in the DNT

Job 38 in the ELBE

Job 38 in the EMTV

Job 38 in the ESV

Job 38 in the FBV

Job 38 in the FEB

Job 38 in the GGMNT

Job 38 in the GNT

Job 38 in the HARY

Job 38 in the HNT

Job 38 in the IRVA

Job 38 in the IRVB

Job 38 in the IRVG

Job 38 in the IRVH

Job 38 in the IRVK

Job 38 in the IRVM

Job 38 in the IRVM2

Job 38 in the IRVO

Job 38 in the IRVP

Job 38 in the IRVT

Job 38 in the IRVT2

Job 38 in the IRVU

Job 38 in the ISVN

Job 38 in the JSNT

Job 38 in the KAPI

Job 38 in the KBT1ETNIK

Job 38 in the KBV

Job 38 in the KJV

Job 38 in the KNFD

Job 38 in the LBA

Job 38 in the LBLA

Job 38 in the LNT

Job 38 in the LSV

Job 38 in the MAAL

Job 38 in the MBV

Job 38 in the MBV2

Job 38 in the MHNT

Job 38 in the MKNFD

Job 38 in the MNG

Job 38 in the MNT

Job 38 in the MNT2

Job 38 in the MRS1T

Job 38 in the NAA

Job 38 in the NASB

Job 38 in the NBLA

Job 38 in the NBS

Job 38 in the NBVTP

Job 38 in the NET2

Job 38 in the NIV11

Job 38 in the NNT

Job 38 in the NNT2

Job 38 in the NNT3

Job 38 in the PDDPT

Job 38 in the PFNT

Job 38 in the RMNT

Job 38 in the SBIAS

Job 38 in the SBIBS

Job 38 in the SBIBS2

Job 38 in the SBICS

Job 38 in the SBIDS

Job 38 in the SBIGS

Job 38 in the SBIHS

Job 38 in the SBIIS

Job 38 in the SBIIS2

Job 38 in the SBIIS3

Job 38 in the SBIKS

Job 38 in the SBIKS2

Job 38 in the SBIMS

Job 38 in the SBIOS

Job 38 in the SBIPS

Job 38 in the SBISS

Job 38 in the SBITS

Job 38 in the SBITS2

Job 38 in the SBITS3

Job 38 in the SBITS4

Job 38 in the SBIUS

Job 38 in the SBIVS

Job 38 in the SBT

Job 38 in the SBT1E

Job 38 in the SCHL

Job 38 in the SNT

Job 38 in the SUSU

Job 38 in the SUSU2

Job 38 in the SYNO

Job 38 in the TBIAOTANT

Job 38 in the TBT1E

Job 38 in the TBT1E2

Job 38 in the TFTIP

Job 38 in the TFTU

Job 38 in the TGNTATF3T

Job 38 in the THAI

Job 38 in the TNFD

Job 38 in the TNT

Job 38 in the TNTIK

Job 38 in the TNTIL

Job 38 in the TNTIN

Job 38 in the TNTIP

Job 38 in the TNTIZ

Job 38 in the TOMA

Job 38 in the TTENT

Job 38 in the UBG

Job 38 in the UGV

Job 38 in the UGV2

Job 38 in the UGV3

Job 38 in the VBL

Job 38 in the VDCC

Job 38 in the YALU

Job 38 in the YAPE

Job 38 in the YBVTP

Job 38 in the ZBP