Psalms 101 (BOKCV)
undefined Zaburi ya Daudi. 1 Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako;kwako wewe, Ee BWANA, nitaimba sifa. 2 Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama:utakuja kwangu lini? Nitatembea nyumbani mwangukwa moyo usio na lawama. 3 Sitaweka mbele ya macho yangukitu kiovu. Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani;hawatashikamana nami. 4 Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami;nitajitenga na kila ubaya. 5 Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri,huyo nitamnyamazisha;mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburihuyo sitamvumilia. 6 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,ili waweze kuishi pamoja nami;yeye ambaye moyo wake hauna lawamaatanitumikia. 7 Mdanganyifu hatakaanyumbani mwangu,yeye asemaye kwa uongohatasimama mbele yangu. 8 Kila asubuhi nitawanyamazishawaovu wote katika nchi;nitamkatilia mbali kila mtenda mabayakutoka mji wa BWANA.